ĐÓMAPµĽş˝

Kupapa Bwana ni Sherehe inayowakirimia waamini mang’amuzi yanayopyaisha matumaini na furaha, tayari kujizatiti katika kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo Yesu kwa uaminifu, nguvu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Kupapa Bwana ni Sherehe inayowakirimia waamini mang’amuzi yanayopyaisha matumaini na furaha, tayari kujizatiti katika kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo Yesu kwa uaminifu, nguvu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu. 

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni: Siku ya 59 Ya Upashanaji Habari Kwa Mwaka 2025

Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 28 Mei 2025 amewatia shime waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Habari Njema ya Wokovu kama ilivyokuwa kwa Mitume wa Kristo Yesu. Iwe ni Sherehe inayowakirimia waamini mang’amuzi yanayopyaisha matumaini na furaha, tayari kujizatiti katika kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo Yesu kwa uaminifu, nguvu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mama Kanisa anasadiki na kufundisha kwamba, Kristo Yesu baada ya kusema nao, akachukuliwa mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Mwili wa Kristo ulitukuzwa wakati ule ule alipofufuka kama zinavyoshuhudia hali mpya na za kimungu ambazo tokea hapo umebaki nazo daima. Lakini kile kipindi cha siku arobaini ambako alizoea kula na kunywa pamoja na wafuasi wake, na kuwafundisha juu ya Ufalme wa mbinguni, utukufu wake bado ulifunikwa na alama za ubinadamu wa kawaida. Tokeo la mwisho la Yesu linakamilika na kuingia bila kurudi kwa ubinadamu wake katika utukufu wa Mungu uliojionesha katika sura ya wingu na mbingu (Lk 24:51) ambako tangu hapo ameketi kuume kwa Mungu. Kwa namna moja tofauti kabisa na ya pekee atajionesha kwa Paulo “kama mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake” katika tokeo la mwisho lililomfanya kuwa Mtume. Hali iliyofunikwa ya utukufu wa Kristo Mfufuka kipindi hiki inaonekana katika maneno yake ya fumbo kwa Mariamu Magdalena: “Sijapata kwenda kwa Baba.Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninapaa kwenda kwa Baba yangu, naye ni Baba yenu.” Hii inaonesha tofauti ya kujidhihirisha kati ya utukufu wa Kristo Mfufuka na ule wa Kristo aliyetukuzwa kuume kwa Baba. Tukio ambalo kwa upande mmoja ni la kihistoria na bora sana linaloonesha kupita toka upande mmoja kwenda upande mwingine. Lakini yote yanabaki yakiwa yameungana kabisa na lile la kwanza yaani kushuka kutoka mbinguni kulikotekelezwa katika Fumbo la Umwilisho. Ubinadamu ukiachiwa katika nguvu zake za maumbile hauwezi kufika kwenye nyumba ya Baba. Kristo Yesu peke yake ameweza kumfungulia mtu njia hii “ili tukae tukiamini kwamba sisi tulio viungo vyake ametutangulia huko aliko Yeye aliye kichwa chetu na shina letu na kwamba, akiisha inuliwa juu ya nchi atawavuta wote kwake!

Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema
Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema   (ANSA)

Huku ni kuinuliwa juu ya Msalaba ambako huonesha na kutangaza kuinuliwa kwa kupaa mbinguni. Huo ndio mwanzo wake. Mbinguni Kristo Yesu anatekeleza Ukuhani wake daima, Yeye ni kiini na mtendaji mkuu wa Liturujia inayomheshimu Baba wa mbinguni. Kristo Yesu ameketi kuume kwa Baba, maana yake: ameketi katika utukufu na heshima ya Kimungu, ambaye Yeye aliyekuwako kama Mwana wa Mungu kabla ya nyakati zote, kama Mungu, na mwenye uwamo mmoja na Baba, anaketi kimwili, baada ya kumwilishwa na baada ya mwili wake kutukuzwa. Kuanzia hapo Mitume wamekuwa ni mashuhuda wa Ufalme usiokuwa na mwisho. Rej. KKK 659-664. Ni katika muktadha wa maadhimisho ya Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni tarehe 29 Mei 2025, lakini kutokana na sababu za kichungaji, Sherehe hii inaadhimishwa Dominika tarehe 1 Juni 2025 sanjari na Maadhimisho ya Siku ya 59 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni inayonogeshwa na kauli mbiu: “Shirikisheni kwa upole tumaini lililo mioyoni mwenu.” Rej. 1Pet 3: 15-16. Kristo Yesu anaendelea kujifunua na kuzungumza na wafuasi wake kwa: Neno, neema na baraka zinazobubujika kutoka katika Sakramenti za Kanisa na uzuri wa mbinguni ambapo waamini wanaalikwa kuukumbatia, ili kwa furaha na shangwe waweze kuwa mahali alipo Yeye ambaye ni kichwa cha mwili wake yaani Kanisa. Rej. Kol1:18; 1Kor 12:12-27.

Mashuhuda wa Habari Njema ya Wokovu
Mashuhuda wa Habari Njema ya Wokovu   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 28 Mei 2025 amewatia shime waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Habari Njema ya Wokovu kama ilivyokuwa kwa Mitume wa Kristo Yesu. Iwe ni Sherehe inayowakirimia waamini mang’amuzi yanayopyaisha matumaini na furaha, tayari kujizatiti katika kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo Yesu kwa uaminifu, nguvu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Waamini wajibidiishe kutafuta uwepo angavu wa Kristo Yesu na upendo wake usiokuwa na kikomo katika uhalisia wa maisha yao. Na kwa msaada wa sala na maombezi ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema, awaombee neema ya kumpenda Kristo Yesu. Baba Mtakatifu Leo XIV amemkumbuka Mwenyeheri Kardinali Stefan Wyszyński, Baba na Mkuu wa Kanisa la Poland, licha ya mateso na madhulumu dhidi ya Kanisa, lakini akabaki mchungaji mwaminifu kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Katika maisha na utume wake, alijipambanua kwa sadaka, majitoleo na hamu yake ya kukuza na kudumisha majadiliano katika ukweli na uwazi, akafanikiwa kulinda na kudumisha umoja wa Kanisa na jamii katika ujumla wake. Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, ushuhuda wa imani yake kwa Kristo Yesu na Kanisa lake, uwe ni kikolezo na msukumo wa kulijali Kanisa na nchi yao katika ujumla wake.

Kupaa Bwana 2025
28 Mei 2025, 16:46