ÐÓMAPµ¼º½

2025.05.08 Uchaguzi wa Papa wa Roma:Papa Leo XIV. 2025.05.08 Uchaguzi wa Papa wa Roma:Papa Leo XIV.  (@Vatican Media)

Kutokea kwa Papa Leo XIV na mavazi ya kiutamaduni

Papa Leo XIV alionekana kwa mara ya kwanza katikati ya dirisha la Basilika ya Mtakatifu Petro mjini Vatican,tarehe 8 Mei 2025 mara baada ya kuchaguliwa,akiwa amevalia mavazi ya kiutamaduni ambayo yalivaliwa na mapapa wengine waliotangulia kama vile Papa Yohane Paulo II,Benedikto XVI lakini haikuwa kwa Papa Francisko.Mavazi haya yana maana gani?

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Leo XIV alirejea kuvaa mozzetta nyekundu ambayo inakumbusha nafasi ya mchungaji mkuu wa Kanisa. Tofauti na siku za nyuma, mozzetta hii ya Papa Leo XIV haina mshazari ulioizungukia, kama zilivokuwa za wakati uliopita bali rahisi tu.  Kwa kuongezea, Papa Leo XIV alivaa msalaba wa kifuani wa dhahabu pia nao ni nembo ya Papa na ishara ya mamlaka ya kichungaji, ambayo inaashiria tofauti ikilinganishwa na ile ya Papa Francisko. Mavazi haya ya kipapa,  tayari yalivaliwa na Papa Yohane Paulo II na Benedikto XVI walipojiwasilishwa kwa ulimwengu katikati ya dirisha kuu la Basilika ya Mtakatifu Petro. Mozzetta (Mantellina) ni moja ya nguo zinazotambulika na za mfano zinazovaliwa na Papa enzi zote, zimejaa historia na maana ya kiliturujia. Aina hii ya joho fupi, naonekana rahisi, ni ya karne za tamaduni  na kuwakilisha moja ya vipengele tofauti vya mavazi ya kipapa.

Papa Leo alijitokea akiwa amevaa Vazi hili la kiutamaduni
Papa Leo alijitokea akiwa amevaa Vazi hili la kiutamaduni   (@Vatican Media)

Muundo wa Mozetta ya Papa iko namna gani?

Kama tulivyosema ni fupi, nafungwa kwenye kifua na vifungo vya mfululizo, ambavyo huvaliwa juu ya mavazi ya kwaya, (surplice au rochet.)  cotta o il rocchetto. Kwa kawaida ina kama kikofia kidogo, kinachoitwa cocullo, ambapo katika muktadha wa Papa Leo XIV akipo bali kilionekana kwa  mapapa waliotangulia, wa enzi za kale, na wakati huo huo ilifutwa kwa wakuu wengine wa kikanisa baada ya Mtaguso wa Pili wa Vatican. Mozzetta hufunika mabega, sehemu ya kifua na mikono, na huvaliwa wakati wa sherehe maalum na vitendo vya umma tu.

Madhumuni ya mozzetta ni nini?

Mozzetta inatumika iwe shughuli ya ishara na ya vitendo. Kwa mtazamo wa mfano, ni ishara ya kisheria na mamlaka ya kikanisa: yeyote anayevaa anadhihirisha jukumu la serikali na mwongozo ndani ya Kanisa Katoliki. Kwa upande wa Papa, mozzetta hiyo inakuwa ishara inayoonekana ya ukuu wake na kazi yake ya kichungaji kama mkuu wa Kanisa la ulimwengu wote. Katika historia, mozzetta pia imekuwa ikivaliwa na washiriki wengine wa makuhani, kama vile makardinali, maaskofu, maabati na wanasheria wa kikanisa, na rangi ni tofauti na vifaa kulingana na hadhi yao na kipindi cha kiliturujia. Walakini, mozzetta ya kipapa inatofautishwa na sifa zingine za kipekee, miongoni mwake uwepo wa aina ya kikofia na wingi wa vifaa vilivyotumika kuitengeneza. Mbali na thamani yake ya mfano, mozzetta awali pia ilikuwa na asili hata ya kazi ya vitendo kwa mfano ilikuwa ni kujilinda kutokana na  baridi wakati wa maadhimisho ya muda mrefu katika Basilika zisizo na joto. Leo hii kazi hiyo haipo tena  katika maadhimisho kwa hiyo ni ya kuwakilisha tu.

Tazama Vazi alilotokea nalo Papa Leo XIV
Tazama Vazi alilotokea nalo Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Nyenzo na rangi ya mozzetta ya kipapa

Mozetta ya Papa inatofautishwa na aina ya vifaa   na rangi, ambayo hubadilika kulingana na wakati na hali ya kiliturujia: Vazi la hariri nyekundu yenye kuzungukwa na mshazari: iliyotumiwa kutoka Novemba 1 hadi Pasaka, inawakilisha maadhimisho ya nyakati muhimu za mwaka wa liturujia na Hadhi ya jukumu la kipapa

Hariri nyekundu: huvaliwa kutoka Pentekoste hadi Oktoba 31, ni toleo rahisi na nyepesi, linalofaa kwa nyakati za kawaida. Damaski nyeupe iliyozungukwa na mshazari: inayotumiwa wakati wa Pasaka, inaashiria usafi na furaha ya Ufufuko.

Damaski nyeupe bila mshazari uliofumwa wa rangi ya fedha: iliyoletwa kwa vipindi vya joto vya Wakati wa Pasaka, pia inajibu kwa haja ya vitendo na faraja. Aina hizi za Mozzetta zimetengenezwa kwa vitambaa vya hariri na damaski, mara nyingi hupambwa kwa urembeshwaji wa dhahabu na ushonaji wa hali ya juu wa kikanisa.

Mshazari wa fedha, uliopo katika matoleo ya siku kuu kubwa zaidi,unasisitiza zaidi hadhi na heshima jukumu la  upapa.

Papa Francisko alitokea kwa mara ya kwanza akiwa amevaa vazi  hili
Papa Francisko alitokea kwa mara ya kwanza akiwa amevaa vazi hili

Mozzetta katika sherehe za upapa

Matumizi ya mozzetta na Papa yameimarishwa tangu mwishoni mwa zama za Kati, na kuwa kipengele tofauti cha mavazi yake ya umma. Kwa karne nyingi, sherehe hiyo imejumuisha matumizi ya mozzetta katika hafla ya vitendo vizito, kama vile kumiliki Basilika ya Laterano, sherehe kuu za kiliturujia na Katekesi. Kipengele cha kuvutia ni kwamba mozzetta ya kipapa ndiyo pekee ya kuhifadhi kikofia kidogo, mara moja kutumika kufunika kichwa, japo kuwa kwa leo hii inaweza kuwa mapambo tu.

Papa Yohane Paulo II naye alikuwa amefaa hivi
Papa Yohane Paulo II naye alikuwa amefaa hivi

Maendeleo na matukio ya sasa

Katika karne ya ishirini, matumizi ya mozzetta ya kipapa yalipata mabadiliko fulani. Kwa mfano Papa Yohane Paulo II alivaa tu katika hafla maalum, wakati Papa Benedikto XVI alipata matumizi ya matoleo tofauti, ikijumuisha ile ya hariri nyekundu yenye kuzungukia mshazari wa fedha na damaski nyeupe, ikipanua matumizi yake hata nje ya nyakati kuu za kiliturujia.

Kwa upande wa  Papa Francisko, hata hivyo, mozzetta ilikuwa karibu kuachwa kabisa, kulingana na mtindo wake wa  kiasi zaidi na usio rasmi. Tunakumbuka Papa wa Argentina alichagua kutoivaa hata wakati wa kuonekana kwake hadharani kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa kwake kunako tarehe 13 Machi 2013.

Papa Paulo I alikuwa amevaa hivi alipojitokeza mbele ya ulimwengu
Papa Paulo I alikuwa amevaa hivi alipojitokeza mbele ya ulimwengu
Mavazi ya Kipapa na Liturujia ya Asmara na Ethiopia,Mei 12
13 Mei 2025, 09:18