Usiku mtulivu kwa Papa huko Hospitali ya Gemelli
Vatican News
"Usiku ulipita kwa amani, Papa alipumzika." Ofisi ya Vyombo vya Habari iliripoti subuhi ya leo, tarehe 23 Februari 2025. Jana tarehe 22 Februari, Papa alikuwa na shida ya kupumua na ilikuwa muhimu kuongezewa damu."
Inasemekana Papa Francisko alitumia oksijeni kupumulia asubuhi hii pia wakati wa uchunguzi. Na vipimo vya chunguzi zaidi wa kliniki vinaendelea. Tutasubiri taarifa ya jioni hii ili kujua matokeo zaidi.
Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican jana jioni, tarehe 22 Februari 2025, ilitoa sasisho lifuatalo: "Hali ya Baba Mtakatifu inaendelea kuwa tete, kwa hivyo, kama ilivyoelezewa jana, Papa hayuko nje ya hatari. Asubuhi ya leo Papa Francisko aliwasilisha tatizo la muda mrefu la ugonjwa wa pumu, ambao pia alihitaji kuwekewe oksijeni.”
Taarifa hiyo aidha ilibainisha kuwa: Vipimo vya damu vya leo pia vilionesha anemia, inayohusishwa na upungufu wa damu, ambayo alitakiwa kungezewa damu.” Baba Mtakatifu anaendelea kuwa macho na alitumia siku nzima akiwa amekaa katika kiti cha sofa hata kama alikuwa na maumivu zaidi kuliko jana. Kwa sasa ubashiri umehifadhiwa."