Ujumbe wa Papa kwa washiriki wa Kozi ya Toba ya Ndani:amani inazaliwa na huruma ya kweli!
Na Angela Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 27 Machi 2025 ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Kozi ya XXXV ya Toba ya Ndani, iliyoandaliwa na Idaya ya Toba ya Kitume kuanzia tarehe 24 hadi 28 Machi 2025 katika Basilika ya Mtakatifu Laurenti – Damaso, jijini Roma kwa ushiriki wa mapadre na makandidte wa Daraja Takatifu kutoka Ulimwenguni kote. Baba Mtakatifu Francisko aliwashukuru kuazia na mkuu Idara ya Toba, Afisa mkuu, mapadre, viongozi na Watumishi wa Idara ya Toba, pamoja na wahudumu wa kawaida wa Basilika za kipapa. Papa alibainisha kuwa “Kozi hii imefanyika wakati wa Kwaresima ya Mwaka Mtakatifu 2025 ambao ni wakati wa uwongofu, toba na kukubali huruma ya Mungu.”
Kuadhimisha Huruma hasa pamoja na mahujaji wa Jubilei ni fursa nzuri
Baba Mtakatifu alikazi kusema kuwa "Kuadhimisha Huruma, hasa pamoja na mahujaji wa Jubilei, ni fursa nzuri: Mungu ametufanya kuwa wahudumu wa Rehema kwa njia ya neema yake, zawadi ambayo tunaikaribisha kwa sababu tulikuwa, watu wa kwanza wa msamaha wake." Papa aliwashukuru na kuwasihi kwamba wawe watu wasala, kwa sababu mizizi ya utendaji wao wa huduma ni katika maombi, ambayo kwayo wanarefusha kazi ya Yesu, ambaye anatulia na daima anarudia kusema: “Wala mimi sikuhukumu; enenda zako wala usitende dhambi tena”(Yh 8:11).
Asante kwa huduma yenu ya lazima ya sakramenti
Baba Mtakatifu FRanciskonanwashauri hao kuwa "Neno hili la ukombozi la Bwana lisikike katika Kanisa lote katika Mwaka wa Jubilei, kwa ajili ya kufanywa upya mioyo, inayobubujika kutoka katika upatanisho na Mungu na kufungua mahusiano mapya ya kidugu. Hata amani, inayotamaniwa sana, izaliwe kutoka katika Huruma, kama tumaini lisilokatisha tamaa,” alisisitiza Papa na kwa kuhitimisha aliwashukuru akisema: “Asante kwa huduma yenu ya lazima ya sakramenti! Mama yetu awalinde katika upendo na subira ya Kristo. Niwabariki kutoka moyoni mwangu na ninawaomba tafadhali mniombee," alihitimisha.