Tarehe 17 Juni,Papa Leo XIV atakutana na Baraza la Maaskofu wa Italia
Vatican News.
Tarehe 17 Juni 2025, Baba Leo XIV atakutana na Baraza la Maaskofu wa Italia katika Mkutano, katika Ukumbi wa Paulo VI, saa 4.00 asubuhi. Hii ilitangazwa na CEI yenyewe kupitia njia zake rasmi. "Tunamshukuru Baba Mtakatifu kwa ishara hii ya ukarimu na umakini kwa Uaskofu wa Italia ambao unaishi maelewano ya kipekee na ya upendo na Mrithi wa Petro, Askofu wa Roma na Mkuu wa Italia," alisisitiza katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Askofu Giuseppe Baturi. Mkutano huo utafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 80 usio wa kawaida kwa baadhi ya majukumu ya kisheria.
Baraza la Maaskofu la Kudumu
Jumanne, tarehe 27 Mei 2025 kuanzia saa 4:30 asubuhi majiara ya Ulaya hadi 10:30, jioni jijini Roma, katika makao makuu ya CEI yaliyoko njia ya Circonvallazione Aurelia 50, Baraza la Kudumu la Maaskofu (CEI) litakutana katika kikao kisicho rasimi. Baada ya Utangulizi wa Kardinali Matteo Zuppi, Askofu Mkuu wa Bologna na Rais wa CEI, hatua zitakazofuata za Njia ya Sinodi zitaoneshwa, kwa maandalizi ya Mkutano wa Tatu wa Sinodi. Wakati wa kazi hizo, Ujumbe wa Siku ya 75 kutoa Shukrani kwa Mungu ya Kitaifa, ambayo itaadhimishwa Novemba 9 ijayo pia utaidhinishwa.