Papa amemteua Kardinali Tagle kuwa Kardinali Askofu wa Kanisa la Albano
Papa amemteua Kardinali Tagle kuwa Kardinali Askofu kwa kumpatia Kanisa la Albano.Ni Kanisa lile lile ambalo hadhi ya Kardinali Prevost wa wakati huo alikuwa amepata mnamo,mwezi Februari na Papa Francisko alipomteua kuwa Kardinali Askofu.
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV amempatia hadhi ya Kardinali Askofu kwa kumpatia Kanisa la Albano Kardinali Luis Antonio G. Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Mapya Mahalia. Ni Kanisa lile lile ambalo hadhi yake ya Kadinali Prevost wa wakati huo, alikuwa ameipata, mnamo mwezi Februari 6 iliyopita kutoka kwa Papa Francisko alipomteua kuwa katika Daraja la Maaskofu.
Sasa ni chaguo la Tagle, Kardinali ambaye katika Misa ya mwanzo wa upapa wake alimpatia Papa pete ya Mvuvi. Kardinali wa Ufilipino pia amejumuishwa katika Daraja la Maaskofu, ambalo Papa Francisko pia aliamua kupanua idadi ya washiriki mnamo 2018. Hadi wakati huo, kiukweli, liliundwa na makardinali wakuu wa majimbo ya miji.
24 Mei 2025, 13:59