Mwanzo wa huduma ya mfuasi wa Mtume Petro wa Papa Leo XIV
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika mahubiri ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuanza kwa huduma ya Mtume Petro, Dominika ya tano ya Pasaka, tarehe 18 Mei 2025, Askofu wa Roma alirejea siku za uchungu za kifo cha Baba Mtakatifu Francisko, huku akionesha huzuni na hisia ya kuachwa kwa umati wa watu walioachwa bila Mchungaji. Umati ambao, hata hivyo, uliishi kila kitu katika nuru ya Ufufuko wa Pasaka, kwa uhakika kwamba Mungu anatembea kando kando ya kila mmoja na kwamba anakusanya kundi lake lililotawanyika.
Papa Leo XIV aliakisi mkutano mkuu wa uchaguzi/ Conclave, uliojumuisha historia na njia tofauti, ambayo mikononi mwa Mungu inatoa chaguo la Papa mpya, mlezi wa imani ya Kikristo na kwa mtazano wa mbali ili kukabiliana na mahitaji, mahangaiko na changamoto za leo hii. Papa Leo alisisitiza kuwa Petro ni mvuvi wa watu, kama vile Mwalimu alivyomfundisha kwa kuwaokoa wanadamu kutoka katika maji ya uovu, na ni juu yake na wanafunzi kutupa wavu wa kuzamisha tumaini la Injili katika maji ya ulimwengu, ili kuvuka bahari ya uzima ili kila mtu aweze kujikuta katika kumbatio la Mungu.
Swali la Kharifa wa mtume Petro ilikuwa ni: Je, Petro anawezaje kutekeleza kazi hii? Jina la Papa Leo ni kwamba “Injili inatuambia kwamba inawezekana tu kwa sababu amepitia katika maisha yake mwenyewe ya upendo usio na kikomo na usio na masharti wa Mungu, hata katika saa ya kushindwa na kukataa. Mungu hujitoa mwenyewe bila kutoridhishwa au hesabu na kwa kuguswa tu na upendo huu hupelekea kuwa zaidi ya kutoa, kutoa maisha kwa ajili ya ndugu zake.
Papa Leo XIV alielekeza majisterio ya Papa, akiiegemeza juu ya upendo wa Kristo, katika mapendo na bila mahali pa kupumzika; maneno ambayo yanatukumbusha yaliyotamkwa na Papa Benedikto wa kumi na sita, ambaye pia yalipendwa na Hayati Papa Francisko, ambaye kwa mujibu wake “Kanisa halikui kwa njia ya kuongoa watu imani, hukua kwa mvuto, kwa njia ya ushuhuda.”
Huduma ya Petro inaakisiwa hasa na upendo huu wa kujitolea, kwa sababu Kanisa la Roma linasimamia kwa upendo na mamlaka yake ya kweli ni upendo wa Kristo. Si jambo la kuwateka wengine kwa dhuluma, propaganda za kidini au njia za mamlaka, lakini daima ni suala la upendo kama Yesu alivyofanya. Upendo unaobadilika na unaotuhitaji kulinda mawe yaliyo hai, wanaume, wanaoitwa kujenga jengo la Mungu katika ushirika wa kidugu, katika upatano wa Roho, katika kuishi pamoja kwa utofauti, bila ubinafsi.
Ni lazima Petro alichunge kundi bila kujiingiza katika majaribu ya kuwa kiongozi peke yake au chifu aliyewekwa juu ya wengine, akijifanya kuwa bwana wa watu waliokabidhiwa kwake (rej. 1Pt 5:3); kinyume chake, anaombwa kutumikia imani ya ndugu zake, akitembea pamoja nao. Kanisa lenye umoja, ishara ya umoja na ushirika, ambayo inakuwa chachu kwa ulimwengu uliopatanishwa. Kanisa kama chachu ndogo ya umoja, ya ushirika, ya udugu ambayo inataka kuuambia ulimwengu, kwa unyenyekevu na furaha kwamba Neno la Kristo linafariji, linaangazia, kwamba ni pendekezo la upendo linalofanya kila mtu kuwa familia moja.
Na hii ndiyo njia ya kuchukua pamoja, miongoni mwetu bali pia na dada Makanisa ya Kikristo, na wale wanaofuata njia nyingine za kidini, pamoja na wale wanaokuza kutotulia kwa kumtafuta Mungu, pamoja na wanawake na wanaume wote wenye mapenzi mema, ili kujenga ulimwengu mpya ambamo amani inatawala. Papa leo XIV alisema “Kaka na dada, hii ni saa ya upendo! Upendo wa Mungu unaotufanya kuwa ndugu miongoni mwetu ndio moyo wa Injili...tujenge Kanisa linalosimikwa katika upendo wa Mungu na ishara ya umoja, Kanisa la kimisionari, linalofungua mikono yake kwa ulimwengu, linalotangaza Neno, linalojiruhusu kuhangaika kwa historia, na ambalo linakuwa chachu ya maelewano kwa wanadamu.”