杏MAP导航

Tafuta

Papa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Gemelli,Roma. Papa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Gemelli,Roma. 

Papa hospitalini Gemelli,upokeaji wa hewa ya mitambo ulisitishwa na afya inaboreka

Kupunguzwa kwa hitaji la oksijeni ya mtiririko wa juu;maendeleo kutokana na mazoezi ya viungo pia kupumua.Asubuhi tarehe 19 Machi Papa Francisko aliadhimisha Misa kwa ajili ya maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Yosefu.Kulingana na madaktari,maambukizi ya mapafu yanadhibitiwa.Maadili ya uchambuzi ni ya kawaida.Na hakuna uamuzi juu ya ibada za Juma kuu Takatifu.

Vatican News

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa kutoka  Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican  iliyotolewa jioni ya leo hii, Jumanne tarehe 19 Machi 2025, kuhusu hali ya afya ya Papa Francisko aliyelazwa hospitalini tangu tarehe 14 Februari katika Hospitali ya  Gemelli, Roma inabainisha kuwa: “Hali ya kimatibabu ya Baba Mtakatifu imethibitishwa kuwa inaboreka. Baba Mtakatifu amesitisha utumiaji wa hewa ya mitambo usio na uvamizi na pia kupunguza hitaji la matibabu ya oksijeni ya mtiririko wa juu. Maendeleo katika mazoezi ya viungo(physiotherapy) na kupumua yanaendelea. Leo asubuhi(Machi 19, katika Maadhimisho ya Mtakatifu Yosefu, Baba Mtakatifu aliadhimisha Misa Takatifu.”

Kulingana na madaktari, maambukizi ya mapafu yanadhibitiwa, ingawa hayajaondolewa. Maadili ya uchambuzi wa kliniki ni ya kawaida. Papa anaendelea kutokuwa na homa. Siku ya Papa ilitumika kati ya matibabu, maombi na kazi kidogo. Bado hakuna uamuzi uliotolewa kuhusu ibada za Juma Kuu Takatifu. Kwa kuzingatia hali thabiti ya Papa, taarifa ya matibabu ijayo haitarajiwi kabla ya Juma lijalo. Ofisi ya Vyombo vya habari,  Vatican  itarejea kutoa taarifa za jumla kwa wanahabari keshokutwa Ijumaa na Jumatatu ijayo.

Afya ya Papa inaboraka siku hadi siku
19 Machi 2025, 20:00