杏MAP导航

Tafuta

Kardinali Farrell alithibitisha rasmi kifo cha Papa Francisko

Camerlengo wa Kanisa Katoliki la Roma,Kardinali Kevin Farrell akiongoza Ibada ya kuhakikisha kifo na kuwekwa mwili wa Hayati Baba Mtakatifu Francisko katika jeneza iliyofanyika Jumatatu usiku saa 2.00 kamili katika Kanisa la nyumba ya Mtakatifu Marta

Vatican News

Ilikuwa ni saa 2:00 usiku masaa ya Ulaya, Jumatatu tarehe 21 Aprili 2025 ambapo Kardinali Kevin Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu katoliki la Roma alipoongoza ibada ya kuhakikisha kifo na kuwekwa kwa mwili wa marehemu Papa Francisko katika jeneza. Tukio hilo ilifanyika katika Kanisa dogo la nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, mahali ambapo Papa Francisko alikuwa anaishi.

Wakati wa kufunga nyumba alikokuwa akiishi Mtakatifu Marta
Wakati wa kufunga nyumba alikokuwa akiishi Mtakatifu Marta   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Waliohudhuria ni pamoja na Dekano wa Makardinali, Kardinali Giovanni Battista Re, na wanafamilia wa hayati Papa Francisko, pamoja na Dk Andrea Arcangeli na Dk. Luigi Carbone, Mkurugenzi na Naibu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Afya na Usafi jijini Vatican.

Wakati wa kufunga ofisi za kitume alikokuwa akifanyia kazi
Wakati wa kufunga ofisi za kitume alikokuwa akifanyia kazi   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kufuatia ibada hiyo, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Afya na Usafi wa Jimbo la Vatican, Dk Andrea Arcangeli alithibitisha kuwa Papa alifariki dunia baada ya kuugua kiharusi, hali iliyosababisha kukosa fahamu na kuporomoka kwa mfumo wa moyo usioweza kurekebishwa.

Uhakiki wa kifo cha Papa

Kulingana na ripoti ya matibabu, ikumbukwe Papa alikuwa na historia ya kushindwa kupumua kwa papo hapo kulikosababishwa na nimonia ya pande mbili za virusi vya mkamba, shinikizo la damu,na kisukari cha Aina ya II.

 

22 Aprili 2025, 10:15