MAP

 Askofu Felix Genn wa  Muenster. Askofu Felix Genn wa Muenster.  (Bistum Muenster)

Ask.Mstaafu Genn wa Münster,Prevost:mwenye uwezo na mnyenyekevu!

Askofu Felix Genn anakumbuka miaka mitano ya ushirikiano na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu. "Nimejua uwazi wake wa hukumu na mtazamo wa upendo wa kweli. Sasa,hata hivyo,hebu tumpe muda wa kukua katika utume wake mpya."

Na Stefanie Stahlhofen,Daniele Piccini na Angella Rwezaula – Vatican

Kusali kwa ajili yake  na tusimtwike matazamio. Hivi ndivyo Askofu Mstaafu wa Münster, Askofu  Felix Genn, ambaye alifanya kazi kwa miaka mitano na aliyekuwa Kardinali Prevost katika Baraza la Kipapa la Maaskofu anamwomba Papa Leo XIV.

Papa Leo XIV tarehe 8 Mei 2025
Papa Leo XIV tarehe 8 Mei 2025

"Prevost alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa  na sasa ghafla anajikuta katika nafasi mpya kabisa. Ninaamini kwamba mtu lazima awe na wakati wa kukua katika kazi ya aina hii," alikazia Askofu aleyeeleza kwamba katika kipindi cha ushirikiano wake na Baraza la Kipapa akiwa pamoja na naye kama mkuu maelewano mazuri ya mara moja, shukrani kwa uwazi wake wa hukumu, umahiri, unyenyekevu na kiasi na njia yenye upendo kikweli.”

Sura mbili muhimu

Picha mbili zilimvutia sana Askofu Mstaafu wa Münster. “Moja,” alieleza, “anayeoneshwa mkutano wake wakati yeye alikuwa bado hajawa  askofu, lakini akiwa Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino na alikuwa ameketi karibu na Papa Francisko. Na kisha niliona picha yake akitoa sakramenti ya Kipaimara huko Peru. Kisha nikaelewa kuwa uso wake ulizungumza juu ya ukaribu na watu, upendo kwa watu, kwa unyenyekevu mkubwa.

Papa Leo XIV alitembelea ndugu zake Waagostinian
Papa Leo XIV alitembelea ndugu zake Waagostinian

Hatabaki peke yake katika utume wake

Kuhusu jinsi Papa Leo XIV atakavyobiliana na utume wake, Askofu Genn anaweza “kufikiria tu kutokana na jinsi alivyojionesha hadharani hadi sasa. Tumeona kwamba alikwenda kwa Mama wa Shauri jema. Tunajua kwamba anaamini katika sala na udugu. Tayari ametembelea jumuiya yake ya Waagostiniani na anaamini pia ushirikiano wa makardinali na watu wote wanaomuombea. Na nadhani hii inampatia usaidizi na ujasiri wa ndani kujua kwamba hayuko peke yake.”

17 Mei 2025, 11:44