Utangazaji wa Carlo Acutis kuwa mtakatifu umeahirishwa
Vatican News
Katika Dominika ya pili ya Pasaka, ambayo pia inajulikana kama Dominika ya Huruma ya Mungu, sherehe ya kutangazwa kuwa Mtakatifu kwa mwenyeheri Carlo Acutis iliyokuwa imeratibiwa, imeahirishwa kwa kijana huyo aliyekufa akiwa na umri wa miaka kumi na tano kwa sababu ya ugonjwa wa saratani ya damu mnamo tarehe 12 Oktoba 2006 na kutangazwa mwenyeheri huko Assisi mnamo tarehe 10 Oktoba 2020. Mwili wake umekuwa ukipumzika tangu 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Maria Mkuu ( Maria maggiore), Assisi.
Kwa njia hiyo Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican imefahamisha kwamba adhimisho la Ekaristi Takatifu na ibada ya kutangazwa kuwa mtakatifu iliyopangwa kufanyika Dominika katika maadhimisho ya Jubilei ya Vijana, imesitishwa.
Jubilei ya Barubaru
Katika taarifa ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji ilibainisha kwamba "kwa umoja na watu wote wa Mungu, Kanisa Katoliki na dunia nzima, kwa huzuni tunaungana katika sala kwa ajili ya kuondokewa na Baba Mtakatifu Francisko." Baraza la kipapa pia lilitangaza kwamba "Jubilei ya Vijana na barubaru imethibitishwa katika mpango wake wa asili. Wakati wa maombi wa "njia ya Msalaba itafanyika Aprili 25: viwanja vya "Majadiliano na jiji". Jumamosi Aprili 26, itakuwa hija za kupita Mlango Mtakatifu na Misa Takatifu, bila kutangazwa kwa Mwenyeheri Carlo Acutis, kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro mnamo Dominika Aprili 27.
Kwa sababu ya muda wa maombolezo, vile vile tamasha la muziki katika (Circo Massimo) jijini lililokuwa limepangwa kufanyika Aprili 26, saa 11 jioni limefutwa