Papa Francisko na saa za mwisho za utulivu na “asante”kwa kurudi kwenye Uwanja
Na Angella Rwezaula - Vatican.
"Asante kwa kunirudisha kwenye Uwanja." Miongoni mwa maneno ya mwisho ya Papa Francisko ambayo aliyasema ni asante kwa wale ambao katika wakati huu wa ugonjwa, lakini hata muda mrefu uliopita, walimwangalia bila kuchoka, kama vile Massimiliano Strappetti, muuguzi ambaye - kama alivyowahi kusema - aliokoa maisha yake kwa kupendekeza afanyiwe upasuaji wa tumbo na ambaye Papa alimteua kuwa kama msaidizi wake wa afya tangu mnamo 2022. Kando yake kwa siku zote 38 za kulazwa katika Hospitali ya Gemelli na saa ishirini na nne kwa siku wakati wa kuendelea kupumzika kwake katika nyumba ya Mtakatifu Marta. Kwa hiyo Strappetti alikuwa na Papa Dominika ya Pasaka, tarehe 20 Aprili katika Baraka ya Urbi et Orbi. Siku moja kabla walikuwa wamekwenda kwenye Basilika ya Mtakatifu Petro ili kukagua "njia" ya kuchukua siku ambayo ingefuata wakati Papa Francisko angetokea katikati ya Kanisa Kuu kwa ajili ya Baraka.
Kukumbatia umati
Na baada ya muda huo, Dominika asubuhi, kwenye balkoni ambayo ni kitovu cha mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, wakati waamini 35,000 wa awali walikuwa tayari wameongezeka kuwa 50,000, Papa alitaka kufanya mshangao wa mwisho, muhim kwenda kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro kuzunguka kwa njia ya kigari cha Papa. Bila hofu ya awali: "Je, unafikiri ninaweza kufanya?" Aliuliza Strappetti ambaye alimtuliza. Kutoka huko kukumbatia umati na hasa kwa watoto. Huu ulikuwa mzunguko wa kwanza baada ya kutoka hospitalini Gemelli na wa mwisho wa maisha yake. Akiwa amechoka lakini akiwa na furaha, Papa Francisko alimshukuru msaidizi wake wa afya binafsi akisema: “Asante kwa kunirudisha kwenye Uwanja huo.” Maneno ambayo yanafichua hitaji la Papa wa Argentina, ambaye amefanya mawasiliano ya moja kwa moja ya kibinadamu kuwa alama ya upapa wake kwa kurejea kati ya watu kabla ya kurudi kwa Baba Mungu.
Saa za mwisho
Papa Francisko kisha alipumzika alasiri na kula chakula cha jioni kwa utulivu. Ilikuwa karibu yapata saa 11.30 alfajiri ambapo dalili za kwanza za ugonjwa zilionekana, na uingiliaji wa haraka wa wale walikuwa wanamtazama. Kwa zaidi ya saa moja baadaye, baada ya kumpungia mkono Strappetti, ambaye alikuwa amelala kitandani katika nyumba yake kwenye ghorofa ya pili ya Nyumba ya Mtakatifu Marta, Papa aliingia katika hali ya kukosa fahamu. Hakuteseka, yote yalitokea kwa haraka, alisema mtu ambaye alikuwa karibu naye katika dakika hizo za mwisho. Kifo cha busara, karibu cha ghafla, bila kungoja kwa muda mrefu na usumbufu mwingi kwa Papa ambaye amekuwa akiweka hali yake ya afya kuwa wazi sana. Kifo kilichotokea siku iliyofuata ya Pasaka, siku moja baada ya kuubariki mji wa Roma na dunia(Urb et Orbi), siku iliyofuata kwa mara nyingine tena, baada ya muda mrefu, kuwakumbatia watu. Yule ambaye, tangu wakati wa kwanza wa uchaguzi wake, mnamo tarehe 13 Machi 2013, alikuwa ameahidi safari ya kwenda pamoja.”