MAP

2025.02.24 Preghiere Policlinico Gemelli- Papa Francesco 2025.02.24 Preghiere Policlinico Gemelli- Papa Francesco  

Papa na siku 38 za utawala kutokea Gemelli kati ya jumbe,uteuzi na miito ya amani

Kama ilivyokuwa mwaka 2020,aliposindikiza ubinadamu wakati wa janga la Uviko-19,leo hii Papa anaendelea kuongoza Mtumbwi wa Kanisa na kuwa mahali pa kumbukumbu ulimwenguni licha ya ugonjwa na katikati ya"dhoruba"za vita,kurudisha silaha tena na umaskini.Maombi mengi ya amani yalienezwa wakati wa kukaa hospitalini Gemelli,kisha ujumbe,barua kwa Gazeti la'Corriere della Sera' na vitendo vya utawala:uteuzi zaidi ya 40 na kuanza mchakato wa Mkutano wa Kikanisa wa 2028.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Miaka mitano iliyopita, jioni ya siku ya tarehe 27 Machi 2025,Baba Mtakatifu Francisko, alikuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro peke yake wakati uwanja hyo ukiwa umejazwa na mwanga wa taa na vikisikika ving’ora. Wanadamu wote walifungiwa majumbani mwao kwa sababu ya janga la Uviko-19, lakini Papa alikuwepo, ndani ya moyo wa Ukristo, peke yake, huku akiwa anasindikizwa na mtazamo wa macho ya wote kupitia runinga za utiririshaji wa maombi ya wote. "Tumegundua kuwa tuko kwenye mtumbwi mmoja, sote ni dhaifu na tumechanganyikiwa, lakini wakati huo huo muhimu na wote tumeitwa kupiga makasia pamoja, na wote tunahitaji kufarijiana. Katika mtumbwi huu… sote tuko hapa,” Papa Francisko alisema wakati huo.” Miaka mitano baadaye, Papa amejikuta “amefungwa” nyumbani kwake, Mtakatifu  Marta, ili kuweza kupata nafuu kama alivyo ashauriwa na  madaktari baada ya nimonia ya pande  mbili ambayo ilihatarisha maisha yake mara mbili na kumlazimu kulazwa hospitalini kwa siku 38. Akiwa peke yake, lakini akisindikizwa kimwili na timu ya matibabu na washirika wake wa karibu zaidi kiroho  na ambao hata hawaamini

Tena bado ni thabiti

Hata  mnamo  tarehe 27 Machi, 2025, kama ilivyokuwa mnamo 2020 - hatua ya kumbukumbu kwa ubinadamu haijapotea. Dhoruba sio janga tena bali vita na migogoro, mbio za silaha na maisha ya watu walionyongwa na vurugu na hatari. "Kwenye mtumbwi huuu ... sote tuko hapa." Mtazamo wa ulimwengu na Kanisa,  Jorge Mario Bergoglio haachi kuongoza mtumbwi huo na hakuacha kufanya hivyo hata wakati wa wa kwaresima aliyotumia huko Gemelli, kati ya dharura ya kupumua, matibabu ya madawa na mazoezi ya viungo. Mikono kwenye usukani wa Kanisa, na macho yake  kuelekea upeo wa Ulaya, Mashariki ya Kati, Afrika na Kusini-Mashariki mwa Asia, yote yaliyosambaratishwa na vita ambavyo kutoka hapa, kutoka nafasi ya ghorofa ya kumi ya Hospitali ya Gemelli  “vilionekana kama vya kipuuzi zaidi.” Maneno yaliyoandikwa katika kutafakari kwa sala ya  Malaika wa Bwana  mnamo tarehe 2 Machi 2025 na ambayo yamebaki katika kumbukumbu ya pamoja. Tarehe 2 Machi ilikuwa ya pili kati ya tafakari sita zilizoenezwa kwa Dominika sita kuanzia  tarehe 14 Februari ambayo ilikuwa ni  siku ya kulazwa hospitalini, ambapo dirisha la kuchungulia  la kibinafsi la Jumba la kitume Vatican, lilibaki limefungwa. Katika kila tafakari yake haijawahi kuwa na ukosefu wa kurejea hali ya migogoro, kuanzia tafakari ya kwanza ya mnamo Februari 16 na kisha ile ya Dominika tarehe  23, katika mkesha wa mwaka wa tatu wa kuanza kwa uchokozi mkubwa wa Urusi dhidi ya Ukraine.

"Siku ya kumbukumbu ya uchungu na ya aibu kwa wanadamu wote," Jorge Mario Bergoglio aliita hivyo, akitualika kuwakumbuka "waathirika wa migogoro yote ya kisilaha na kuombea zawadi ya amani huko Palestina, Israel na Mashariki ya Kati yote, huko Myanmar, Kivu na Sudan." Mwaliko pia ulitolewa katika Sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 9 Machi 2025, kabla ya kuanza  Kwaresima, ambapo alionesha "wasiwasi" wake kwa kufufuliwa tena kwa ghasia nchini Syria, akitumaini  kwamba"heshima kamili kwa sehemu zote za kikabila na kidini za jamii, hasa raia zitafuatwa". Kisha tarehe 16 Machi, Dominika  ilijaa na uwepo wa watoto wa mataifa mbalimbali katika Uwanja wa Gemelli, ambao aliwaomba msaada wa maombi hasa kwa "nchi zilizojeruhiwa na vita.” Tena tarehe 23 Machi, siku ya kutoka hospitalini, Papa Francisko alishiriki uchungu wa kuanza tena kwa mashambulizi ya mabomu ya Israel huko Gaza: "Naomba silaha zinyamazishwe mara moja; na kuwa na ujasiri wa kuanza tena mazungumzo, ili mateka wote waachiliwe na usitishaji wa mwisho wa mapigano ufikiwe", aliandika, akilaani hali ya kibinadamu "kwa mara nyingine tena mbaya sana" katika Ukanda ambayo "inahitaji kujitolea kwa haraka kwa pande zinazopigana na jumuiya ya kimataifa".

Maneno ya kijihami, akili, dunia

Na siyo tu katika sala ya maombi, bali kati ya maneno ya amani yaliyosambazwa kutoka Gemelli bado kuna maneno ya  kushangaza yaliyotomwa kwa Mkurugenzi wa Gazeti la Corriere della Sera, Luciano Fontana, katika barua ya  kujibu ujumbe wa matashi mema aliytomiwa kwa ajili ya kupona haraka. Barua hiyo ilichapishwa kwa usahihi katika siku za tangazo lenye utata la mpango wa "ReArm Europe" yaani “kujihami kwa Ulaya”na Papa alihimiza upokonye silaha, akianza na maneno ambayo yanasomeka kuwa “kamwe si maneno tu: ni ukweli unaojenga mazingira ya mwanadamu. Maneno yanaweza kuunganisha au kugawanya, kutumikia ukweli au kuutumia." "Lazima tupokonye silaha ya  maneno, kunyang'anya silaha za akili na kupokonya Dunia", ndiyo ulikuwa wito wa Papa, "wakati vita haifanyi chochote isipokuwa kuharibu jamii na mazingira, bila kutoa suluhisho kwa mizozo, diplomasia na mashirika ya kimataifa yanahitaji maisha mapya na uaminifu".

Zaidi ya teuzi 40 pamoja na barua ya mkono wake

Katika sahihi yake ya kitaliki ndogo, Papa  Francisko alihitimisha barua katika gazeti la Italia. Papa mwenyewe aliweka sawa chini ya nyaraka, zilizosainiwa wakati wa siku za kulazwa hospitalini. Kwa teuzi  44 zilifanyika wakati wa majuma sita akiwa  Gemelli, kuanzia na  maaskofu, maaskofu wakuu, Mabalozi kama vile: (Burkina Faso, Chile, Belarus) na pia Gavana wa mji wa  Vatican Sr  Raffaella Petrini, na Machi 15, siku moja baada ya kulazwa hospitalini. Siku kumi baadaye, Papa aliwateua makatibu wapya wawili wa Gavana wa mji wa Vatican: Monsinyo Nappa, hadi sasa katibu msaidizi wa Baraza la Uinjilishaji, na wakili Puglisi-Alibrandi, hadi sasa makamu wa katibu mkuu. Vitendo vya utawala kama  vile Barua nyingine (Chirograph) iliyochapishwa mnamo Februari 26 ya kuanzisha Tume ya Misaada ya Makao ya Vatican (Commissio de donationibus pro Sancta Sede) ambacho ni chombo kipya cha "kuhimiza michango na kampeni maalum" kati ya waamini, Mabaraza ya Maaskofu na wafadhili wengine watarajiwa, pamoja na "kuchangisha fedha kutoka kwa wafadhili wenye mapenzi mema kwa ajili ya mipango  maalum iliyotolewa na Taasisi za Curia Romana na Tawala za mji wa Vatican.”

Kuanza kwa safari

Katika siku 38 za utawala wa Mtumbwi wa Kanisa  wakati wa dhoruba ya ugonjwa na hali ya ulimwengu, pia kuna katekesi nne zilizotayarishwa kwa siku  ya Jumatano kuanzia na ile ya tarehe (19 na 26 Februari - 5 na 19 Machi), jumbe sita (pamoja na Ujumbe wa Kwaresima au zile zilizoelekezwa kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha; kwa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto Wadogo, na kuna barua iliyotumwa kwa Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi, ili kuanzisha ratiba ya safari itakayoongoza Mkutano wa Kikanisa wa mwaka  2028 mjini  Vatican, ili kuweza kuunganisha yale ambayo yametimia hadi wakati huo, bila kuitisha Sinodi mpya. Uamuzi huo unaliweka Kanisa la Ulimwengu wote katika safari tena kwa miaka mitatu ijayo, na ambao daima unasindikizwa na Baba Mtakatifu. Kamwe kutokuwa pekee yake, hata ikiwa ametengwa; kamwe kuwa dhaifu, hata wakati akiwa katika kupona taratibu; kamwe kutokuwepo,  hata kama yuko mbali kimwini na waamini kwa sababu ya janga la ulimwengu au ugonjwa wa kibinafsi.

Siku 38 za Papa Hospitalini akiendelea kuongoza mtumbwi
27 Machi 2025, 17:03