Mei 18 Papa atapewa ishara 2 za utume wa Kipapa:Pete na Pallium!
Na Angella Rwezaula ā Vatican.
Kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu litakalofanyika tarehe 18 Mei 2025 saa 4.00,asubuhi masaa ya Ulaya katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na katika uwanja ulio mbele yake, Papa Leo XIV, Askofu wa Roma, ataaanza rasmi Huduma yake ya Mfuasi wa kiti na, akiwa mrithi wa mtume Petro na hivyo kuwa Mchungaji wa Kanisa Katoliki. Ibada hii, kama inavyofafanuliwa na Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa, inajumuisha nyakati kadhaa za thamani kubwa ya ishara ambapo alama ya kiaskofu ya "Petro" ya kale inajitokeza ambayo ni: Pallium na Pete ya Mvuvi.
Pallium
Pallium ni vazi la kiliturujia lililotengenezwa kwa pamba ya kondoo. Hii inamkumbusha Mchungaji Mwema, ambaye huwaweka kondoo waliopotea mabegani mwake, na itikio la Petro mara tatu kwa ombi la Yesu aliyefufuka la kulisha wana kondoo wake na kondoo wake. Kama vile Simeoni wa Thesalonike anavyoandika katika De sacris ordinationibus kuwa, "inaashiria Mwokozi ambaye, akikutana nasi kama kondoo waliopotea, anawabeba mabegani mwake, na kuchukua asili yetu ya kibinadamu katika Umwilisho, ameigawa, kwa kifo chake msalabani ametupatia Baba na kwa ufufuko ametuinua." Hi ni kitambaa chembamba ambacho kinakaa juu ya mabega, juu ya chasuble, vazi la liturujia. Kina mbavu mbili nyeusi zinazoning'inia mbele na nyuma, imepambwa kwa misalaba sita ya hariri nyeusi - moja juu ya kila kichwa kinachoshuka hadi kifuani na nyuma na nne kwenye pete inayokaa juu ya mabega - na imepambwa, mbele na nyuma, na pini tatu (acicula) zinazowakilisha misumari mitatu ya msalaba wa Kristo.
Pete ya Mvuvi
Pete ya Mvuvi ina thamani maalum ya pete ya muhuri ambayo inathibitisha imani kwa kiasi kikubwa, kazi iliyokabidhiwa kwa Petro kuthibitisha ndugu zake. Inaitwa pete ya āMvuviā kwa sababu Petro ndiye Mtume ambaye, akiwa na imani katika neno la Yesu, alivuta nyavu za kuvua samaki kimuujiza kutoka kwenye mtumbwi hadi nchi kavu.
Katika kaburi la Mtakatifu Petro
Liturujia itaanzia ndani ya Kanisa Kuu la Vatican, ambapo Papa mpya wa Roma atashuka, pamoja na Mapatriaki wa Makanisa ya Mashariki, kwenye Kaburi la Mtakatifu Petro, na kutulia katika sala na kisha wanamfukizia ubani. Kipinidi hiki knataka kusisitiza uhusiano wa karibu wa Askofu wa Roma na Mtume Petro na kwa kifo chake cha kishahidi, mahali pale pale ambapo Mfuasi wa kwanza wa Kristo alikiri imani yake kwa damu yake, pamoja na Wakristo wengine wengi waliotoa ushuhuda huo pamoja naye. Kisha mashemasi wawili huchukua Pallium, Pete ya Mvuvi na Kitabu cha Injili na kuanza maandamano kuelekea Madhabahu ya maadhimisho, kwenye jukwa la mbele, kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro.
Katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Vatican
Papa Leo XIV atapanda na kujiunga na maandamano, huku wimbo wa sifa (Laudes Regiæ) wa litania ukiimbwa, kuomba maombezi ya Mapapa watakatifu, mashahidi, na watakatifu wa Kanisa la Roma. Kutokea lango kuu la Kanisa kuu la Vatican kutaningāinia kitambaa cha samaki wa kimuujiza, ambacho kinaelezea mazungumzo kati ya Yesu na Petro, ambapo ni mrejesho wa uwazi katika liturujia la Neno na maandiko ya maadhimisho hayo. Hii ni nakala ya mchoro uliyoundwa kwa ajili ya Kikanisa cha Sistine, juu ya kitambaa cha Raffaello Sanzio na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Vatican. Katika Madhabahu, badala yake, kutawekwa sanamu ya Mama wa Shauri jema kutoka Madhabahu ya Maria huko Genazzano. Ibada ya kubariki na kunyunyiza maji takatifu itafuata, kama ya Dominika ya Pasaka. Baadaye Gloria inaimbwa, ikifuatiwa na sala, kwa kurejea mpango wa Baba wa kujenga Kanisa lake juu ya Petro.
Liturujia ya Neno
Liturujia ya Neno Itaanza ambapo Somo la Kwanza, litasomwa kwa lugha ya Kihispania, ambacho ni kifungu kutoka Matendo ya Mitume (Mdo 4:8-12) ambamo Petro anatangaza kwamba Kristo ni "jiwe lililokataliwa na waashi" na kuandikwa kwa Kiitaliano, Kiitikio ni Zaburi ya (Zab 117/118) inafafanua mada ya "jiwe" kwamba: "Jiwe lililokataliwa na waashi limekuwa jiwe kuu la msingi", wakati huo Somo la Pili, litasomwa kwa lugha ya Kiingereza, lililochukuliwa kutoka katika Waraka wa Kwanza wa Petro (1 Pt 5: 1-5. 10-11). Somo hili linaakisi uhusiano uliopo kati ya Petro, Kanisa la Roma na huduma ya Mrithi wake. Injili, ni kutoka kwa Yohane itakayosomwa kwa Kilatini na Kigiriki (Yh 21:15-19 ), ambayo inahusu ombi la Yesu mara tatu kwa Petro kulisha "wana kondoo wake" na "kondoo wake", na ni moja ya maandiko ambayo kwa kawaida yalipata kazi maalum na ya kibinafsi aliyopewa Petro katika kundi la mitume kumi na wawili.
Kupewa kwa Nembo ya Kiaskofu ya Petro
Baada ya kusomwa kwa Injili, makardinali watatu wa daraja tatu (mashemasi, kikuhani na maaskofu) na kutoka mabara tofauti watakaribia Papa Leo XIV: wa kwanza atamvalisha Pallium juu yake, wa pili ataomba, kwa sala maalum, kwa uwepo na msaada wa Bwana juu ya Papa; na tatu pia atasali sala, ikimwomba Kristo, "mchungaji na askofu wa roho zetu", aliyejenga Kanisa juu ya mwamba wa Petro, na ambaye alitambuliwa na Petro mwenyewe kuwa "Mwana wa Mungu aliye hai", ili aweze kumpatia Papa mpya Pete ya Muhuri wa Mvuvi, na kisha kumpatia Pete ya Mvuvi. Wakati huo unamalizika kwa kusali sala ya Roho Mtakatifu ili amtajirishe Papa mpya kwa nguvu na upole katika kuwahifadhi wanafunzi wa Kristo katika umoja wa ushirika, kisha Papa atabariki waamini wote kwa Kitabu cha Injili, huku akitangaza kwa Kigiriki: "Ad multos annos!"
Ibada ya utii
Baada ya ibada ya kiishara ya "utii" ya Papa kwa wawakilishi kumi na wawili wa makundi yote ya watu wa Mungu, wanaotoka sehemu mbalimbali za dunia, maadhimisho yataendelea na mahubiri ya Papa. Kisha wimbo wa Nasadiki utaimbwa ikifuatiwa na sala ya waamini yenye maombi matano, katika lugha ya Kireno, Kifaransa, Kiarabu, Kipoland na Kichina. Sala hizo zitaombwa kwa ajili ya Kanisa, lililoenea duniani kote, kwa ajili ya Papa wa Roma, anayeanza huduma yake, kwa wale wanaoshikilia majukumu ya serikali, kwa wale wanaojikuta katika mateso na shida, kwa ajili ya mkusanyiko wenyewe wa siku hiyo.
Liturujia ya Ekaristi
Wakati huo wimbo wa matoleo utaimbwa wa "Tu es pastor ovium"(wewe ni mchungaji wa zizi lako). maombi juu ya matoleo ya mkate na divai nayasihi kwamba kupitia huduma ya umisionari ya Kanisa matunda ya ukombozi yaweze kuenea kwa ulimwengu wote. Papa Leo XIV atasali "Sala ya Ekaristi " au "Kanoni ya Kirumi" na baadaye ibada ya kumunio itafanyika mwishoni Papa atamwomba Mungu alithibitishe Kanisa katika umoja na mapendo na yeye mwenyewe kuokolewa na kulindwa pamoja na kundi ambalo limekabidhiwa kwake.
Ibada za kuhitimisha
Kabla ya kuhitimisha maadhimisho hayo, Papa atatoa hotuba fupi na baada ya uimbaji wa Sala ya Malkia wa Mbingu(Regina Caeli) atatoa baraka kuu ambayo inarudi kwenye sura ya kibiblia ya mzabibu na shamba la mizabibu, inayotumika kwa Kanisa, likiomba kwamba "Bwana alinde na kutunza mzabibu alioupanda," na kuomba uso wake wa wokovu.