Msalaba wa kifuani kwa Papa Leo XIV
Na Tiziana Campisi na Angella Rwezaula–Vatican.
Ndugu msomaji wa Vatican News kuna mambo ambayo unapaswa kuyatambua hatua kwa hatua katika mwanzao wa Upapa wa Papa Leo XIV. Katikati ni masalia ya Mtakatifu Agostino, Baba wa Kanisa, anayetufundisha kufuata njia ya mambo ya ndani ili kumpata Mungu na kuelewa Neno lake kwa imani na akili na kisha kuwashirikisha wengine. Kuna ujumbe wa thamani na wa kina unaopaswa kushikwa katika msalaba wa kifuani aliovaa Papa Leo XIV mnamo tarehe 8 Mei 2025, siku ya kuchaguliwa kwake, alipojiwasilisha kwa ulimwengu akitazama kutokea katikati ya Dirisha la Basilika ya Mtakatifu Petro.
Ndani yake pamoja na kipande cha mifupa ya Askofu wa Hippo, baba wa kiroho wa Shirika la Mtakatifu Agostino, ambaye kwa Utawala wake na maandishi yake aliwavuvia Ndugu wengi, watawa, masista na walei kukumbatia Injili kama wajenzi wa ushirika na wahamasishaji wa wema wa wote, kuna masalia mengine manne ambayo ni ya: Mtakatifu Monica, upande wa juu, ya Mtakatifu Thomas wa Villanova, upande wa kushoto, ya Mwenyeheri Anselmo Polanco, upande wa kulia na ya Mwenyeheri Giuseppe Bartolomeo Menochio chini yake.
Zawadi kutoka kwa Makao makuu ya Shirika
Padre Josef Sciberras mwendesha mchakato wa kutangazwa watakatifu katika Shirika la Waagostiniani, aliwachagulia zawadi Makao makuu ya Shirika kumpatia nduhu yao Robert Prevost, siku aliyoundwa kuwa Kardinali, kunako tarehe 30 Septemba 2023, na hiyo zawadi inaibua sura za utakatifu zilizounganishwa na familia ya Shirika la Mtakatifu Agostino ambalo inajumuisha uaminifu, mageuzi, huduma na kifodini. Mtawa huyo ambaye hakuficha furaha yake katika kuchaguliwa kwa Papa mpya akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican, alisema kwamba: Kardinali Prevost wa wakati huo "alisisimka" alipopewa Msalaba wa kifuani, wakati wa sherehe iliyoandaliwa kwa ajili yake katika Jumba la maonesho la Chuo cha Kimataifa cha Mtakatifu Monica, akifahamu kwamba atakuwa na masalia ya Mtakatifu Agostino na mama yake Monica kifuani.
"Siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, Jumanne iliyopita, nilimtumia ujumbe nikipendekeza avae msalaba ambao tulimpatia, ili kupata ulinzi wa Watakatifu wa Mtakatifu Agostino na Monica, alibainisha Padre Sciberras alioneza kuwa “sina hakika kwamba aliuvaa kwa sababu ya pendekezo langu, lakini nilipoona kwamba alikuwa amevaa kwa ajili ya kiapo na kwamba alikuwa amevaa wakati wa kutazama nje ya Kanisa Kuu la Vatican akiupendelea kuliko mwingine ambao angeweza kuchagua, nilifurahi sana.”
Agostino na Monica
Sehemu hiyo ya mifupa ya Askofu wa Hippo katika msalaba wa kifuani wa Papa Leo XIV pia unataka kukumbuka Shirika la Mtakatifu Agostino, ambalo, lililoanzishwa na Vatican mnamo 1244, limechukua hatua kwa hatua msimamo wake bora wa maisha, likitoa matunda ya utakatifu kwa karne nyingi kwa njia ya maisha ya kijumuiya, kazi kubwa ya kitume, mafunzo ya kiroho, mafundisho ya Baba wa Kanisa Agostino na tasaufi yake. Kwa njia hiyo Masalia ya Mtakatifu Monica pia ni ishara ya uhusiano wa Agostino na mama yake, mwanamke shupavu na mstahimilivu ambaye kwa machozi yake na maombi yake bila kuchoka mwanae alipata kuongoka. Kwa njia hiyo kuchaguliwa kwake ni kama zawadi kutoka kwa Mungu. Hata Hayati Papa Francisko alijitolea sana, mara nyingi alitembelea kaburi katika Kanisa la Mtakatifu Agostino lililoko Campo Marzio jijini Roma, wakati wote alipokuwa Kardinali na kama Papa.
Mtakatifu Maonica hawezi kutengenishwa na Monica mama yake
Kwa Shirika la Mtakatifu Agostino, sura ya Monica haiwezi kutenganishwa na uzoefu wa uongofu na kuwekwa wakfu kwa mwanawe, msingi wa kiroho wa Waagostiniani. Mtakatifu Thomas wa Villanova, Askofu Mkuu wa Valencia, aliyeishi kati ya karne ya 15 na 16, alikuwa mrekebishaji wa maisha ya kitawa. Yeye ni kielelezo cha mchungaji mkamilifu kwa kundi lake, "kwa harufu ya kondoo wake, kutumia usemi unaopendwa sana na Papa Francis", anaongeza Padre Sciberras. Alikuwa na umakini mkubwa kwa maskini na alikuza misheni katika Ulimwengu Mpya. Mwanatheolojia mkuu, mnamo 1550 alianzisha seminari huko Velencia, Uhispania - bado hai hadi leo - kabla ya Baraza la Trento kudhibiti malezi ya mapadre.
Thomas wa Villanova
Mtakatifu Thomas wa Villanova, Askofu Mkuu wa Valencia, aliyeishi kati ya karne ya 15 na 16, alikuwa mrekebishaji wa maisha ya kitawa. Yeye ni kielelezo cha mchungaji mkamilifu kwa kundi lake, "kwa harufu ya kondoo wake, kutumia usemi uliopendwa sana na Hayati Papa Francisko", aliongeza Padre Sciberras. Alikuwa na umakini mkubwa kwa maskini na alihamasisha misheni katika Ulimwengu Mpya. Mtaalimungu mkuu, mnamo 1550 alianzisha seminari huko Velencia, Hispania ambayo bado iko hai hadi leo kabla ya Mkutano wa Trento kudhibiti malezi ya mapadre.
Anselmo Polanco
Mwenyeheri Anselmo Polanco, Askofu wa Teruel, shahidi wa mateso ya kidini nchini Hispania (1936-1939), ndiye mchungaji aliyetoa maisha yake hadi mwisho kwa ajili ya roho zilizokabidhiwa kwake. Kwa ke yeye alisema: “Kama hata jimbo langu moja nitabaki." Na alibaki mwaminifu kwa watu wake na kwa Papa, alipigwa risasi kwa ushuhuda wake wa imani na kwa nguvu ya neno lake la kiinjili.
Bartolomeo Menochio
Giuseppe Bartolomeo Menochio, Askofu wa Porfirio na Mkuu wa Sakrestia ya kipapa tangu 1800, alitumikia Kanisa kwa ujasiri wakati wa dhoruba ya utawala wa Napoleon, akiwa thabiti katika imani na pia mwaminifu kwa Papa hata katika nyakati ngumu zaidi. Ni muhimu kurejea kwa Kanisa la Roma, alikufa akiwa na sifa ya utakatifu mnamo tarehe 25 Machi 1823. Mnamo 1991, Papa Paulo II alitambua ushujaa wa fadhila zake. Alimwakilisha mchungaji, kuwa ndiye Askofu pekee ambaye hakutaka kula kiapo cha utii kwa Napoleon na ambaye alijitolea kabisa kwa watu wa Roma.
Tamko la imani, mwelekeo wa kichungaji
Mabaki ya Watakatifu Agostino, Monica, Thomas wa Villanova, Mwenyeheri Polanco na Mtumishi wa Mungu Menochio yalikuwa yamehifadhiwa katika Eneo maalum la Ofisi ya mwendesha mchakato wa kutangazwa watakatifu, katika Nyumba Mama wa Shirika hilo na Padre Sciberras ambaye aliyakabidhi kwa Antonino Cottone Kifaa hicho cha Masalia ili kuwaweka kwenye msalaba wa kifuani baadaye yakakabishwa kwa kaka yao ambaye sasa ni Papa Leo wa XIV.
Kwa mujibu wa maelezo alisema kuwa:"Si mapambo rahisi lakini ni taaluma inayoonekana ya imani na mwelekeo wa kweli wa kichungaji. Masalia yaliyomo ndani ya Msalaba huo kwa hiyo yanaibua takwimu za utakatifu zinazohusishwa na Shirika la Agostiniani ambalo linajumuisha uaminifu, mageuzi, huduma na kifo cha kishahidi:mambo yote ambayo yanaakisi na kusaidia huduma ya Papa mpya," alisema mwanashirika huyo.
Asante sana kwa kusoma makala hii. Ikiwa unataka kujua masasisho mengine,tunakualika ujiandikishwa kwa kubonyeza hapa: cliccando qui