MAP

Papa katika Kanisa Kuu la Laterano,Roma:Ninawapenda!

“Kanisa la Roma ni urithi wa historia kubwa,umoja unajengwa awali ya yote kwa kupiga magoti,katika chaguzi za maisha hatuko peke yetu,mkristo pamoja nanyi na Askofu kwa ajili yenu,anayesikiliza wote,ninawakikishia kuwa ninawapenda.”Haya yamo kwenye mahubiri ya Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa katika Kanisa kuu la Laterano mahali aliposimikwa rasimi kwa jimbo lake Kuu la Roma,jioni tarehe 25 Mei 2025.

Na Angella Rwezula – Vatican.

Katika siku ambayo Baba Mtakatifu Leo XIV amesimikwa rasimi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterano, jioni ya Dominika tarehe 25 Mei 2025,  baada ya masomo alianza na salamu kwa wawakilishi wote waliokuwapo kuanzia na makardinali, maaksofu wasaidizi wa Jimbo la Roma na maaskofu wengine wote, mapadre, waamini na wote wenye majukumu katika jumuiya ya kichungaji, mashemasi, watawa wa kike na kiume na mamlaka ya kiraia.

Kardinali Reina akimkaribisha Papa Leo XIV
Kardinali Reina akimkaribisha Papa Leo XIV   (@Vatican Media)
Misa katika Kanisa Kuu la Laterano
Misa katika Kanisa Kuu la Laterano   (@VATICAN MEDIA)

Kanisa la Roma ni mrithi wa historia kuu inayojikita katika ushuhuda wa Petro, Paulo na mashahidi wasiohesabika, na lina utume wa pekee, unaooneshwa vyema na yale yaliyoandikwa kwenye mbele ya Kanisa kuu hili: kuwa Mater omnium Ecclesiarum, yaani Mama wa Makanisa yote. Baba Mtakatifu Francisko ametualika mara kwa mara kutafakari juu ya mwelekeo wa kimama wa Kanisa (Evangelii gaudium, 46-49.139-141; Katekesi, 13 Januari 2016) na sifa zake: huruma, utayari wa kujitolea na uwezo huo wa kusikiliza ambao huruhusu sio tu kusaidia, lakini mara nyingi kutazamia mahitaji na matarajio, hata kabla ya kuoneshwa. Hizi ni tabia ambazo tunatumaini zitakua kila mahali katika watu wa Mungu, ikiwa ni pamoja na hapa, katika familia kuu ya jimbo: kwa waamini, kwa wachungaji, na ndani yangu kwanza kabisa.

Misa ya Papa katika Kanisa Kuu la Laterano
Misa ya Papa katika Kanisa Kuu la Laterano   (@Vatican Media)

Masomo ambayo tumesikia yanaweza kutusaidia kuyatafakari. Katika Matendo ya Mitume (taz. 15:1-2.22-29), hasa, inasimuliwa jinsi jumuiya ya kwanza ilikabiliana na changamoto ya kufungulia ulimwengu wa kipagani katika kutangaza Injili. Haukuwa mchakato rahisi: ulihitaji uvumilivu mwingi na kusikilizana; hii ilitokea kwanza kabisa ndani ya jumuiya ya Antiokia, ambapo ndugu, kwa njia ya mazungumzo - hata majadiliano - walikuja kufafanua suala hilo pamoja. Lakini Paulo na Barnaba walipanda kwenda Yerusalemu. Hawakuamua wao wenyewe: walitafuta ushirika na Mama Kanisa na wakaenda huko kwa unyenyekevu. Huko walimkuta Petro na Mitume wakiwasikiliza. Ndivyo yalianza mazungumzo ambayo hatimaye yaliongoza kwenye uamuzi sahihi: kutambua na kuzingatia uchovu wa watu wapya, ilikubaliwa kutoweka mizigo mingi juu yao, bali kujiwekea kikomo kwa kuomba mambo muhimu (Mdo 15:28-29). Kwa hivyo, kile ambacho kingeonekana kama shida kikawa fursa kwa kila mtu kutafakari na kukua.

Maandishi ya Biblia, hata hivyo, yanatuambia zaidi, kwenda mbali ya mienendo tajiri na ya kuvutia ya kibinadamu ya tukio hilo. Hili linafunuliwa kwetu kwa maneno ambayo ndugu wa Yerusalemu wanawaambia, katika barua, kwa wale wa Antiokia, kuwajulisha maamuzi yaliyochukuliwa. Wanaandika: “Ikaonekana kuwa vyema [...] kwa Roho Mtakatifu na kwetu" (Mdo 15:28). Na wanasisitiza, yaani, kwamba katika historia nzima usikilizaji muhimu zaidi, ambao ulifanya kila kitu kingine kiwezekane, ulikuwa ni ule wa sauti ya Mungu. Wanatukumbusha, kwa hivyo, kwamba ushirika hujengwa kwanza kabisa "juu ya kupiga magoti", katika sala na katika kujitolea kwa kuendelea kwa uongofu. Ni katika mvutano huu tu, kiukweli, kila mtu anaweza kusikia ndani yake sauti ya Roho ikilia: "Abba! Baba!" (Gal 4:6) na kwa sababu hiyo wasikilize na kuwaelewa wengine kama ndugu.

Misa katika kanisa Kuu la Laterano
Misa katika kanisa Kuu la Laterano   (@Vatican Media)

Injili pia inarudia ujumbe huu kwetu (Yh 14:23-29), ikituambia kwamba katika chaguzi za maisha hatuko peke yetu. Roho hututegemeza na kutuonesha njia ya kufuata, “inatufundisha” na “kutukumbusha” yale yote ambayo Yesu alituambia  (Yh 14:26). Kwanza kabisa, Roho anatufundisha maneno ya Bwana, akikazia sana juu yetu, kulingana na mfano wa kibiblia wa sheria iliyoandikwa tena kwenye mbao za mawe, lakini ni katika mioyo yetu (Yer 31:33); zawadi ambayo inatusaidia kukua hadi kufikia hatua ya kuwa “barua ya Kristo” (2 Kor 3:3)  sisi kwa sisi. Na ndivyo ilivyo hasa: sisi sote tuna uwezo zaidi wa kutangaza Injili kadiri tunavyojiruhusu kushindwa na kubadilishwa kwayo, tukiruhusu nguvu ya Roho kutusafisha kwa ndani, kufanya maneno yetu kuwa rahisi, shauku zetu za uaminifu na wazi, matendo yetu ya ukarimu.

Kukumbuka

Na hapa kitenzi kingine kinatumika: "kumbuka", ambacho ni, kurudisha umakini wa moyo kwa yale ambayo tumepitia na kujifunza, kupenya kwa undani zaidi maana yake na kufurahiya uzuri wake. Ninafikiria, katika suala hili, juu ya njia yenye mahitaji ambayo Jimbo la Roma limekuwa likifuata katika miaka hii, iliyofafanuliwa katika viwango mbali mbali vya usikilizaji: kuelekea ulimwengu unaoizunguka, kukaribisha changamoto zake, na ndani ya jumuiya, kuelewa mahitaji na kukuza mipango ya busara na ya kinabii ya uinjilishaji na mapendo. Ni njia ngumu, ambayo bado inaendelea, ambayo inatafuta kukumbatia ukweli tajiri sana, lakini pia ngumu sana. Hata hivyo, inastahili historia ya Kanisa hili, ambalo mara nyingi limeonesha uwezo wake wa kufikiri "pakubwa", likitumia bila kujibakiza katika mipango ya ujasiri, na kujiweka mstari wa mbele hata katika hali mpya na changamoto.

Misa katika kanisa Kuu  huko Laterano
Misa katika kanisa Kuu huko Laterano   (@Vatican Media)

Shukrani kwa juhudi nyingi ya makaribisho

Ishara ya hii ni kazi kubwa ambayo Jimbo zima, katika siku hizi, linajitolea kwa ajili ya  Jubilei, katika kuwakaribisha na kuwatunza mahujaji na katika mipango mingine mingi. Shukrani kwa juhudi nyingi, jiji linaonekana kwa wale wanaokuja huko, wakati mwingine kutoka mbali sana, kama nyumba kubwa iliyo wazi na ya kukaribisha, na zaidi ya yote kama makao ya imani.

Kujitolea kusikiliza

Papa amesema kuwa “Kwa upande wangu, ninaeleza hamu na kujitolea kuingia katika eneo hili kubwa la ujenzi kwa kusikiliza, kadiri niwezavyo, kwa kila mtu, kujifunza, kuelewa na kuamua pamoja yaani kuwa: “Mkristo pamoja nanyi na Askofu kwa ajili yenu”, kama Mtakatifu Agostino alivyosema ( Hotuba 340, 1). Ninanaomba mnisaidie kufanya hivyo katika juhudi za pamoja za sala na mapendo, nikikumbuka maneno ya Mtakatifu Leo Mkuu:"Mema yote tunayofanya katika kutekeleza huduma yetu ni kazi ya Kristo; na sio kutoka kwetu, ambayo hatuwezi kufanya chochote bila yeye, lakini kutoka kwake tunamtukuza, ambaye ufanisi wote wa kazi yetu hutoka kwake" (Mahubiri 5, de natali ipsius, 4). Kwa maneno haya, kwa kumalizia, ningependa kuongeza yale ya Mwenyeheri Yohane Paulo wa Kwanza, ambaye mnamo tarehe 23 Septemba 1978, kwa uso wenye kung'aa na utulivu ambao tayari ulimpatia jina la utani la "Papa wa Tabasamu", aliisalimu familia yake mpya ya jimbo kwa njia hii: "Mtakatifu Pio X," alisema, "akiingia Venezia kama Patriarki, akitamka akiwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Marko: ningeonekanaje kwa wavenezia ikiwa nisingewapenda?

Misa katika Kanisa Kuu huko Laterano
Misa katika Kanisa Kuu huko Laterano   (@VATICAN MEDIA)

Ninasema kitu sawa na Waroma kuwa: Ninaweza kuwahakikishia kwamba ninawapenda, kwamba ninatamani tu kuingia katika huduma yenu na kuweka chini ya uwezo wangu wote duni, kidogo nilichonacho na nilicho” ( Mahubiri ya Kusimiwa katika Kanisa Kuu la Rma, 23 Septemba 1978). Mimi pia ninawaonesha upendo wangu wote, kwa hamu ya kushiriki nanyi, katika safari ya pamoja, furaha na huzuni, juhudi na matumaini. Mimi pia ninajitoa “kidogo nilichonacho na nilivyo,” na ninaikabidhi kwa maombezi ya Watakatifu Petro na Paulo na ya kaka na dada wengine wengi ambao utakatifu wao umeangazia historia ya Kanisa hili na mitaa ya jiji hili. Bikira Maria atusindikize na kutuombea. Baada ya misa kabla ya Baraka , Papa Leo alitoa zawadi ya kikombe kwa Makamu wake kama ishara ya ubaba. Na baadaye akatoa baraka.

Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano
Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano   (@Vatican Media)

Maneno ya Papa akiwa katikati ya dirisha la Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane


Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa katikati ya dirisha la Kanisa kwa ajili ya Baraka ya mji wa Roma, mara baada ya Misa Takatifu na baraka ya kwanza ya mjini wa Roma, alizungumza bila kusoma akianza  na:  “Amani iwe nanyi!” Ndugu wapendwa, jumuiya ya Roma, ninayo furaha kubwa kuwa pamoja nanyi jioni ya leo, katika tendo hili la kiliturujia, ambamo tumeadhimisha kusimikwa kwangu kama Askofu wenu mpya wa Roma. Asanteni nyote! Kuishi imani yetu, hasa katika Mwaka huu wa Jubilei, tukitafuta matumaini; lakini tukijaribu kuwa sisi wenyewe shahidi ambao wanatoa tumaini kwa ulimwengu."

Papa akitoa baraka na salamu
Papa akitoa baraka na salamu   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo vile vile alisema kuwa "Ulimwengu unaoteseka sana, uchungu mwingi, kutokana na vita, jeuri, umaskini! Lakini Bwana anatuomba sisi Wakristo kuwa daima mashuhuda hawa walio hai. Kuishi imani yetu, kuhisi mioyoni mwetu kwamba Yesu Kristo yupo na kujua kwamba Yeye hutusindikiza daima katika safari yetu. Asante kwa kutembea pamoja! Sote tutembee pamoja! Daima niombeeni, ambaye pamoja nanyi ni Mkristo na kwa ajili yeni ni Askofu. Asanteni nyote!” Papa alihitimisha kwa kutoa Baraka na kuwatakia jioni njema wote na kusema kuwa tuishi na furaha hii kila wakati. Asante.”

Papa akisalimia waamini
Papa akisalimia waamini   (@Vatican Media)
Mahubiri ya Papa huko Laterano
25 Mei 2025, 17:42