Papa Leo XIV:Mapapa wanapita Curia inabaki,sawa na makanisa mahalia ya Curia za Maaskofu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican Jumamosi tarehe 24 Mei 2025 alikutana na maofisa wa Curia Roman, Wenyeviti wa Mabaraza ya Kipapa, wafanyakazi wa mji wa Vatican, Gavana wa mji wa Vatican na Vicariate ya Roma. Mara baada ya kuingia katika ukumbi huo, alipokelewa na shangwe na makofi mengi yaliyodumu muda dakika tatu hivi ambapo kwa matani Papa alisema: “Asanteni! Makofi yanapodumu kwa muda mrefu kuliko hotuba, itabidi nitoe hotuba ndefu zaidi!. Kwa hivyo... kuweni makini! Asante! Asante!" Huu ulikuwa ni utani tu ili kusitisha makofi hayo na vifijo. Huu ulikuwa ni mkutano wake wa kwanza wa Papa tangu alipochaguliwa pamoja na wafanyakazi wa kila ngazi na kila kategoria ya Nchi ndogo duniani, wakiwa wamesindikizwa na familia zao. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu akifanya ishara ya Msalaba kwa kukatisha makofi alisema: Kwa jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amani iwe kwenu."
"Nina furaha kuweza kuwasalimu ninyi nyote, mnaounda jumuiya zinazofanya kazi za Curia ya Romana, Gavana na Vicariate ya Roma. Nawasalimu Wakuu wa Mabaraza ya Kipapa na Wakuu wengine, Wakuu wa Ofisi na Viongozi wote; pamoja na Mamlaka za Jiji la Vatican, maafisa na wafanyakazi. Na ninafurahi sana kwamba wanafamilia wengi pia wapo, wakichukua fursa ya siku kuwa Jumamosi. Mkutano wetu huu wa kwanza kwa hakika si wakati wa kutoa hotuba za kimipango, bali ni fursa yangu ya kutoa asante kwa huduma mnayofanya, na huduma hii ambayo, kwa kusema, “ninarithi” kutoka kwa Watangulizi wangu. Asante sana. Ndiyo, kama mnavyojua, nilifika miaka miwili tu iliyopita, wakati Baba Mtakatifu Francisko aliponiteua kuwa Mwenyekiti wa Baraza ka kipapa la Maaskofu.
Papa Leo alielezea huduma yake katika Nchi ya Amerika kusini kwamba:“Kwa njia hiyo niliacha Jimbo la Chiclayo nchini Peru, na nilikuja kufanya kazi hapa. Ni mabadiliko mangapi! Na sasa…. Ni kitu gani ninaweza kusema? Ni kile ambacho alisema tu Simoni Petro kwa Yesu katika ziwa la Teberia kwamba: “Bwana, wewe unajua yote, wewe unajua jinsi ninavyokupenda”Yh 21,17). Mapapa wanapita, Curia inabaki. Hii ni sawa na kila Kanisa mahalia, kwenye Curia za Maaskofu. Na hivyo ni sawa sawa hata Curia ya Maaskofu wa Roma. Curia ni taasisi ambayo inalinda, na inaendeleza kumbu kumbu ya kihistoria ya Kanisa, ya huduma ya maaskofu wake. Hiyo ni muhimu sana. Kumbukumbu ni kitu muhimu sana katika kila kiungo hai. Na hii haielekezi kwenye wakati uliopita, lakini inamwilishwa na wakati uliopita na kuelekeza wakati ujao. Bila kumbukumbu safari inapotea, inapita kwa maana ya njia.”
Katika hili Papa Leo alisisitza kuwa: “Kwa maana hiyo wapendwa hili ni wazo la kwanza ambalo ninapenda kushirikishana nanyi: kufanya kazi katika Curia Romana maana yake ni kuchangia kwa kuzingatia uhai wa kumbu kumbu ya Makao makuu ya Kitume, kwa maana iliyo hai ambayo nimemaliza kutaja, kwa njia hiyo huduma ya Papa inaweza kuwa nzuri kwa namna nyingine. Kisha kuna mantiki nyingine ambayo ninapenda kusisitiza, ya kukamilisha ile ya kumbukumbu yaani ya ukuu wa kimisionari wa Curia na ya kila taasisi zinazounganishwa na huduma ya Petro. Katika suala hili Papa Francisko alisisitiza sana, na kwa usahihi na mpango alioutangaza katika Waraka wa kitume wa Evangelii gaudiumu, ilibadilisha Curia Romana. Na hiyo alifanya kuweka katika mwendelezo wa Watangulizi wake hasa wa Mtakatifu Paulo VI na Mtakatifu Yohane Paulo II.”
Kwa uzoefu wake wa kimisionari Papa Leo XIV alisema: “Kama ninavyofikiri mnajua, uzoefu wa utume mnaofanya katika maisha yetu na si kwa wabatizwa, kama ilivyo kwa wakristo wote, lakini kwa sababu kama mtawa wa kiagostino nilikuwa mmisionari huko Peru, na katikati ya watu wa Peru nilikomaa wito wangu wakichungaji. Sitoweza kushukuru vya kutosha Bwana kwa zawadi hiyo! Kisha wito wa kuhudumia Kanisa hata Curia Romana umekuwa utume mpya, ambao nimeshirikisha ninyi katika miaka hii miwili. Na bado ninandelea na nitaendelea, hadi Mungu atakapopenda, katika huduma hii ambayo nilikabidhiwa. Kwa hiyo, ninarudia tena kile nilichosema katika salamu yangu ya kwanza, jioni ya Mei 8: "Lazima tutafute pamoja jinsi ya kuwa Kanisa la kimisionari, Kanisa linalojenga madaraja, mazungumzo, daima wazi kwa kukaribisha [...] kwa kukumbatia kwa mikono miwili kila mtu, wale wote wanaohitaji upendo wetu, uwepo wetu, mazungumzo na upendo."
Baba Mtakatifu Leo alikazia kuwa: "Maneno hayo yalikuwa yanaelekezwa kwa Kanisa la Roma. Na sasa nayarudia kwa kufikiria utume wa Kanisa hili kwa njia ya Makanisa yote na ulimwengu mzima, wa kuhudumia ushirika, umoja katika upendo na katika ukweli. Bwana amelisema kwa Petro na wafuasi wake katika kazi hiyo, na kwenu ninyi kwa namna tofauti kushirikiana kwa ajili ya kazi kuu. Kila mmoja anatoa mchango wake kwa kujikita katika kazi ya kila siku kwa jitihada na hata kwa imani, kwa sababu imani na sala ni kama chumvi katika chakula itoayo radhia"
BabaMtakatifu Leo alisema kuwa "Ikiwa ni lazima sote tushirikiane katika sababu kuu ya umoja na upendo, na tujaribu kufanya hivyo kwanza kabisa kwa tabia zetu katika hali za kila siku, kuanzia pia mahali pa kazi. Kila mtu anaweza kuwa mjenzi wa umoja na mitazamo yake kwa wenzake, kushinda kutoelewana kusikoepukika kwa subira na unyenyekevu, kujiweka katika nafsi za watu wengine, kuepuka chuki na pia kuwa na tabia nzuri ya ucheshi, kama Papa Francisko alivyotufundisha."
Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Leo XIV alisema "Ndugu wapendwa Kaka na dada, ninawashukuru tena kwa moyo! Tuko kwenye mwezi Mei: tumuombe pamoja Bikira Maria, ili abariki Curia Romana na Mji wa Vatican, na hata familia zenu, hasa watoto, wazee na watu wagonjwa na wanaoteseka. Salamu Maria….”