Jiji la Roma linatoa heshima kwa Papa Leo XIV
Vatican News
Katika Uwanja wa Ara Coeli, chini ya ngazi za kilima cha Manispaa, Papa Leo XIV atapokea heshima kutoka kwa Jiji la Roma kwa mikono ya Meya wa mji, Bwana Roberto Gualtieri. Katika taarifa iliyotolewa kutoka Vyombo vya habari Vatican ilitangaza kuwa tukio hilo litafanyika saa 10:15 jioni, Dominika, tarehe 25 Mei, 2025, siku ambayo Papa Leo XIV ataongoza adhimisho la Ekaristi Takatifu na kusimikwa kwenye Kanisa Kuu la Roma kuwa Askofu wa Roma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterano.
Katika taarifa hiyo inabainisha kuwa mara baada ya liturujia, Baba Mtakatifu ataonekana kutokea katikati ya Kanisa Kuu la Lateranoili kubariki mji wa Roma. Saa 1 jioni, Papa atahamia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kwa muda wa maombi mbele ya Picha ya Bikira Maria Salus Populi Romani( Afya ya Waroma.)