Misa ya kumbukizi ya kupigwa risasi Papa Yohane Paulo II
Vatican News
Miaka 44 iliyopita, kunako tarehe 13 Mei 1981, Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa mwathirika wa shambulio katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Ili kukumbuka tukio hilo, Jumanne tarehe 13 Mei 2025, saa 12 jioni masaa ya Ulaya katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Kardinali Stanislaw Dziwisz ambaye wakati huo alikuwa katibu wa Papa wa Poland, aliongoza Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kiti cha Mtakatifu Petro na kukiwa na ushiriki wa wazi kwa wote. Baada ya adhimisho la kiliturujia, yalifanyika maandamano kutoka kwenye madhabahu ya Mtakatifu Petro hadi kwenye kaburi la Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili liliko pembeni kulia mwa Kanisa Kuu hilo.
Siku aliyopshabuliwa na risasi Mtakatifu Yohane Paulo II
Risasi ziligeuzwa na mkono wa Mpaji tu
Siku hiyo mnamo mwaka 1981, saa 11:17 jioni., Papa Wojtyla alikuwa akizunguka katika Uwanja akiwa juu ya Gari la Papa (ÐÓMAPµ¼º½mobile )mbele waamini walioudhuria Katekesi ya Jumatano, wakati alipoanguka ghafla, akijeruhiwa na risasi zilizofyatuliwa na Ali Agca. Papa alihamishiwa mara moja haraka katika hospitali ya Gemelli jijini Roma. Alifanyiwa upasuaji, akipambana na uhai wake, na akaokolewa. Daima alikuwa na imani kwamba ni Mama Yetu wa Fatima, ambaye ukumbusho wake wa kiliturujia huadhimishwa kila ifikapo Mei 13, ambaye "amepindua risasi" na kuokoa maisha yake.
Vikasha vya maganda ya risasi zilizorushwa na Ali Agca.
Msaada wa Mama wa Mbinguni
Mwaka mmoja baada ya shambulio hilo, Mtakatifu Yohane Paulo II alitembelea Madhabahu ya Fatima kumshukuru Bikira. Aliwaambia waamini waliokuwa wakimsikiliza: "Ningependa kuwaambia kwa ujasiri kwamba wakati shambulio lilifanyika mwaka mmoja uliopita katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, nilipopata fahamu, mawazo yangu mara moja yalikimbilia kwenye Madhabahu hii kutoa shukrani kwa Moyo wa Mama wa Mbinguni. Katika yote yaliyotokea, niliona - na nitarudia tena na tena - ulinzi maalum wa uzazi wa Maria."