Papa hospitalini Gemelli,upokeaji wa hewa ya mitambo ulisitishwa na afya inaboreka
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa kutoka Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican iliyotolewa jioni ya leo hii, Jumanne tarehe 19 Machi 2025, kuhusu hali ya afya ya Papa Francisko aliyelazwa hospitalini tangu tarehe 14 Februari katika Hospitali ya Gemelli, Roma inabainisha kuwa: “Hali ya kimatibabu ya Baba Mtakatifu imethibitishwa kuwa inaboreka. Baba Mtakatifu amesitisha utumiaji wa hewa ya mitambo usio na uvamizi na pia kupunguza hitaji la matibabu ya oksijeni ya mtiririko wa juu. Maendeleo katika mazoezi ya viungo(physiotherapy) na kupumua yanaendelea. Leo asubuhi(Machi 19, katika Maadhimisho ya Mtakatifu Yosefu, Baba Mtakatifu aliadhimisha Misa Takatifu.â€
Kulingana na madaktari, maambukizi ya mapafu yanadhibitiwa, ingawa hayajaondolewa. Maadili ya uchambuzi wa kliniki ni ya kawaida. Papa anaendelea kutokuwa na homa. Siku ya Papa ilitumika kati ya matibabu, maombi na kazi kidogo. Bado hakuna uamuzi uliotolewa kuhusu ibada za Juma Kuu Takatifu. Kwa kuzingatia hali thabiti ya Papa, taarifa ya matibabu ijayo haitarajiwi kabla ya Juma lijalo. Ofisi ya Vyombo vya habari, Vatican itarejea kutoa taarifa za jumla kwa wanahabari keshokutwa Ijumaa na Jumatatu ijayo.