Papa Leo XIV atembelea Baraza la Kipapa la Maaskofu
Vatican News
Jumanne asubuhi tarehe 20 Mei 2025 Baba Mtakatifu Leo XIV alitembelea Baraza la Kipapa la Maaskofu kwa kushitukiza ambako aliadhimisha Misa katika kikanisa hicho. Haya yalitangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican.
Katika makao makuu yaliyoko katika Uwanja wa Pio XII ambayo alikuwa Mwenyekiti wake tangu kuteuliwa kwake kunako tarehe 30 Januari 2023 hadi kuchaguliwa kwake kuwa Papa Leo XIV. Alifika karibu saa 4.00 asubuhi marija ya Ulaya ndani ya gari ndogo jeusi ambalo tayari limeonekana kwa ziara zake nje ya Vatican.
Ya kwanza mnamo tarehe 10 Mei 2025, huko Genazzano, kusali katika Madhabahu ya Mama wa Shauri Jema, na ile ya Juma moja kabisa iliyopita alipokwenda Nyumba Mama ya Shirika la Waagostiniani ambapo aliadhimisha Misa na kula chakula cha mchana na ndugu zake wa Waagostiniani.
Kwa njia hiyo, safari hii ilikuwa ya tatu ya kushangaza iliyosalimiwa na makofi na nyimbo za "Viva il Papa" kutoka katika umati mdogo uliokusanyika kwenye Uwanja mita chache kutoka kwenye nguzo za Mtakatifu Petro na Watu wengine walikusanyika katika njia ya Corridori, kwa hiyo nyuma ya jengo, kusubiri gari na Papa kuondoka kwenye eneno hilo, baada ya saa moja na nusu.