Mazishi ya Papa ni tarehe 26 Aprili 2025 saa 4.00 kamili katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Vatican news
Misa ya Mazishi ya Baba Mtakatifu Francisko itafanyika Jumamosi ijayo, tarehe 26 Aprili 2025, saa 4:00 kamili asubuhi, mbele ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, kama ilivyoelezwa katika ‘Ordo Exsequiarum Romani Pontificis.’ Hayo yametangazwa na Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa, tarehe 22 Aprili, huku ikiripoti kwamba ibada ya mazishi itaongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali.
Ibada ya mwisho “Ultima commendatio na la Valedictio itafanyika.†Kisha jeneza la Papa litapelekwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na kutoka hapo hadi kwenye Kanisa la Mtakatifu Maria Mkuu kwa maziko.
Viongozi kadhaa wa nchi na serikali wametangaza ushiriki wao.
Kutoa heshima kwa mwili wa Papa 23 Aprili
Siku ya Jumatano, tarehe 23 Aprili 2025 saa 3:00 asubuhi masaa ya Ulaya, jeneza lenye mwili wa marehemu Papa wa Roma Francisko litatolewa kwenye Kikanisa cha Nyumba ya Mtakatifu Marta Domus hadi kwenye Basilika ya kipapa ya Mtakatifu Petro, kama ilivyoelezwa katika kanuni ya maziko ya Papa wa Roma (Ordo Exsequiarum Romani Pontificis (nn. 41-65). Baada ya muda wa maombi, yakiongozwa na Mwadhama Kardinali Kevin Joseph Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu katoliki la Roma, msafara wa kupeleka jeneza katika Basilika utaanza
Maandamano hayo yatapitia katika uwanja wa mtakatifu Marta na uwanja wa Protomartiri Romani; kutokea kwenye Tao la Kengele hadi kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro na kuingia kwenye Kanisa kuu la Vatican kupitia mlango wa kati. Na katika Madhabahu ya maungamo, Camerlengo ataongoza Ibada ya Neno na mwisho wake maandamano ya waamini kutoa heshima kwa Papa wa Roma yataanza. Makardinali, wakiwa wamevalia mavazi yao yanayofaa watakutana katika Kikanisa cha Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, saa 2.45 asubuhi. Wote wanahusika na ibada hiyo watakuwapo.
Ratiba ya kuaga mwili wa Hayati papa Francisko
Mwishoni mwa Ibada ya kuhamisha jeneza la marehemu Baba Mtakatifu wa Roma katika Kanisa kuu la Vatican, itakayofanyika kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa, saa 3:00 asubuhi ya tarehe 23 Aprili, Kanisa kuu litaendelea kuwa wazi kwa waamini wanaotaka kuuaga mwili wa Baba Mtakatifu kwa nyakati zifuatazo.
Jumatano, Aprili 23: saa 5:00 asubuhi hadi saa- 6:00 usiku, masaa ya Ulaya
Alhamisi, Aprili 24: saa 1:00 asubuhi hadi saa saa 6:00 siku, masaa ya Ulaya
Ijumaa, Aprili 25: saa 1:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni, masaa ya Ulaya