ĐÓMAPµĽş˝

2025.05. instagram ya kwanza ya  Papa Leo XIV 2025.05. instagram ya kwanza ya Papa Leo XIV 

Papa Leo XIV achapisha chapisho la kwanza kwenye akaunti za mitandao ya kijamii za kipapa

Katika akaunti za mitandao ya kijamii za Papa,chapisho la kwanza la Papa Leo XIV limechapishwa ambazo zilitumiwa kwa ufanisi mkubwa na watangulizi wake,kama Papa Francisko na Papa Benedikto XVI.

Na Angella Rwezaula – vatican.

Papa Leo XIV alichagua "kudumisha uwepo hai wa mitandao ya kijamii kupitia akaunti rasmi za kipapa kwenye X na Instagram," kulingana na taarifa kutoka vyombo vya habari  vya baraza la Kipapa la Mawasiliano, Jumanne tarehe 13 Mei 2025, Chapisho la kwanza la Papa kwenye Instagram lilichukuliwa kutoka katika hotuba yake ya kwanza ya umma katika Baraka  ya  Urbi et Orbi, mara tu baada ya kuchaguliwa kwake tarehe 8 Mei 2025 na ilijumuisha picha kadhaa za siku za kwanza za upapa wake.  "Amani iwe kwenu nyote! Ndiyo ilikuwa salamu ya kwanza kusemwa na Kristo Mfufuka, Mchungaji Mwema. Ningependa salamu hii ya amani isikike mioyoni mwenu, katika familia zenu, na kati ya watu wote, popote walipo, katika kila taifa na duniani kote."

Wafuasi wa akaunti ya Pontifex

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Baraza la Kipapa la Mawasiliano (Baraza letu) lilibainisha kuwa akaunti rasmi ya kwenye X inahesabu jumla ya wafuasi milioni 52 katika lugha tisa. Maudhui yaliyotumwa na hayati Papa Francisko yatahifadhiwa katika sehemu maalum ya tovuti ya kitaasisi ya ().

Katika Instagram, akaunti mpya ya Papa itakuwa na jina @Pontifex - Papa Leo XIV, ambayo itakuwa akaunti pekee rasmi ya papa kwenye jukwaa linalomilikiwa na Meta. Akaunti ya Papa Francisko  itaendelea kupatikana kama kumbukumbu ya ukumbusho," ilibainisha taarifa kwa vyombo vya habari. Hayati Papa Francisko alidumisha uwepo wake katika mitandao ya kijamii, akichapisha karibu machapisho 50,000, mengi yakichapisha dondoo za hotuba zake kwenye X na picha kutoka katika matukio yake ya umma kwenye Instagram.

“Machapisho haya ni msaada wa karibu kila siku katika kipindi chote cha Papa Francisko kwa jumbe fupi za asili ya kiinjili na mawaidha kwa ajili ya amani, haki ya kijamii, na kujali uumbaji" ilisema taarifa hiyo kwa vyombo vya habari. Mnamo mwaka 2020 pekee, yaliyomo kwenye vyombo vya  kijamii ya  Hayati  Papa Francisko yalitazamwa zaidi ya mara bilioni 27.

Mitandao ya kijamii ya Papa

Papa Benedikto XVI alikuwa Papa wa kwanza kufungua akaunti ya mtandao wa kijamii, kutuma ujumbe wa kwanza wa Papa alipokuwa na umri wa miaka 84, kwenye kile kilichoitwa Twitter, tarehe 12 Desemba 2012.  "Wapendwa marafiki, ninafuraha kuwasiliana nanyi kupitia Twitter. Asanteni kwa majibu yenu ya ukarimu. Ninawabariki nyote kutoka moyoni mwangu," aliandika Papa huyo mzaliwa wa Ujerumani. Tweet yake yenye herufi 140 ilifungua mlango kwa Vatican kukumbatia aina ya kisasa ya mawasiliano ya kijamii.

Alipochaguliwa kuwa Papa wa 266, Papa Francisko alitumia akaunti hiyo hiyo ya Twitter, kutuma ujumbe wake wa kwanza: “Wapendwa, ninawashukuru kutoka moyoni mwangu na kuwaomba muendelee kuniombea.”

Tarehe 19 Machi 2016, katika maadhimisho ya Mtakatifu Yosefu, Papa Francisko alipanua uwepo wa papa katika mitanado ya kijamii kwa kufungua akaunti yake ya Instagram,(  yenye jina: @franciscus. Chapisho lake la kwanza lilikuwa picha yake huku akipiga magoti katika maombi yenye nukuu: "Niombee" katika lugha kadhaa.

Kwa njia hiyo Papa Leo XIV anapotumia tena njia za kisasa za mawasiliano ya kijamii, taasisi za Kanisa na Wakatoliki wote wanaweza kutazama mwongozo wake na msukumo wa jinsi ya kujiendesha mtandaoni.

Chapisho jipya la Papa Leo XIV katika Pontifex
14 Mei 2025, 10:45