MAP

Askofu Robert Francis Prevost akiwa na Balozi wa Vatican wa Peru Paolo Rocco Gualtieri (wa nne kushoto). Askofu Robert Francis Prevost akiwa na Balozi wa Vatican wa Peru Paolo Rocco Gualtieri (wa nne kushoto). 

Papa Leone XIV,Balozi wa Vatican,Perù:Uzoefu wa utume wake ni utajiri wa upapa!

Askofu Mkuu Paolo Rocco Gualtieri,Balozi wa Vatican nchini Peru anasimuliza kwa shuuku ya nchi ya Amerika Kusini baada ya uchaguzi wa Papa kuwa: “Yuko katika moyo wa Peru,hapa alitembea pamoja na watu wake.”

Na Benedetta Capelli na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa sauti ya Askofu Mkuu  Paolo Rocco Gualtieri, Balozi wa Vatican nchini  Peru tangu 2022, inasikika kuwa bado kuna hisia na shauku ya watu ambao walihisi kuguswa na neema ya kumjua na kusindikizwa Papa wa baadaye. Alama iliyoachwa na Askofu Robert Francis Prevost, bado iko hai na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Televisheni na magazeti ulimwenguni kote, zimewekwa katika kumbukumbu ya kujitolea kwake wakati wa janga uviko  la 2020 na juhudi zake baada ya kupita kwa mafuriko ya El Niño mnamo 2023.

Furaha ya kuchaguliwa kwa Papa Mpya
Furaha ya kuchaguliwa kwa Papa Mpya   (AFP or licensors)

Marafiki wawili makuhani wanakumbuka Papa Leo XIV, ile miaka ya Prevost huko Peru kuwa ni "Mmisionari wa kweli". Ushuhuda uliokusanywa kutoka kwa watu waliomfahamu Padre Prevost wa wakati huo: mchungaji mwenye uwezo wa kuzungumza na watu, makini na changamoto za kijamii na aliyehuishwa sana na ...

Kardinali Prevost akiwa na dada zake watawa wa Kasha 22 Mei 2024
Kardinali Prevost akiwa na dada zake watawa wa Kasha 22 Mei 2024

Moyo ulitia nanga kwa Peru

"Nchi nzima inafurahia kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV kwa sababu alitumia muda mwingi wa maisha yake hapa Peru ambako alipata uzoefu mkubwa", alisema Askofu Mkuu Gualtieri. "Alifika akiwa mdogo sana akiwa padre na mmisionari kisha akawa profesa wa sheria za Kanisa katika Seminari kuu, aliishi uzoefu wa mamlaka mbili za Kanda , alikuwa mwalimu, msimamizi wa kitume wa Jimbo kuu la Chiclayo na kisha Askofu. Uzoefu mzuri, alitoa moyo wake kwa Peru".

Akiwa juu ya Farasi kutembelea waamini wake sehemu za milimani
Akiwa juu ya Farasi kutembelea waamini wake sehemu za milimani

Kutia moyo kwa wakazi wa Peru

Kwa mwakilishi wa Papa, ambaye aliwasili huko Peru mnamo Desemba 2022, miezi michache kabla ya Papa Francisko kumteua Prevost kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu, uchaguzi wa Papa Leo XIV unapaswa pia kutambuliwa kama "kutia moyo kwa nchi ambayo inakabiliwa na hali si rahisi ya kijamii na kisiasa." Kwa ajili yake, uwazi ni kielelezo cha "mchungaji aliye karibu sana na watu wake, ambaye alitembea na watu wake. Wananchi wamemshika sana, anakumbuka alipokuja nchini kwa mara ya kwanza akiwa Kardinali nilifurahi sana kumsindikiza Chiclayo na wananchi walifurahi sana. Unaweza kuona kwamba alikuwa mchungaji wa karibu."

Papa mkuu

"Ninaamini kwamba uzoefu huko Peru Askofu Mkuu Gualtieri alisisitiza - ulikuwa mzuri kwake kama mmisionari, kama mwalimu, na askofu wa Chiclayo. Yeye ni mtu rahisi sana lakini amedhamiria, mchungaji mkuu, ningemfafanua hivyo. Atakuwa Papa mkuu." Huduma ambayo bado itadai "lakini kwa jina la umoja, ili tuweze kutembea pamoja kama Kanisa la pamoja, Kanisa la Kisinodi, Kanisa linalotembea kama watu na, kama yeye mwenyewe alivyosema, kuangazia usiku wa ulimwengu. Kiukweli ni muhimu kukuza umoja na amani katika ulimwengu unaopitia, kama Papa Francis alivyosema, vita vya ulimwengu vimegawanyika vipande."
 

Siku ya kukabidhiwa Kanisa la la Mtakatifu Monica
Siku ya kukabidhiwa Kanisa la la Mtakatifu Monica   (Vatican Media)

Na sasa tunaye Papa Leo XIV ambaye amemrithi mtanguliz wake Hayati Papa Francisko.

17 Mei 2025, 12:06