Papa Leo XIV atembelea Jumuiya ya Waagostiniani!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Misa iliyoadhimishwa na ndugu zake wa Mtakatifu Agostino, katika siku ambayo Mama Kanisa anamkumbuka Bikira Maria wa Fatima. Baadaye chakula pamoja nao kama ilivyokuwa kama kawaida na yeye wakati alipokuwa Kardinali. Papa Leone XIV alikwenda kabla ya saa sita Jumanne tarehe 13 Mei 2025 katika Nyumba Kuu ya Shirika la Mtakatifu Agostioni, ambapo kwa miaka 12 aliishi humo kuanzia 2001 hai 2013, kipindi ambacho yeye alikuwa ni Mkuu wa Shirika hilo ulimwenguni. Mita chache zilizopitiwa na gari jeusi ambalo lililompeleka Papa Leo XIV kutoka Vatican hadi Njia ya Paolo VI, karibu na nguzo ya Bernini, zinzozunguka Uwanja wa Mtakatifu petro ili kufanya ziara ya kibinafsi kwa familia yake ya kitawa, ambapo ushawishi wa kwanza ni ule wa kanuni zilizozingatiwa, kwa sababu iliwekwa na Askofu wa Hippo(yaani Mtakatifu Agostino) katika kanuni ya maisha kwa ndugu zake isemayo: “Sababu muhimu ambayo nimewaunganisha kuwa pamoja ni kwamba mnaishi kwa amani ndani ya nyumba na kuwa na roho moja na moyo mmoja ulioelekezwa kwa Mungu."
Mamia ya watu walikusanyika mbele ya lango la ukumbi wa Nyumba Mama ya Waagostinani na katika eneo jirani, wakijazana kwenye njia ya Paolo VI, ili kusubiri kuondoka kwa Papa katika Nyumba kuu ya Waagostiniani hata wakikabiliana na mvua kubwa isiyotarajiwa. Papa aliondoka kwenye jumuiya ya ndugu karibu saa 9:00 alasiri, akiwasalimu wale waliokuwa wakimsubiri.
Mkuu wa Shirika wa wakati huu, Padre Alejandro Moral, aliviambia vyombo vyetu vya habari vya Vatican kwamba kila kitu kilifanyika katika ukumbi wa mikutano ya jumla na kwamba Papa aliongoza Liturujia ya Ekaristi katika kikanisa chao ikifuatiwa na chakula cha mchana na mazungumzo ya faragaha kwao. Mahojiano ya Padre Alejandro Moral na Vatican News
Ulikuwa mkutano wa aina gani?
Kwa kawaida alikuja kula hapa na alitaka kushukuru jumuiya kwa hili. Alikuja kuadhimisha Ekaristi na kula pamoja nasi. Ilikuwa ni ziara ya kifamilia, ya shukrani. Zilikuwa nyakati zilizotumiwa pamoja ambazo zilijulikana sana, za kupendeza sana. Kwa sababu anajua kila mtu na wote tunamfahamu na ndiyo maana ni vizuri sana.
Je, mlitumia muda wa pamoja?
Ndiyo, lakini pia kulikuwa na watu wengine waliokuja kumsalimia: wafanyakazi wanaofanya kazi nasi, na wapishi.
Ilikuwa ni wakati wa kufurahisha?
Ndiyo, kuishi kwa pamoja. Ilikuwa ni ziara yake ya kwanza kama Papa, sote tulifurahi sana.
Alikuambia nini?
Kwamba lazima daima tuwe karibu na kila mmoja wetu, kuishi, kama Mtakatifu Agostino anavyoomba kuishi kwa umoja.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kusasisha kwa kujiandikisha kwenye jarida letu la kila siku. Just click here