Waziri Mkuu wa Italia Bi Giorgia Meloni,atembelea Papa Hospitalini Gemelli
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jumba la Waziri Mkuu wa Italia, inabainisha kuwa Bi Giorgia Meloni alikwenda Hospitali ya Gemelli kumtembelea Baba Mtakatifu.Bi Meloni alieleza kwa Papa matashi mema ya kupona kwa niaba ya Serikali na Taifa zima.“Nimefurahi sana kumkuta akiwa macho na msikivu,”alisema Waziri Mkuu wa Italia Bi Meloni.“Tulitaniana kama kawaida.Hajapoteza msemo wake wa ucheshi.”
19 Februari 2025, 16:22