Papa akutana na marais wa Ukraine na Peru
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV alikuwa na mikutano miwili mjini Vatican nje ya maadhimisho ya Ekaristi katika mwanzo wa huduma ya Mtakatifu Petro, Dominika tarehe 18 Mei 2025.
Kwanza alimsalimia Rais wa Peru Bi Dina Ercilia Boluarte Zegarra ambaye aliandika kwenye X kwamba amempelekea Papa ukaribu wa upendo wa watu wa Peru. Kisha akamkumbuka Askofu mpya wa Roma, kama “mtumishi wa Mungu aliyejitolea miaka mingi kwa ajili ya utume wa Injili na kuwahudumia wahitaji zaidi nchini.”
Baadaye Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky pamoja na mkewe Olena Zelenska.
Pia rais huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa X shukrani zake kwa maneno yaliyotamkwa kwenye sala ya Malkia wa Mbingu kuhusu Ukraine hasa "kuhusu hitaji la amani ya haki" kwa sababu "kila taifa linastahili kuishi kwa amani na usalama."
Kisha katika ukuras huo alitoa matashi mema ya utume anaoitiwa Papa kwa matumaini kwamba, sala za "amani ya haki na maisha ya utu kwa wote zitasikika.”