ÐÓMAPµ¼º½

2025.05.22 Partecipanti all'Assemblea Generale delle Pontificie Opere Missionarie

Papa amemteua Kardinali Tagle kuwa Kardinali Askofu wa Kanisa la Albano

Papa amemteua Kardinali Tagle kuwa Kardinali Askofu kwa kumpatia Kanisa la Albano.Ni Kanisa lile lile ambalo hadhi ya Kardinali Prevost wa wakati huo alikuwa amepata mnamo,mwezi Februari na Papa Francisko alipomteua kuwa Kardinali Askofu.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV amempatia  hadhi ya Kardinali Askofu kwa kumpatia Kanisa la Albano Kardinali Luis Antonio G. Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Mapya Mahalia. Ni Kanisa lile lile ambalo hadhi yake ya Kadinali Prevost wa wakati huo,  alikuwa ameipata, mnamo mwezi  Februari 6 iliyopita kutoka kwa  Papa Francisko alipomteua kuwa katika  Daraja la Maaskofu.

Sasa ni chaguo la Tagle, Kardinali ambaye katika Misa ya mwanzo wa upapa wake alimpatia Papa pete ya Mvuvi. Kardinali wa Ufilipino pia amejumuishwa katika Daraja la Maaskofu, ambalo Papa Francisko pia aliamua kupanua idadi ya washiriki mnamo 2018. Hadi wakati huo, kiukweli, liliundwa na makardinali wakuu wa majimbo ya miji.

24 Mei 2025, 13:59