ĐÓMAPµĽş˝

Serikali ya Italia inapenda kuunga mkono juhudi za Vatican katika kutafuta, kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano Serikali ya Italia inapenda kuunga mkono juhudi za Vatican katika kutafuta, kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano 

Italia na Vatican Kuendelea Kushirikiana Katika Kukuza Amani

Waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni, amezungumza kwa njia ya simu na Baba Mtakatifu Leo XIV, ametumia fursa hii, kumpongeza Baba Mtakatifu Leo XIV kwa kuchaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki na kwamba, kuna uhusiano wa pekee kati ya Italia na Khalifa wa Mtakatifu Petro. Serikali ya Italia inapenda kuunga mkono juhudi za Vatican katika kutafuta, kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano sehemu mbalimbali za dunia. Kuna uhusiano mwema!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mtakatifu Yohane XXIII katika Wosia wake wa Kitume, “Pacem in terris” yaani “Amani Duniani” anasema amani inasimikwa katika: ukweli, haki, upendo na uhuru. Kumbe, kuna haja ya kukuza na kudumisha utamaduni wa kuheshimu: utu, heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu sanjari na haki msingi za binadamu na kwamba, kila mtu anapaswa kuwajibika, ili kujenga na kuimarisha mafungamano ya kijamii na mahusiano pamoja na Mwenyezi Mungu. Ni katika muktadha huu wa kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano sehemu mbalimbali za dunia, Waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni, akizungumza na Baba Mtakatifu Leo XIV amemhakikishia kwamba, Serikali ya Italia itaendelea kuunga mkono juhudi za Vatican katika kutafuta na kudumisha amani sehemu mbalimbali za dunia.

Papa Leo XIV akisalimiana na watu wa Mungu baada ya kuchaguliwa
Papa Leo XIV akisalimiana na watu wa Mungu baada ya kuchaguliwa   (AFP or licensors)

Waziri mkuu wa Italia Meloni, ametumia fursa hii, kumpongeza Baba Mtakatifu Leo XIV kwa kuchaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki na kwamba, kuna uhusiano wa pekee kati ya Italia na Khalifa wa Mtakatifu Petro. Serikali ya Italia inapenda kuunga mkono juhudi za Vatican katika kutafuta, kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano sehemu mbalimbali za dunia. Italia itaendeleza juhudi zake za kusaidia kusitisha vita kwa kuwekeza zaidi kwenye mchakato wa majadiliano katika ukweli na uwazi. Italia itaendelea kushirikiana na Vatican katika mchakato wa maendeleo fungamani ya binadamu yanayosimikwa katika kanuni maadili na utu wema. Sayansi ya matumizi ya teknolojia ya akili unde ni changamoto kubwa katika ulimwengu mamboleo. Italia katika Kipindi chake cha uongozi wa Kundi la Nchi Saba zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani, G7 imetoa kipaumbele cha pekee kwa: utu, heshima na haki msingi za binadamu na fursa za ajira mambo msingi ambayo Baba Mtakatifu Leo XIV aliyafanyia rejea wakati wa mkutano wake wa kwanza na Baraza la Makardinali, tarehe 10 Mei 2025.

Italia na Vatican
16 Mei 2025, 14:53