Kubatilishwa kwa Pete ya Mvuvi
Vatican News
Wakati wa Mkutano Mkuu wa kumi na mbili, Makardinali 173 walijadili mada kuu za Kanisa: Amani, Mazingira, Sinodi na mageuzi ya Papa Francisko. Kitambulisho cha "upapa na mchungaji" kiliainishwa. Pete ya mvuvi na mihuri ya upapa ilibatilishwa. Wito wa kusitisha mapigano katika maeneo ya vita ilibanishwa. Ni katika maelezo yaliyotolewa na msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, asubuhi ya leo tarehe 6 Mei 2025 katika mkutano mkuu wa kumi na mbili wa makardinali ulioanza saa 3:00 kwa muda wa maombi ya pamoja. Makardinali 173 walikuwepo, wakiwemo wapiga kura 130. Hotuba 26 zilishughulikia masuala mengi. Marekebisho ya Papa Francisko ambayo yanahitaji kuendelezwa kama vile: “sheria juu ya unyanyasaji, suala la kiuchumi, Curia Romana, sinodi, kazi ya amani, utunzaji wa kazi ya uumbaji. Mada ya Ushirika pia ilisisitizwa kama wito kwa Papa mpya, ili awe mjenzi wa madaraja, na mchungaji, mwalimu wa ubinadamu na uso wa Kanisa la Kisamaria.”
Katika majadiliano hato pia kipindi cha vita, vurugu na ubaguzi wa kina vilizungumzwa na zaidi awe Papa wa huruma, sinodi na matumaini inahitajika. Kadhalika walizungumza kuhusu Sheria ya Kanisa na uwezo wa Papa, kuhusu migawanyiko na namna ya kuwa makardinali katika Kanisa, kuhusu ukaribu wa Sherehe ya Kristo Mfalme na Siku ya Maskini, ilithibitishwa kwa pamoja, kuhusu hitaji la mikutano ya Baraza la Makardinali kwenye hafla ya Mkutano wa uchaguzi wa Makardinali wapya. Kuanzishwa na malezi ya Kikristo kama matendo ya kimisionari yalijadiliwa, kumbukumbu ya ushuhuda wa mashahuda wa imani katika nchi zenye migogoro na ambapo kuna mipaka ya uhuru wa kidini na suala la dharura la mabadiliko ya tabia nchi. Mada ya tarehe ya Pasaka, Baraza la Nicea na mazungumzo ya kiekumene yalitajwa. Wito ilisisitizwa kwa pande zinazohusika kwa usitishaji vita wa kudumu na mazungumzo katika baadhi ya hali za migogoro, ambapo amani ya haki na ya kudumu inaombwa.
Na wakati wa mkutano wa asubuhi kwa njia hiyo, Pete ya mvuvi Mchungaji ilibatilishwa. Hii ni pete ya mchungaji Papa ambayo haikuvunjwa kwa mujibu wa Ordo Exsequiarum Romani Ponteficis ,yaani “Kanuni za mazishi ya Papa wa Roma” iliyoidhinishwa na Papa Francisko kunako tarehe 29 Aprili 2024. Pete ya Kipapa ya Papa Francisko ilikuwa ya Fedha iliyong’arishwa. Na ilikuwa inawakilishwa na picha ya Petro na ufunguo. Na pia imefuatwa Muhuri wake aliokuwa anautumia.
Mkutano uliisha saa 6.30 mchana. Hakuna Makutano mwingine Mkuu uliopangwa. Baadhi ya maelekezo halisi za nyakati yalitolewa: Kesho asubuhi tarehe 7 Mei 2025 saa 4:00 kamili asubuhi Misa kabla ya (pro eligendo Pontifice,) ya uchaguzi wa Papa itafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Kisha saa 9:45 alasiri, Makardinali watahamia kutoka Nyumba ya Mtakatifu Marta hadi Jumba la Kitume wakiwa wamevalia nguo za kwaya kwa ajili ya kuingia kwenye (Conclave,)mkutano mkuu.
Kuanzia Alhamisi:
Saa 1:45 asubuhi Makardinali watatoka katika nyumba ya Mtakatifu Marta hadi Jumba Kuu la Kitume
Saa 2:15 asubuhi, Misa Takatifu na Masifu katika kikanisa cha Paolina
Saa 3:15 asubuhi Masifu ya Kati katika Kikanisa cha Sistine na kura.
Kuonekana Moshi ikiwa inawezakana: ni baada ya saa 4.30 asubuhi na baada ya saa 6.00 mchana masaa ya Ulaya.
Saa 6:30 mchana ni kurudi tena nyumba ya Mtakatifu Marta kwa chakula cha machana.
Saa 9.45 alasiri kwenda tena Jumba la Kitume
Saa 10.30 jioni kupiga kura katika Kikanisa cha Sistine.
Moshi utatokea ikiwezekana: baada ya saa 11:30 jioni na ndani ya saa 1.00 za jioni.
Baada ya kura kuna masifu ya jioni katika kikanisa cha Sistine
Saa 1.30 jioni ni kurudi katika Nyumba ya Mtakatifu Marta.
Haya ndiyo yalikuwa ni maelezo yaliyofafanuliwa na Dk. Bruni Msemaji wa Vyombo vya habarina kuweka wazi kwamba kuonekana kwa moshi kutakuwa ni baada ya saa 4.30 za asubuhi na baada ya saa 11.30 jioni ikiwa kutakuwa na uchaguzi yaani moshi mweupe.