ÐÓMAPµ¼º½

Papa Francisko anaendelea na matibabu,Hospitalini Gemelli. Papa Francisko anaendelea na matibabu,Hospitalini Gemelli.  (AFP or licensors)

Papa huko Gemelli,hali ni thabiti.Alipakwa majivu na kupiga simu huko Gaza

Hapakutokea hali yoyote mpya ngumu,oksijeni ya mtiririko wa juu iliendelea wakati wa mchana na hewa wa mitambo itaendelea usiku.Alianza tena shughuli ndogo,alitumia siku nzima amekaa kwenye sofa.Aliongeza mazoezi ya kupumua na tiba ya viungo.Hizi ni taarifa zilizosasishwa jioni hii Jumatano Machi 5 na Ofisi ya Vyombo vya Habari,Vatican.

Vatican News

"Baba Mtakatifu pia alibaki thabiti leo hii bila kuwasilisha matukio ya kushindwa kupumua. Kama ilivyopangwa, wakati wa mchana, alipata matibabu ya oksijeni ya mtiririko wa juu na wakati huo huo  upokeaji wa hewa ya mitambo usio na uvamizi utarejeshwa wakati wa usiku.

Baba Mtakatifu ameongeza mazoezi ya kupumua na mazoezi hai ya viungo. Alitumia siku nzima akiwa katika kiti cha sofa. Kwa kuzingatia ugumu wa hali nzima ya kliniki, utabiri unabaki kuhifadhiwa.

Asubuhi ya leo katika nyumba ya kibinafsi kwenye  ghorofa ya 10, Baba Mtakatifu alishiriki katika ibada ya baraka ya Majivu Matakatifu ambapo alipakwa majivu juu ya kichwa chake na mshereheshaji, kisha akapokea Ekaristi.

Baadaye alijitolea kwa shughuli fulani ndogo ndogo. Pia asubuhi alimpigia simu Padre Gabriel Romanelli, Paroko wa Familia Takatifu ya Gaza. Alasiri alibadilishana kazi kwa kupumzika."

Haya ndiyo yaliyoripotiwa katika taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican iliyotolewa jioni hii, Jumatano tarehe 5 Machi 2025, kuhusu afya ya Papa, ambaye amelazwa hospitalini tangu 14 Februari 2025 huko Gemelli Roma.

 

Sasisho jipya la habari hii ni saa 1.30 jioni,  siku ya Jumatano 5 Machi 2025 masaa ya Ulaya.

05 Machi 2025, 19:30