ĐÓMAPµĽş˝

Katekesi ya Jumatano hii haikufanyika katika Ukumbi wa Paulo VI kwa sababu Papa bado amelazwa Hospitalini. Katekesi ya Jumatano hii haikufanyika katika Ukumbi wa Paulo VI kwa sababu Papa bado amelazwa Hospitalini.  (Vatican Media)

Papa:tuwaige Simeoni na Anna,mahujaji wa matumaini wanafufua mioyo ya kaka na dada!

Katekesi ya Papa aliyopaswa kufanya katika Ukumbi wa Paulo VI na ambayo ilifutwa kutokana na kulazwa kwa muda mrefu katika hospitali ya Gemelli imechapishwa.Katika tafakari hii ni mzunguko wa Jubilei 2025.Baba Mtakatifu anafafanua Uwasilishaji wa Yesu Hekaluni na anatualika kuwa kama Simeoni na Anna,mahujaji wa tumaini wenye macho safi yenye uwezo wa kuona zaidi ya kile kinachoonekana mbele yetu.

Vatican News

Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imechapisha Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko iliyotayarishwa kwa ajili ya Katekesi yake ya Jumatano tarehe 26 Februari 2025, na ambayo haikufanyika kutokana na kulazwa kwa muda mrefu katika Hospitali ya A. Gemelli, Roma. Tafakari hii ni sehemu ya mzunguko wa Jubilei 2025: "Yesu Kristo tumaini letu. Utoto wa Yesu" na kwa kupendekeza tafakari ya kuwakilishwa kwa Yesu Hekaluni na kifungu cha: “Macho yangu yameona wokovu (Lk 2,30).   Kwa hiyo kwa kuwakilishwa kwa Yesu Hekaluni ni kifungu cha Injili kutoka Injili ya Luka kisemacho: “Basi Simeoni, akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako.”( Luka 2,27-29).

Utiifu wa Maria na Yosefu kwa Sheria ya Bwana

Wapendwa kaka na dada, habari za asubuhi! Tutafakari leo hii uzuri wa “Yesu Kristo, tumini letu” (1Tm 1,1) katika Fumbo la uwakilishi wake kwenye Hekalu. Katika simulizi ya  utoto wa Yesu, mwinjili Luka anatuonesha utiifu wa Maria na Yosefu kwa Sheria ya Bwana na maagizo yake yote. Kiukweli, katika Israeli hapakuwa na wajibu wa kumleta mtoto Hekaluni, bali  wale walioishi kwa kusikiliza Neno la Bwana na kutamani kuendana nalo, waliona kuwa ni mazoezi ya thamani. Ndivyo alivyofanya Anna, mama yake nabii Samweli, ambaye alikuwa tasa; Mungu alisikia maombi yake na, baada ya kupata mwanawe, alimpeleka hekaluni na kumtoa milele kwa Bwana (1Sam 1:24-28). Kwa hiyo Luka anasimulia tendo la kwanza la ibada ya Yesu, lililoadhimishwa katika mji mtakatifu, Yerusalemu, ambalo litakuwa lengo la huduma yake yote ya msafiri tangu wakati anapofanya uamuzi thabiti wa kwenda huko ( Luka 9:51), kuelekea utimizo wa utume wake.

Hekalu/ Kanisa ni nyumba ya sala

Maria na Yosefu hawajiwekei kikomo kwa kupandikiza Yesu katika historia ya familia, ya watu, ya muungano na Bwana Mungu. Wanamtunza kwa matunzo na ukuaji wake, na wanamwingiza kwenye mazingira ya imani na ibada. Na wao wenyewe hukua polepole - katika ufahamu wa wito unaowazidi mbali. Katika Hekalu, ambalo ni "nyumba ya sala" (Lk 19:46), Roho Mtakatifu anazungumza na moyo wa mtu mzee: Simeoni, mshiriki wa watu watakatifu wa Mungu waliotayarishwa kwa kungoja na tumaini, anayelisha hamu ya utimilifu wa ahadi za Mungu kwa Israeli kupitia manabii. Simeoni anahisi uwepo wa Mpakwa-Mafuta wa Bwana Hekaluni, anaona nuru inayoangaza kati ya watu waliozama “katika giza” ( Isa 9:1) na kwenda kukutana na mtoto huyo ambaye, kama Isaya anavyotabiri, “amezaliwa kwa ajili yetu”, ni mwana ambaye “tumepewa sisi”, “Mfalme wa Amani” (Isa 9:5).

Kukutana na Mwokozi wa Mataifa

Simeoni anamkumbatia mtoto huyo ambaye, mdogo na asiye na ulinzi, anapumzika mikononi mwake; lakini ni yeye, kiuhalisia, ndiye anayepata faraja na utimilifu wa kuwepo kwake kwa kumshika karibu.Anaidhihirisha katika wimbo uliojaa shukurani zenye kusisimua, ambao katika Kanisa umekuwa sala ya mwisho wa siku isemayo:“Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, Uliouweka tayari machoni pa watu wote; Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.” (Lk 2,29-32). Simeoni anaimba juu ya furaha ya wale ambao wameona, ya wale ambao wametambua na wanaweza kusambaza kwa wengine kukutana na Mwokozi wa Israeli na  wa Mataifa. Yeye ni shuhuda wa imani, ambayo anapokea kama zawadi na kuwasiliana na wengine; yeye ni shahidi wa tumaini lisilokatisha tamaa; ni ushuhuda wa upendo wa Mungu, unaoujaza moyo wa mwanadamu furaha na amani. Akiwa amejawa na faraja hii ya kiroho, mzee Simeoni anaona kifo si mwisho, bali ni utimilifu, kama utimilifu, anangojea kama "dada" ambaye haangamizi bali anamtambulisha maisha ya kweli ambayo tayari amekwisha kuonja na ambayo anaamini.

Simeoni na Anna ni mahujaji wa matumaini

Siku hiyo, Simeoni hakua pekee yake aliyeona wokovu ukiwa mwili ndani ya mtoto Yesu.  Kitu kimoja kinatokea kwa Anna, mwanamke katika miaka yake ya zaid ya themanini, mjane, aliyejitolea kabisa kwa huduma ya Hekalu na aliyewekwa wakfu kwa maombi. Anapomwona mtoto huyo, kiukweli, Ana anasherehekea Mungu wa Israeli, ambaye aliwakomboa watu wake katika mtoto huyo mdogo, na anawaambia wengine juu yake, akieneza neno la unabii kwa ukarimu. Wimbo wa ukombozi wa wazee wawili hivyo hutoa tangazo la Jubilei kwa watu wote na kwa ulimwengu. Katika Hekalu la Yerusalemu, matumaini yanawashwa tena mioyoni mwao kwa sababu Kristo tumaini letu ameingia humo. Ndugu wapendwa, na tuwaige Simeoni na Anna, hawa "mahujaji wa matumaini" walio na macho safi na yanayoweza kuona zaidi ya kile kinachookana; wanaojua jinsi ya "kunusa" uwepo wa Mungu katika udogo, wanaojua jinsi ya kukaribisha kwa furaha kutembelewa na Mungu na kufufua tumaini katika mioyo ya kaka na dada.

Tafakari ya Katekesi ya Papa 26 Februari 2025
26 Februari 2025, 16:23