Papa Hospitalini Gemelli,vigezo na vipimo vya damu ni imara.Tiba inaendelea
Vatican News
“Hali za kimatibabu za Baba Mtakatifu zimebaki kuwa shwari zikilinganishwa na siku zilizopita. Leo pia hajawasilisha matukio ya kushindwa kupumua.
Baba Mtakatifu aliendelea na mazoezi ya kupumua na ya mwili yenye faida. Vigezo vyote vya mzunguko wa damu na vipimo vya damu vilibakia imara.
Hakuwa na homa. Madaktari bado wanadumisha utabiri uliohifadhiwa. Kwa kuzingatia uthabiti wa hali halisi ya kliniki, taarifa itakayofuata ya matibabu itatolewa Jumamosi.
Baba Mtakatifu leo hii alijikita na baadhi ya shughuli ndogo ndogo wakati wa asubuhi na mchana, alipumzika na kusali. Kabla ya chakula cha mchana alipokea Ekaristi.”
Ndiyo taarifa iliyotolewa jioni ya leo hii Alhamisi tarehe 6 Machi 2025, utoka Ukumbi wa Vyombo vya habari Vatican, kuhusiana na afya ya Baba Mtakatifu aliyelazwa tangu tarehe 14 Februari 2025, katika Hospitali ya Gemelli Roma.