Papa Leo XIV:tutazame maisha yetu kama safari ya kumfuata Yesu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Maria ni msindikizaji katika safari ya kwenda kwa Yesu. Kwa uhakika huu Baba Mtakatifu Leo XIV alituhimiza tusali kwa Bwana kwa sifa kila siku. Alisisitiza hayo usiku wa tarehe 31 Mei 2025 kwenye Grotto ya Lourdes katika bustani ya Vatican, katika tafakari yake fupi iliyotolewa kwa waamini walioshiriki, kwa mujibu wa mapokeo, katika Rozari Takatifu mwishoni mwa mwezi Mei, iliyowekwa kwa Bikira. Sala hiyo iliyoongozwa na Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na Makamu wa Papa kwa ajili ya mji wa Vatican, iliyoanza saa 2:00 usiku masaa ya Ulaya.
Kwa Waamini wapatao elfu mbili walitaka kushiriki katika maombi hayo. Kulikuwa na Makardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Makardinali, Lazzaro You Heung-sik, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makleri, Giuseppe Versaldi, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki. Na kisha maaskofu, watu waliowekwa wakfu, paroko wa Basilika ya Vatican , familia nyingi, vijana, wazee, na watu wa kujitolea wa Unitalsi walioanzi maandamano katika Kanisa la Mtakatifu Stefano wa Abissini hadi uwazi ambapo ni mahali pa ukumbusho wa tokeo la Maria kwa Bernadette.
Baba Mtakatifu Leo XIV akianza alisema kuwa "kwa furaha naungana nanyi katika Mkesha huu wa Maombi mwishoni mwa Mwezi wa Mei. Ni ishara ya imani ambayo kwayo tunakusanyika kwa njia rahisi na ya kujitolea chini ya vazi la uzazi la Maria. Mwaka huu, basi, unakumbuka baadhi ya vipengele muhimu vya Jubilei tunayoadhimisha: sifa, safari, matumaini na, zaidi ya yote, imani iliyotafakariwa na kudhihirika pamoja. Akigusia rozari Takatifu ambayo tayari waamini walimaliza kusali kwa pamoja aliongeza kuwa sala, kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyosisitiza, kwa uhalisi wa Maria na moyo wa Kikristo, ambao unazingatia ndani yenyewe undani wa ujumbe wote wa Kiinjili" (Waraka wa Kitume Rosarium Virginis Mariae, 16 Oktoba 2002, 1).
Na kiukweli, ukitafakari juu ya Mafumbo ya Furaha, wakati wa safari mliyofanya na kusimama,kana kwamba kwenye safari ni katika sehemu nyingi za maisha ya Yesu: katika nyumba ya Nazareti kutafakari Matamshi, katika yale ya Zakaria, kutafakari Kutembelewa - ambayo tunasherehekea leo ikiwa na maana tarehe 31 Mei 2025, katika Groto ya kutafakari: Hekalu la Bethlehemu, kisha Noeli katika hekalu la Bethlehem, kupatikana kwa Yesu. Wakati wa kutembea mlisali Salamu Maria iiliyorudiwa kwa imani, ambayo ni maneno ya Malaika kwa Mama wa Mungu: Salamu, umejaa neema, Bwana yu pamoja nawe" (Lk 1:28) na kwa Elizabeti anayemkaribisha kwa furaha akisema: "Umebarikiwa wewe katika wanawake, na mzao wa tumbo lako amebarikiwa!" (Lk 1:42). Kwa kuongezea, Papa Leo XI V alisema hatua za waamini siku hiyo kwa hiyo zimetiwa alama na Neno la Mungu, ambalo limetia alama, kwa mdundo wake, maendeleo yao, vituo vyao na kuondoka kwao, kama vile watu wa Israeli jangwani, katika safari yao kuelekea Nchi ya Ahadi.
Basi, Papa aliongeza “na tutazame maisha yetu kama safari ya kumfuata Yesu, ya kufuatwa, kama tulivyofanya jioni ya leo, pamoja na Maria.” Na tumwombe Bwana kujua jinsi ya kumsifu kila siku, "kwa uzima na kwa ulimi, kwa moyo na kwa midomo, kwa sauti na kwa mwenendo" (Mtakatifu Agostino, Hotuba 256, 1), kuepuka mafarakano: ulimi unaofanana na maisha na midomo kwa dhamiri. Papa Leo XIV alitoa salamu zake kwa Makardinali waliokuwapo, Maaskofu, mapadre, watu waliowekwa wakfu na waamini wote. Alipenda kueleza, hasa, upendo na shukrani kwa Masista Wabenediktini wa Monasteri ya Mater Ecclesiae(Hawa wamo ndani ya mji wa Vatican) ambao kwa maombi yao yaliyofichika na ya kudumu wanaunga mkono jumuiya yetu na kazi yetu.” Furaha ya wakati huu ibaki na kukua ndani yetu, “katika maisha yetu binafsi na ya kifamilia, katika kila mazingira, hasa katika maisha ya familia hii ambayo hapa Vatican inalihudumia Kanisa la kiulimwengu” (Benedikto XVI, Hitimisho la mwezi wa Mei, 31 Mei 2012). Bwana atubariki na atusindikize daima na Maria atuombee. Asante!”
Hata hivyo wakati wa kumsubiri Baba Mtakatifu afike, Kardinali Gambetti, aliwaalika kufurahi kama vile moyo wa Maria ulivyoruka kwa tangazo la Malaika. Hivi ndivyo tunapaswa kujibu, alisema, vinginevyo tuna hatari ya kutoikaribisha neema. Tunapaswa kujibu shalom. Na pia alikumbuka kipindi cha kibinafsi cha wakati, akirudi kutoka Lourdes, baada ya kuwa amepewa fursa ya kufanya uzoefu katika eneo hilo takatifu alitambua kwa undani jinsi Bikira alivyomtendea Bernadette, msichana maskini, kwa heshima kamili, akimtambulisha kwa njia ya kuzaliwa upya. Mwanga wa mishumaa ulionesha uzuri wa Bustani, mwishoni mwa siku iliyojaa jua.