Carmela,“mwanamke wa maua ya njano”kila siku huko Gemelli kwa Papa,leo ameniona!
Na Salvatore Cernuzio – Roma
Shada lile la maua ya manjano alilokuwa amempelekea Papa, kama alivyofanya mara nyingine kumi wakati wa siku hizi 38 za kulazwa hospitalini, lililazimika kuchukuliwa na polisi kwa sababu Carmela karibu alipoteze kutoka mikononi mwake. Kikubwa sana kilikuwa hisia ya kujisikia anatazamwa na macho ya Papa Francisko: “juu yangu kutoka kwenye balcony ya Gemelli, katika kuonekana kwake kwa mara ya kwanza tangu kulazwa hospitali, na kumsikiliza wakati ilipowekwa sauti yake,” alisema mwanamke huyo. Sauti ya Papa ilikuwa “Ninaona mwanamke hapo na maua ya njano. Ni mwema!”
Bi Carmela alisema: "Sijui la kusema. Asante, asante, asante. Asante kwa Bwana na Baba Mtakatifu. Sikufikiri 'nimeonekana' hivyo." Mwanamke huyo Carmela Mancuso, mwenye umri wa miaka 78, kutoka Calabria lakini akiishi Roma kwa miaka sita, aliweza kuzungumza na mwandishi akiwa anaonekana hata kuelemewa na machozi. Sauti ilitetemeka kama ile ya mtu ambaye amepata wakati mgumu. Ni mbali sana kuliko matarajio, mbali sana na haiwezi kufikiwa. "Baba Mtakatifu alitakiwa kutoa baraka na badala yake aliona shada langu la waridi. Natamani apone haraka na arudi kwetu kama zamani."
Maua ni kama "tiba"
Inawezekana kwamba Papa ambaye kisha alipeleka shada la maua kwa Bikira Maria Mkuu Chini ya miguu ya Picha ya Salus Populi Romani (yaani Afya ya watu wa Roma) alikuwa tayari amemwona bibi huyo mfupi, mwenye tabia za upole na nywele za kijivu zilizopigwa na upepo, siku za nyuma, katika mojawapo ya washiriki wengi wa katekesi ya kila Jumatano na watu wengine ambao walipeleka maua. Bi Carmela akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican alisema: “Kwangu mimi maua ni tiba” ambayo ukipenda, yanayoendana na maombi, anayomwomba Mungu kwa ajili ya wagonjwa wote, zaidi kwa ajili ya Papa. Tangu Papa Francisko alazwe hospitalini kwa nimonia ya pande mbili, Bi Carmela ameondoka nyumbani kwake katika eneo la Monteverde "angalau mara 10-12" ili kwa kuchukua treni hadi kituo cha Gemelli. “Nilikuwa na furaha hii ya kuleta maua kwa Baba Mtakatifu."
Shada la kwanza kwa Mtoto wa Hospitali ya Bambino Gesù
Mara ya kwanza Bi Carmela alitumia maua kama sala, ujumbe na, kiukweli, matibabu, alikuwa katika hospitali, hospitali ya watoto ya Kipapa ua Bambino Gesù. "Nilikuwa nikienda huko mara kwa mara na kulikuwa na mtoto wa kike wa miezi 3 ambaye alilazimika kufanyiwa upasuaji mdogo. Nilimfahamu shangazi yangu katika safari ya kwenda katika Huruma ya Mungu (mahali patakatifu hatua chache kutoka Mtakatifu Petro), tulikuwa pamoja na siku moja aliniambia: 'Lazima niende Hospitali ya Bambino Gesù sasa, mpwa wangu yupo na anapaswa kufanyiwa upasuaji'. Alikuwa na wasiwasi wote. ‘Sijui la kufanya,’ akaniambia. Nikamjibu ‘nitakupeleka’ na hivyo nikaongozana naye, nikaenda mpaka juu na upasuaji ukafanyika. Kwa bahati nzuri, ilikuwa ya mafanikio! Kwa hivyo wazo la kwanza lilikuwa kupeleka maua. Kuanzia hapo kila mara nilianza kuleta maua kama ishara ya shukrani, kiukweli kila nikileta maua naweka kadi ndogo yenye ujumbe mwingi na ninaomba baraka kwa jamaa zangu, kwa marafiki zangu.” Na kwa mwezi mmoja sasa pia kwa ajili ya Papa.”
Salamu kutokea balcony ya Gemelli
"Lakini ni hisia iliyoje ...", alitoa maoni mwanamke huyo, akikatiza historia yake kukumbuka zile za sekunde fupi alizotumia akiwa huko Gemelli. "Nilikuwa nikipunga mkono hivi ... nilifanya kwa wazo hili: Ninazipungia kama nilivyofanya mara nyingi kwenye Katekesi yake, Papa, kila aliponiona pale alifanya ishara (akifungua mikono yake). Nina picha nyingi. Leo nilitokea kuwa mstari wa mbele na kuwaza, ‘Acha tuone ikiwa hili bado linafanya kazi.’ Aliniona, siamini.” "Tumuombee" Carmela Mancuso alisema hakuwahi kuhofia maisha ya Papa Francisko: "Hapana, hapana, siku zote. Siku zote nilikuwa na imani hii kubwa nilipokuja hapa." Sasa Papa ameondoka na kurudi SMtakatifu anta Marta, lakini kupona kwake kutakuwa kwa muda mrefu. Kwa hiyo, bibi huyo alisisitiza, hatupaswi kuacha kusali: “Tumtie moyo, tufuatane naye, atafanikiwa. Atakuwa kama msichana mdogo wa Mtoto Yesu aliyeponywa. Yeye pia, hakika."