Ujumbe wa Papa kwa wanahija wa Czech:Bwana ni mwaminifu na ahadi zake hazikatishi tamaa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Dominik Duka aliongoza Ibada ya Misa takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican ambapo mwanzoni mwa misa hiyo Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu aliongoza alisoma Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa wanahija wa Jubilei Kitaifa kutoka Jamhuri ya Czech, Jumamosi tarehe tarehe 29 Machi 2025, na ambao walipita Mlango Mtakatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko aliwarejea, ndugu maaskofu, mapadre, watawa wa kike na kiume, na waamini walei kaka na dada katika Bwana. “Nilipendelea kuwa nanyi binafsi ili kushirikishana kipindi hiki cha imani na cha umoja, lakini kwa sababu ya kuendelea kupona, ninaungana nanyi kiroho, kwa kuwashukuru kwa moyo kwa ajili ya sala zenu. Baba Mtakatifu Francisko anatoa salamu za upendo kwao, Jamhuri ya Czech (Ucheki), ambao wamefika Roma kwa ajili ya kutumiza hija ya kitaifa katika mwaka huu wa Jubilei. Amemshukuru Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Askofu Mkuu Jan Graubner, maaskofu wote waliokuwapo, mapadre, watawa kike na kiume na waamini walei.
Bwana ni mwanifu na ahadi zake hazikatishi tamaa
Papa anabainisha kuwa Safari yao ni ishara ya dhati ya shauku ya kupyaisha imani, ya kuthibitisha uhusiano na Mfuasi wa Petro, na kukiri kwa imani kukubali kwao kwa Bwana ambaye daima anatambea nasi, anatusaidia katika majaribu na kutuita kuwa mashuhuda wa amani yake na upendo wake. Yeye ni mwaminifu kwa ahadi zake, kwa sababu matumanini hayakatishi tamaa(rej. Rm 5,5; Bolla Spes non confundit). Safari yao ni ishara ya imani inayojikita katika utajiri wa kiutamaduni wa kikristo wa ardhi yao, inayoangazwa na ushuhuda wa watakatifu Adalberto, Cyril na Metodio na wengine wengi. Wao wanabeba mwanga wa Injili kwa ujasiri na subira, hata katika maeneo ambayo utafikiri haiwezekani.
Mfano wa mashuhuda unatufundisha utume wa kikristo usioonekana wazi
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe huo aidha anabainisha kwamba Mfano wao, unatufundisha kuwa utume wa kikristo hauwezi kutegemea matokeo yanayoonekana, bali juu ya imani kwa Mungu. Hata sisi tunaitwa kutangaza Injili kwa imani, bila kuogopa matatizo na vizingiti. Mtakatifu Paulo anatukumbusha: “Mimi nilipanda, Apolo akanyunyizia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu,”(1Kor 3,6).
Kwa njia hiyo shughuli yetu ni kupanda na kumwagilia kwa upendo na uvumilivu, bila kukata tamaa. Mungu anatuomba tutoe kile kidogo chetu na kile ambacho tunacho. Tufikiri mikate mitano na samaki wawili: katika mikono ya Yesu viligeuka kuwa chakula cha kutosha kwa watu wengi (Rej.Mt 14,13-21). Na ndivyo hivyo inakuwa katika jitihada zetu katika imani; ikiwa tunamwamini Bwana kwa moyo wa ukarimu, atakuwa Yeye kujaza mara mbili na kufanya kuongezeka kwa matunda kwa namna ambayo hatuwezi hata kufikiria. Kwa njia hiyo hatupaswi kupoteza kamwe imani.
Mungu anatenda hata kama hatuoni matokeo ya haraka
Kharifa wa Mtume Petro aliendelea kukazia kusema kuwa “Mungu anatenda hata kama hatuoni kwa haraka matokeo. Historia ya watakatifu wao, Papa amesema kuwa inatufundisha. Tufikiri uvumilivu wa Yohane Nepomuceno na mashuhuda wengi wa imani ya Nchi yao. Maisha yao yanatonesha kuwa, anayemtegemea Mungu hawezi kuachwa kamwe, hata wakati wa majaribu, kama yale ya kuteswa. Papa Francisko aliongeza “Tutembee pamoja, wachungaji, na watu, katika njia hii nzuri ya imani, kwa kusaidiana mmoja na mwingine na tunageuka na maisha yetu, mashuhuda wa imani na matumaini katika Ulimwengu ambao unahitaji sana, hata Ulaya. Kwa kuhitimisha Papa amebainisha kuwa “Imani yetu sio kwa ajili yetu tu, bali ni zawadi ya kushirikishana kwa furaha. Ninawakabidhi hija yenu kwa Bikira Maria, Mama wa Matumaini, ili muimairishwe katika imani, matumaini na mapendo. Ninawabariki kwa moyo ninyi nyote na watu wenu. Na ninawaomba tafadhali msali kwa ajili yangu.”
Hija ya kitaifa ya Kanisa la Czech ilianza Ijumaa tarehe 28 Machi 2025 kwa sala katika Kaburi la Mtakatifu Cyril katika Basilika ya Mtakatifu Clement ili kukumbuka mizizi ya imani ya kikristo katika ardhi hizo ambazo kwa neema ya Watakatifu Cyril na Methodius, waliweza kupata Biblia na maandishi ya kiliturujia yaliyotafsiriwa kwa lugha yao ya kislavi. Hawa ni wanahija elfu mbili. Dominika tarehe 30 Machi 2025 katika hitimisho la Hija yao saa 9.00 alasili, masaa ya Ulaya watashiriki misa Takatifu katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu Roma na ayakayeongoza misa hiyo ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Czech Askofu Mkuu Jan Graubner.