Zawadi ya Papa ya keki ya furaha ya Mtakatifu Agostino
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Zawadi tamu na ya kukaribishwa sana ilitolewa katika kwa Baba Mtakatifu Leo XIV ambayo ni "Keki ya Furaha" ya Mtakatifu Augostino, kama iitwavyo. Ni keki iliyotengenezwa kwa unga wa nafaka tatu na asali, ambayo viungo vyake vimetiwa msukumo na Askofu wa Hippo(mtakatifu Agostino) mwenyewe katika moja ya mijadala yake, kwenye kazi ya maandishi ya: "De beata vita", miongoni mwa mambo mengine ni kazi inayohusu mada ya furaha. Kwa hivyo ndipo linapotoka jina la keki hiyo keki ya furaha. Rafiki wa zamani wa Papa Leo aliitayarisha kwa ajili ya Papa na hivyo aliifunga na kuituma kwa Papa Leo XIV kwenye hafla ya kumbukizi ya Mtakatifu Rita. Papa alifurahia jambo hilo kwa furaha pamoja na ndugu zake na katibu wake wa kibinafsi.
Maandalizi na mapishi yaliyoagizwa na Mtakatifu Agostino
Aina hii ya keki, ya kuliwa ikiwa baridi, ilizaliwa kama jaribio kaskazini mwa Italia, hasa katika manispaa ya Cassago Brianza, ambapo Agostino aliandika kazi yake ya De beata vita. Katika kazi hii Mtakatifu Agostino anasimulia siku ya kuzaliwa kwake 32, mnamo Novemba 13, ambapo alisherehekea na chakula cha mchana pamoja na mtoto wake Adeodato, mama yake Monica, kaka yake Navigio, binamu zake Rustico na Lastidiano na wanafunzi wake Licenzio na Trigezio. "Nadhani ninapaswa kutoa chakula cha mchana kwa siku yangu ya kuzaliwa zaidi sio tu kwa mwili wetu, bali pia kwa roho," Mtakatifu Agostino aliwaambia wageni.