ĐÓMAPµĽş˝

2025.05.19 Papa akutana na Wawakilishi wa dini mbali mbali(Mkutano wa kiekumene. 2025.05.19 Papa akutana na Wawakilishi wa dini mbali mbali(Mkutano wa kiekumene.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa viongozi wa kidini:Leo ni wakati wa mazungumzo na kujenga madaraja!

Papa Leo XIV akikutana na wawakilishi wa makanisa mengine, jumuiya za kikanisa na dini nyingine alitoa ushauri wa kufanya juhudi za pamoja,kuwa dhidhi ya itikadi na sera za kisaisa, kwa ajili ya amani ulimwenguni.Kukataa vita,silaha na uchumi unaoleta umasikini.Amewatia moyo katika safari ya kiekumene na kusisitiza kuendeleza mazungumzo kati ya Wayahudi na Wakristo na kuendeleza uhusiano na Waislamu katika kuheshimiana na uhuru wa dhamiri.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV amefanya Mkutano wa wawakilishi wa Makanisa mengine na Jumuiya za Kikanisa na dini nyingine, Jumatatu tarehe 19 Mei 2025 katika ukumbi wa Clementina mjini Vatican. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu ameonesha furaha kubwa kuwapa salamu zake za upendo kwa wote, wawakilishi wa makanisa mengine ya jumumuya za kikanisa, kama vile dini nyingine ambazo walipenda kuwa sehemu ya maadhimisho ya kuanza kwake  huduma  ya Askofu wa Roma na Mfuasi wa Petro. Wakati akimkaribisha ndugu yake, Patriaki Bartolomeo, Theofilos III na Mar Awa III na kwa kila mmoja wao,  Papa Leo XIV alitoa shukrani kubwa kwa uwepo wao, sala kwa ajili ya Papa za faraja kubwa na kutiwa moyo.

Mkutano wa kiekumene
Mkutano wa kiekumene   (@Vatican Media)

Moja ya sehemu ya nguvu ya Upapa wa Papa Francisko ilikuwa ni ile ya udugu wa ulimwengu. Katika hilo Roho Mtakatifu alimsukuma kweli  atumie nafasi kubwa ya ufunguzi na mwanzo ambao tayari ulikuwa umefuatiliwa na mapapa waliopita, hasa kuanzia na Mtakatifu Yohane XXIII. Papa wa Wote ni Ndugu  aliendeleza njia ya kiekumene na mazungumzo ya kidini, na alifanya hivyo juu ya yote kwa kukuza uhusiano kati ya watu, ili, bila kuchukua chochote kutoka kwa vifungo vya kikanisa, kipengele cha kibinadamu cha kukutana kilithaminiwa daima. Mungu atusaidie kutunza ushuhuda wake! Baba Mtakatifu Leo XIV alisema kuwa kuchaguliwa kwake kumekuja sambamba na maadhimisho ya miaka 1700 tangu kufanyika Mkutano wa kwanza wa kiekumene huko Nicea. Mkutano huo unawakilisha na hatua msingi kwa ajili ya kufanyia kazi ya sala ya Nasadiki shirikishi,  kwa Makanisa na Jumuiya zote za kikanisa. Tunaposafiri kuelekea kuanzishwa tena kwa ushirika kamili kati ya Wakristo wote, tunatambua kwamba umoja huu unaweza tu kuwa umoja katika imani.

Kwa kuwa ni Askofu wa Roma, Baba Mtakatifu amefikiria moja ya majukumu yake ya kipaumbele  katika kutafuta urejesho kamili na umoja unaonekana kati ya wale wote ambao wanakiri imani moja  kwa Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kiukweli, umoja ule daima ulikuwa wasiwasi wake daima, kama ushuhuda wa kauli mbiu yake ambayo alichagua katika huduma yake ya kiaskofu : In Illo uno unum, msemo wa Mtakatifu Agostino wa Hipo ambaye anakumbusha kama hata sisi kuwa licha ya kuwa wengi (in Quell’unico), ule mmoja yaani Kristo, sisi ni wamoja (Zaburi ya 127, 3).

Mkutano wa kiekumene
Mkutano wa kiekumene   (@Vatican Media)

Umoja wetu unajiwakilishwa, kiukweli katika kiwango ambacho tunajihusisha katika Bwana Yesu Kristo. Kwa kiasi ambacho sisi ni waamini na watiifu kwake, ndivyo tulivyoungana kati yetu. Kwa hiyo, kama wakristo, sisi sote tunaishi kwa kusali na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kufikia hatua kwa hatua hatima hii ambayo na inabaki kuwa kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa utambuzi zaidi kwamba Sinodi na Uekumene vinaungana moja kwa moja, Baba Mtakatifu Leo XIV ameongeza kusema kuwa anapenda kuwahakikishia nia yake ya kuendeleza jitihada za Papa Francisko katika kuhamasisha tabia ya kisinodi ya Kanisa Katoliki na katika kuendeleza mitindo mipya na dhati kwa ajili ya sinodi ya kina daima katika nyanja ya kiekumene.

Papa Leo XIV aliendelea  kuwa Mkutano wao wa pamoja una, na lazima uwe wa kina hata katika maana pana ambayo inawaunganisha wote katika roho ya udugu wa kibinadamu ambao alikuwa amewaeleza hapo awali. Leo hii, ni kipindi cha mazungumzo na cha ujenzi wa madaraja. Papa alikazia kusema,  kwa njia hiyo anayo furaha na shukrani kwa uwepo wa Wawakilishi wa tamaduni nyingine za kidini, ambao wanashiriki katika utafutaji wa Mungu na mapenzi yake, ambayo daima na upendo wake tu na wa maisha kwa ajili ya wanaume na wanawake na kwa viumbe vyote.

Mkutano wa kiekumene
Mkutano wa kiekumene   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV alisema kuwa,  wao wamekuwa mashuhuda muhimu wa nguvu zilizotimizwa na Papa Francisko katika kusaidia mazungumzo ya kidini. Kwa njia ya maneno yake na matendo yake, alifungua matarajio mapya ya kukutana, ili kuhamasisha “utamaduni wa mazungumzo kama njia; ushirikiano wa pamoja kama mwelekeo; utambuzi wa pamoja kama mtindo na kigezo”(Hati ya Udugu wa kibinadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi pamoja (Abu Dhhabi,4 Februari 2019).

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu ameshukuru Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini kwa ajili ya Jukumu muhimu ambalo linahusisha kwa uvumilivu wa kazi ya kutia moyo mikutano na mabadilishano ya dhati, yanayotazama ujenzi wa uhusiano unaojikita juu ya udugu wa kibinadamu. Katika hilo, pia Papa amependa kutoa  salamu maalum kwa kaka na dada wayahudi na waislamu. Kwa sababu ya mizizi ya kiyahudi ya kikirsto, wakristo wote  wanauhusiano maalum na Uyahudi.

Katika Tamko la Mtaguso wa Nostra aetate(n. 4) –(Enzi zetu), ulisisitiza kwa urithi mkubwa wa kiroho wa pamoja kwa wakristo na wayahudi, kuhimiza ujuzi na kuheshimiana. Mazungumzo ya kitaalimungu kwa wakristo na wayahudi inabaki kuwa muhimu daima na ipo rohoni mwake. Hata katika kipindi kigumu ambacho kimegubikwa na migogoro na kutokuelewana, ni lazima kuendelea kwa kazi katika mazungumoz yetu hata ya thamani. Uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na Waislamu yamekuwa ya kuendelea katika juhudi kwa ajili ya mazungumzo na ya udugu, kwa kusaidia na kupendelewa na heshima ya kaka na dada hawa“ ambao wanaabudu Mungu mmoja, aliye hai na anayeishi, mwenye huruma na mwenyezi, muumba mbingu na dunia, ambaye alizungumza na waamini,”3).

Mkutano wa kiekumene
Mkutano wa kiekumene   (@Vatican Media)

Mbinu hiyo, inayoundwa katika msingi wa heshima ya pamoja, na juu ya uhuru wa dhamiri, inawakilisha msingi kwa ajili ya ujenzi wa msingi kati ya jumuiya zetu. Baba Mtakatifu alielezea kwa wote, yaani wawakilishi wa tamaduni nyingine za kidini shukurani kwa ushiriki wao na mkutano huo, na kwa mchango wake wa amani, katika ulimwengu uliojeruhiwa na vurugu, na migogoro, kila mmoja wa jumuiya ambayo wamewakilisha wanatoa mchango wao wenyewe wa hekima, huruma, na kujitolea kwa manufaa ya ubinadamu na ulinzi wa nyumba yetu ya pamoja.

Mkutano wa kiekumene
Mkutano wa kiekumene   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV anaamini kwamba ikiwa tutakuwa na maelewano na huru dhidi ya itikadi na sera za siasa, tunaweza kuwa na muafaka na kusema “hapana vita na Ndiyo ya “amani;” “hapana,”  kukumbilia silaha na ndiyo ya kutokuwa na silaha; “hapana” uchumi ambao unaleta umaskini wa watu na Dunia na “ndiyo” kwa maendeleo Fungamani. Ushuhuda wa udugu wetu ambao Papa Leo XIV,  anatamani alisema wanaweza kuonesha ishara muafaka ya kuchangia kwa hakika ili kujenga ulimwengu ulio na amani, kama mioyo inavyotamani wote kuwa wanaume na wanawake wa mapenzi mema. Baba Mtakatifu Leo XIV alihitimisha kwa kuwashukuru tena  ukaribu wao. “Tunaomba katika mioyo yetu baraka za Mungu: wema na hekima yake isiyo na kikomo itusaidie kuishi kama watoto na kaka na dada zake kati yetu, ili tumaini liweze kukua ulimwenguni.”

Hotuba ya Papa
19 Mei 2025, 11:51