MAP

Mara baada ya Misa Takatifu, Baba Mtakatifu kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu, aliwashukuru watu wote wa Mungu waliohudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu anapouanza utume wake rasmi kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Mara baada ya Misa Takatifu, Baba Mtakatifu kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu, aliwashukuru watu wote wa Mungu waliohudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu anapouanza utume wake rasmi kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.  (ANSA)

Baba Mtakatifu Leo XIV Awashukuru na Kuwapongeza Watu wa Mungu

Mara baada ya Misa Takatifu, Baba Mtakatifu kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu, aliwashukuru watu wote wa Mungu waliohudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu anapouanza utume wake rasmi kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Amewashukuru wawakilishi wa Makanisa, Jumuiya za Kikristo pamoja na waamini wa dini mbalimbali waliohudhuria, bila kuwasahau viongozi wa Serikali na falme za dunia. Amemtaja Mwenyeheri Padre Camille Costa: Shuhuda wa upendo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV katika mahubiri, yake Dominika tarehe 18 Mei 2025 alipouanza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro wa 267 na Askofu wa Roma, amegusia: kifo cha Papa Francisko; Umoja na Mshikamano wa Baraza la Makardinali pamoja na sala za waamini; Ujenzi wa Kanisa linalosimikwa katika upendo wa Mungu; Kwa kukuza na kudumisha: Umoja na mshikamano wa Kanisa, chachu ya upatanisho, tayari kujikita katika mchakato wa ujenzi wa Kanisa la Kisinodi na Kimisionari. Baba Mtakatifu Leo XIV ametambua uwepo wa umati mkubwa wa watu wa Mungu kutoka sehemu mbalimbali za dunia waliofika kushuhudia anapouanza utume wake rasmi kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Papa Leo XIV akiwasalimia waamini waliofurika Uwanjani
Papa Leo XIV akiwasalimia waamini waliofurika Uwanjani   (@Vatican Media)

Kwa kifo cha Papa Francisko, waamini waligubikwa na huzuni na majonzi makubwa, wakawa kama kondoo wasio na mchungaji. Rej. Mt 9:36. Waamini wakajikita zaidi katika imani kwa Kristo Mfufuka kwa kutambua kwamba, kamwe Kristo hawezi kuwaacha kondoo wake wapotee, atawakusanya, na kuwalinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.Rej. Yer 31:10. Mara baada ya Misa Takatifu, Baba Mtakatifu kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu, aliwashukuru watu wote wa Mungu waliohudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu anapouanza utume wake rasmi kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Amewashukuru wawakilishi wa Makanisa, Jumuiya za Kikristo pamoja na waamini wa dini mbalimbali waliohudhuria, bila kuwasahau viongozi wa Serikali na falme za dunia.

Papa Leo XIV akizungumza na wawakilishi wa Makanisa na Jumuiya za Kikristo
Papa Leo XIV akizungumza na wawakilishi wa Makanisa na Jumuiya za Kikristo   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuwasalimia na kuwapongeza wanachama wa vyama mbalimbali vya kitume waliokuwa wanashiriki katika maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo, kuanzia tarehe 16 hadi 18 Mei 2025. Baba Mtakatifu amewashukuru wanachama wa vyama vya kitume kwa kuendelea kupyaisha amana na utajiri wa Ibada mbalimbali. Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, katika maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu, amehisi uwepo wa Papa Francisko, anayeendelea kulisindikiza Kanisa kwa sala na maombezi yake kutoka huko juu aliko. Amemkumbuka Mtumishi wa Mungu Padre Camille Costa de Beauregard wa Jimbo Katoliki la Chambèry, nchini Ufaransa aliyetangazwa kuwa ni Mwenyeheri kwa niaba ya Baba Mtakatifu Leo XIV na Askofu mkuu Celestino Migliore, Jumamosi tarehe 17 Mei 2025. Mwenyeheri Padre Camille Costa de Beauregard aliishi kati ya mwaka 1841 hadi mwaka 1910, shuhuda mkuu wa upendo kwa shughuli za kichungaji.

Mwenyeheri Padre Camille Costa de Beauregard
Mwenyeheri Padre Camille Costa de Beauregard

Baba Mtakatifu Leo XIV amesema, katika furaha ya imani, umoja na ushirika, Kanisa kamwe haliwezi kuwasahau watu wanaoteseka kutokana na vita. Kwa namna ya pekee watoto, familia na wazee wanaoteseka kwa kusiginwa na baa la njaa. Huko Myanmar, bado kuna kinzani na vita ambayo inaendelea kuwaathiri vijana wa kizazi kipya. Ukraine inaendelea kusubiri kwa matumaini makubwa majadiliano yanayoendelea, ili kweli amani ya kweli na ya kudumu iweze kupatikana. Baba Mtakatifu Leo XIV anapoanza rasmi maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro na Askofu wa Roma, akiwa ndani ya “mtumbwi wa Mtakatifu Petro”, anapenda kumwangalia Bikira Maria, Nyota ya Bahari na Mama wa Shauri Jema, kama alama ya matumaini. Anamwomba, Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa awaombee walimwengu, zawadi ya amani, awe ni faraja kwa wale wanaoteseka na chemchemi ya neema itakayowawezesha watu wote wa Mungu kuwa ni mashuhuda wa Kristo Mfufuka.

Papa Leo XIV Malkia wa Mbingu
19 Mei 2025, 11:40