Papa alilala usiku mzima na ameanza tena kupewa Okisjeni bila barakoa
Vatican News
“Papa alilala usiku mzima na sasa anaendelea na mapumziko.” Ndiyo taarifa kutoka Ukumbi wa Vyombo vya Habari, Vatican iliyosasishwa asubuhi Jumanne tarehe 4 Machi 2025.
Baadaye pia taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Vyombo vya habari iliripoti kwamba "Papa anaendelea na matibabu yake na mazoezi ya kupumua. Alianza tena uingizaji hewa ya mtiririko wa juu (kwa hivyo usio wa hewa ya mitambo) kwa kutumia oksijeni za puani. Aidha asubuhi alijikita na mapumziko na sala. Hali kwa sasa inaonekana kuwa tulivu katika mfumo tete."
Kama inavyojulikana Papa Francisko anasindikizwa na Wafanyakazi wa Afya wa Mji wa Vatican na Kikundi cha Madaktari wa Hospitali ya Gemelli.
Katika taarifa kutoka Ofisi ya vyombo vya habari vya Vatican jioni ya Jumatatu tarehe 3 Machi 2025, kuhusu hali ya afya ya Papa, aliyelazwa hospitalini tangu 14 Februari 2025 katika Hospitali ya Gemelli, Roma ilibanisha kuwa: "Leo, Baba Mtakatifu aliwasilisha matukio mawili ya kushindwa kupumua kwa papo hapo, kulikosababishwa na mkusanyiko mkubwa wa kamasi kwenye(endobronchial)kikoromeo na matokeo ya (bronchospasm)kukosa kupumua kwa papo hapo. Kwa hiyo kilitumika kifaa cha uchunguzi kiitwacho(Bronchoscopy)cha aina mbili na kutoa kamasi kwa wingi. Wakati wa mchana, alipewa tena hewa ya mitambo isiyo na uvamizi. Baba Mtakatifu ameendelea kuwa macho daima, mwenye mwelekeo na ushirikiano. Utabiri unabaki kuhifadhiwa.
Ikumbukwe Papa Francisko alilazwa Hospitalini Gemelli, Roma tangu tarehe 14 Februari akiwa na ugonjwa wa Mkamba(Bronchitis) na baada ya katika vipimo vya kina ilionekana kuwa na Nimonia ya pande zote mbili.
Jioni ya leo hii tarehe 4 Machi 2025, ikiwa ni siku ya tisa ya kusali Rozari kwa ajili ya afya ya Baba Mtakatifu, Sala itakayofanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 3.00 usiku masaa ya Ulaya na saa 5.00 masaa ya Afrika Mashariki na Kati, itaongozwa na Kardinali Arthur Roche, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa.
Habari hii imesasishwa saa 9.00 alasili masaa ya Ulaya, saa 11.00 masaa ya Afrika Mashariki na Kati.