ÐÓMAPµ¼º½

Papa anaendelea na matibabu Roma. Papa anaendelea na matibabu Roma.  (ANSA)

Papa Hospitalini Gemelli,matukio mawili ya kushindwa kupumua papo kwa hapo

Matukio mawili yaliyojitokeza leo hii yalisababishwa na mkusanyiko wa kamasi,ambazo zilitolewa.Ameendelea kupokeaji hewa ya mitambo isiyovamia tena.Papa Francisko daima alibaki kuwa macho na mwelekeo mzuri.

Vatican News

"Leo, Baba Mtakatifu aliwasilisha matukio mawili ya kushindwa kupumua kwa papo hapo, kulikosababishwa na mkusanyiko mkubwa wa kamasi kwenye(endobronchial)kikoromeo na matokeo ya (bronchospasm)kukosa kupumua kwa papo hapo.

Kwa hiyo kilitumika kifaa cha uchunguzi kiitwacho(Bronchoscopy)cha aina mbili na kutoa kamasi kwa wingi. Wakati wa mchana, alipewa tena hewa ya mitambo isiyo na uvamizi.

Baba Mtakatifu ameendelea kuwa macho daima, mwenye mwelekeo na ushirikiano. Utabiri unabaki kuhifadhiwa."

Haya ndiyo yaliyoripotiwa katika taarifa kutoka Ofisi ya vyombo vya habari vya Vatican jioni hii, Jumatatu tarehe 3 Machi 2025, kuhusu hali ya afya ya Papa, aliyelazwa hospitalini tangu 14 Februari  2025 katika Hospitali ya Gemelli.

Sasisho hili ni saa 1.30 za jioni masaa ya Ulaya, Jumatatu tarehe 3 Machi 2025.

03 Machi 2025, 19:30