ÐÓMAPµ¼º½

Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa mwaliko kwa Jumuiya ya Kimataifa kusitisha vita nchini Ukraine na Ukanda wa Gaza na kuanza kujikita katika mchakato wa majadiliano katika ukweli na uwazi. Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa mwaliko kwa Jumuiya ya Kimataifa kusitisha vita nchini Ukraine na Ukanda wa Gaza na kuanza kujikita katika mchakato wa majadiliano katika ukweli na uwazi.  (AFP or licensors)

Papa Leo XIV: Wito wa Kusitisha Vita Nchini Ukraine na Ukanda wa Gaza

Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na mashambulizi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu. Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa mwaliko kwa wahusika wakuu wa vita hii kusitisha vita na kuanza kujielekeza katika mchakato wa majadiliano katika ukweli na uwazi, ili kujenga na kudumisha amani ya kudumu. Baba Mtakatifu ametoa mwaliko kwa waamini kujiunga pamoja naye kwa ajili ya kuombea amani Ukraine na maeneo ya vita.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 28 Mei 2025 ameonesha uwepo wake wa karibu kwa watu wa Mungu wanaoteseka kutokana na madhara ya vita huko nchini Ukraine. Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na mashambulizi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu. Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa mwaliko kwa wahusika wakuu wa vita hii kusitisha vita na kuanza kujielekeza katika mchakato wa majadiliano katika ukweli na uwazi, ili kujenga na kudumisha amani ya kudumu. Baba Mtakatifu ametoa mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema, kujiunga pamoja naye kwa ajili ya kuombea amani nchini Ukraine pamoja na maeneo mbalimbali yaliyoathirika kwa vita.

Papa Leo XIV Asisitiza umuhimu wa kusitisha vita nchini Ukraine
Papa Leo XIV Asisitiza umuhimu wa kusitisha vita nchini Ukraine   (AFP or licensors)

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Leo XIV anasikitika kusema kwamba, kilio cha watu wa Mungu Ukanda wa Gaza, kinaendelea kupanda mbinguni kutokana na vifo vya watu wasiokuwa na hatia. Kuna umati mkubwa wa watoto wanaoendelea kuteseka kutokana na vita pamoja na baa la njaa linaloendelea kusigina utu, heshima na haki msingi za watoto hawa. Kwa mara nyingine tena, Baba Mtakatifu Leo XIV anawaalika viongozi wakuu wa Mataifa kusitisha vita hii, mateka na wafungwa wa vita waachiliwe huru na kwamba, sheria za Kimataifa zilindwe na kuheshimiwa na wote. Bikira Maria Malkia wa Amani, awaombee watu wote!

Wito wa Amani
28 Mei 2025, 14:54