MAP

2025.06.06Papa akutana na Mashirika matatu katika fursa ya ushiriki wao wa Mkutano wao Mkuu wa Mwaka. 2025.06.06Papa akutana na Mashirika matatu katika fursa ya ushiriki wao wa Mkutano wao Mkuu wa Mwaka.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa Mashirika 3 ya kitawa:dhamira ya uongofu,ari ya utume na joto la huruma!

Papa Leo XIV alikutana Ijumaa tarehe 6 Juni 2025 na wawakilishi wa mashirika matatu yaliyoanzishwa kwa karne tofauti.Papa aliakisi uzuri wa Kanisa,ambao wanauonesha kupitia karama zao mbalimbali na utume wa kitume.Papa amewaalika kukumbatia upumbavu wa Msalaba,hata katikati ya kutoelewana na dhihaka ya ulimwengu.Kisha anlimtaja Mtakatifu Agostino na dawa yake ya uovu kuwa ni msamaha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Wawakilishi wa Mashirika Matatu  yaliyoanzishwa kwa karne nane zilizopita tarehe 6 Juni 2025 ambayo  ni Shirika la Misheni za Afrika, Daraja la Tatu la Mtakatifu Francis na Watumishi wa Roho ya Uponyaji.  Papa alianza hotuba yake alieleza kuwa wengi wao  walifika kwenye  mkutano katika muktadha wa Mkutano wao mkuu, wakati muhimu katika maisha yao na katika yale ya Kanisa zima. Basi tuombe kwanza kwa Bwana kwa ajili ya Taasisi zao na watu wote waliowekwa wakfu, ili kwa mtazamo yao pekee na zaidi ya yote kwa Mungu, waunganishe kutafakari, ambayo kwayo wanashikamana na Mungu kwa akili na moyo, kwa bidii ya kitume, ambayo wanajitahidi kushirikiana nayo katika kazi ya ukombozi”(Perfectae caritatis, 5). Papa Leo alisisitiza kwamba wao waliwakilisha hapo mambo matatu ya kweli ya karama zilizozaliwa kwa nyakati tofauti katika historia ya Kanisa, kwa kukabiliana na mahitaji ya aina mbalimbali, lakini yenye umoja na yanayosaidiana katika uzuri wa upatano wa Mwili wa Fumbo wa Kristo (taz. Lumen gentium, 7).

Papa akutana na mashirika matatu ya kitawa
Papa akutana na mashirika matatu ya kitawa   (@VATICAN MEDIA)

Akianza na la zamani, Papa alisema Shirika la  kizamani zaidi ya waliokuwapo ni la Daraja  la Tatu la Kawaida la Mtakatifu Francis ambalo mwanzo wake ulianzia kwa  Mtakatifu wa Assisi mwenyewe, isipokuwa kwa kuinuliwa kuwa shirika  lililotokea baadaye na Papa Nicholas V (taz. Pastoralis officii, 20 Julai 1447).  Mada wazozungumzia katika Mkutano Mkuu 113 ilihusu “maisha ya pamoja, malezi na miito” kwamba  zinahusu kidogo Familia kuu ya Mungu. Ni muhimu, hata hivyo, kwamba, kama mada waliyojikita nayo kwa kazi zao kama wasemavyo, waziendeleze katika mwanga wa karama yao ya "kutubu." Hii kiukweli inatukumbusha kwamba,  kulingana na maneno yenyewe ya Mtakatifu Francis - kupitia safari ya mara kwa mara ya uongofu tunaweza kutoa ndugu zetu tu  "maneno yenye harufu nzuri ya Bwana wetu Yesu Kristo" (Barua ya Kwanza kwa Waamini, 19).

Kwa upande wa Shirika la Misheni za Kiafrika

Baba Mtakatifu Leo XIV aidha aligeukia shirika jingine kuwa “la hivi karibuni  zaidi ni Shirika la Misheni za Kiafrika, lililoanzishwa tarehe 8 Desemba 1856 na Mhashamu Askofu Melchior de Marion Brésillac, ishara ya roho ya kimisionari ambayo ndiyo kiini cha maisha ya Kanisa (taz. Evangelii gaudium, 273). Historia ya Taasisi yao, ndugu wapendwa, inashuhudia ukweli huu: uaminifu kwa utume, kwa hakika, kwa kukufanya washinde matatizo mengi ndani na nje ya jumuiya yao kwa muda, kumekuwezesha kukua, kwa kweli kuchota kutoka katika dhiki fursa na msukumo wa kuanza kuelekea katika upeo mpya wa kitume barani Afrika na kisha sehemu nyingine za dunia. Katika suala hili, himizo lililoachiwa kwao na Mwanzilishi ni nzuri: kubaki waaminifu, katika tangazo, kwa usahili wa mahubiri ya kitume na, wakati huo huo, daima tayari kukumbatia “upumbavu wa Msalaba”(taz. 1Kor 1:17-25): rahisi na utulivu, hata katika hali ya kutoelewana na dhihaka ya ulimwengu. Papa Leo XIV aliongeza kusema kuwa kuwa huru kutokana na hali yoyote kwa sababu "wamejazwa" na Kristo, na uwezo wa kuwaleta ndugu kwenye kukutana Naye kwa sababu ya kuhuishwa na shauku moja: kutangaza Injili yake kwa ulimwengu wote (taz. Flp 1:12-14.21). Ni ishara kuu iliyoje kwa Kanisa zima na kwa ulimwengu wote!

Papa akutana na mashirika matatu ya kitawa
Papa akutana na mashirika matatu ya kitawa   (@Vatican Media)

Shirika la Watumishi wa Roho Mponyaji

Hatimaye Baba Mtakatifu Leo XIV aliwatazama Taasisi iliyoanzishwa hivi karibuni: Watumishi wa Roho Mponyaji. Watumishi wa Roho huyo anayekaa ndani yetu (Rm 8:9) kupitia karama ya Ubatizo na anayeponya “quod est saucium,” yaani, kile kilichojeruhiwa” - kama tutakavyoimba katika siku chache katika Sala ya Pentekoste. Watumishi wa Roho ya Uponyaji: hivi ndivyo Padre Gerald Fitzgerald alitaka wawe, ambaye mwaka 1942 alianza kazi yenu ya kuwatunza mapadre kwa shida, “Pro Christo prete,” kama kauli mbiu yenu inavyosema (taz. Katiba, 4,4). Tangu wakati huo, wametekeleza, katika sehemu mbalimbali za dunia, huduma yao ya ukaribu, unyenyekevu, uvumilivu, unyeti na wa busara na watu waliojeruhiwa sana, wakiwapa njia za matibabu zinazo changanya maisha rahisi na makali ya kiroho, ya kibinafsi na ya kijamii pamoja na usaidizi wa kitaaluma uliohitimu sana, unaotofautishwa kulingana na mahitaji yao. Uwepo wao pia unatukumbusha jambo muhimu: kwamba sisi sote, ingawa tumeitwa kuwa wahudumu wa Kristo, tabibu wa roho, kwa ajili ya kaka na dada zetu (taz. Lk 5:31-32), kwanza kabisa ni wagonjwa wanaohitaji kuponywa. Kama Mtakatifu Agostino anavyosema, kwa kutumia mfano wa mtumbwi, sisi sote "katika maisha haya tuna nyufa ambazo ni maalum kwa maisha yetu ya kufa na udhaifu, ambayo dhambi huingia kutoka katika mawimbi ya karne hii"(Mahubiri 278, 13,13).

Papa akutana na mashirika matatu ya kitawa
Papa akutana na mashirika matatu ya kitawa   (@Vatican Media)

Na Askofu Mtakatifu wa Hippo alipendekeza suluhisho la uovu: "Kujiondoa wenyewe na sio kuzama," alisema, "tuchukue ... himizo hili ... na tusamehe!"(ibid.) Hebu tusamehe, kwa sababu kila mahali, “katika parokia zetu, katika jumuiya, katika vyama na harakati, kwa ufupi, popote palipo na Wakristo, mtu yeyote (…) (anaweza) kupata chemchemi ya huruma” (Papa Francisko: Misericordiae Vultus, 11 Aprili 2015, 12). Papa alihitimisha kwa kuwashukuru, ambayo leo katika ukumbi huo imeonesha Kanisa katika nyanja tatu za uzuri wake: dhamira ya uongofu, ari ya utume na joto la huruma. Asante kwa kazi yote unayofanya, ulimwenguni kote. Ninawabariki na kuwaombea, katika novena hii ya Pentekoste, ili mzidi kuwa vyombo vya Roho Mtakatifu kulingana na mipango ya Mungu. Asante.

06 Juni 2025, 16:50