ĞÓMAPµ¼º½

Papa atoa ujumbe kwa Tamasha la Muziki SANREMO, Italia. Papa atoa ujumbe kwa Tamasha la Muziki SANREMO, Italia. 

Papa kwa Tamasha,Sanremo:Muziki ni chombo cha amani,vita vinaharibu watoto

Baba Mtakatifu alionekana akitoa ujumbe wa video katika Ukumbi wa Ariston kwa tamasha la muziki la Italia:"Muziki unaweza kusaidia watu kuishi pamoja,alisema na akikumbuka Siku ya Watoto Duniani,alielekeza mawazo yake kwa watoto wadogo ambao wanalia na kuteseka kwa ajili ya dhuluma nyingi duniani.Papa alionesha shauku ya kuona waliochukiana wakipeana mikono,kukumbatiana na kusema kuwa maisha,muziki na wimbo:amani inawezekana!â€

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Watazamaji wengi wa  Ariston walijawa na ukimya wa mshangao mkubwa wakati, ule wa muda mfupi kabla ya saa 4 usiku tarehe 11 Februari 2025 ambapo, mwenyeji na mkurugenzi wa kisanii wa Sanremo 2025,(Tamasha la Muziki Italia), Carlo Conti, alitangaza 'uwepo,' kati ya waimbaji wanaoshindana na wageni maalum, wa mgeni ambaye hakuwahi kutokea: ‘Papa.’ Kwa njia ya video uliyorekodiwa katika nyumba yake huko Mtakatifu Marta mjini Vatican, ambayo haukuwa imejumuishwa katika programu ya tamasha hili, Baba Mtakatifu  Francisko aliungana na  watazamaji wa toleo la 75 la tukio maarufu la muziki la Italia kukumbusha umuhimu wa muziki na ujumbe unaoweza kuwasilisha. Ujumbe wa "amani", kama ule ulioimbwa mara moja baadaye na waimbaji wawili mmoja wa  Israeli Noa na mwimbaji wa Kipalestina Mira Awad, walioalikwa na kuimba kwa  lugha ya  Kiebrania, Kiarabu na Kiingereza kwa wimbo wa “Imagine†usiyosahaulika wa mwimbaji John Lennon. “Muziki ni uzuri, muziki ni chombo cha amani. Ni lugha ambayo watu wote, kwa njia tofauti, huzungumza na kufikia moyo wa kila mtu. Muziki unaweza kusaidia watu kuishi pamojaâ€

Kukumbuka Siku ya Mtoto Duniani

Kwa mujibu wa Jorge Mario Bergoglio - Papa Francisko alikumbuka kumbukumbu ya kibinafsi, ya mama yake,  Maria  Regina ambaye, alisema: "aliniambia na kunielezea baadhi ya vifungu kutoka katika kazi za sauti za muziki (Liric)  na kunifanya kuelewa hisia ya maelewano na ujumbe ambao unaweza kutoka katika muziki.†Kumbukumbu nyingine, iliyohifadhiwa "moyoni mwake", Papa basi alitaka kushiriki kwenye jukwaa la Sanremo ni la: Siku ya Watoto Duniani iliyoadhimishwa mnamo Mei 2024 kwenye Uwanja wa Kitaifa  Olimpic jijini  Roma, lililoratibuwa na Conti mwenyewe. "Ulikuwa ni wakati mzuri pamoja na kuwepo kwa maelfu ya watoto kutoka duniani kote,†Alisema Papa Francisko.

Vita huharibu watoto

Kwa kutoa umakini wa Italia na Ulimwenguni, Papa alisema: “Ni kwa watoto wangapi wengi wasioweza kuimba,  watoto wengi ambao hawawezi kuimba maishani, na kulia na kuteseka kwa dhuluma nyingi ulimwenguni, kwa vita vingi, hali ya migogoro. Vita vinaharibu watoto. Tusisahau kamwe kwamba vita siku zote ni kushindwa.â€

Shauku ya kuona waliochukiana wakipeana mikono na kukumbatiana

Kwa upande wa Baba Mtakatifu pia alielezea shauku yake kwamba “ Ninachotamani zaidi ni kuona wale ambao wamechukiana wakipeana mikono, kukumbatiana na kusema katika maisha yao, muziki na wimbo: amani inawezekana! Leo mnafanya na manaifanya ijulikane kupitia muziki," alimwambia Carlo Conti.

Kujitolea kwa ulimwengu wa haki zaidi na wa kindugu

Kwa wale wote walikuwapo Papa Francisko aliwaachia matashi mema yake kuwa “, Francesco: "Jaribuni kupata jioni njema.†Kisha aliwasalimu “wote waliounganishwa, hasa wale wanaoteseka na anaonesha matumaini kwamba muziki mzuri unaweza kufikia moyo wa kila mtu.†Muziki unaweza kufungua moyo kwa maelewano, kwa furaha ya kuwa pamoja, kwa lugha ya pamoja na uelewano, na kutufanya tujitoe kwa ulimwengu wa haki na wa kindugu zaidi.

Shukrani kutoka kwa Carlo Conti kwa Papa

Maneno ya Papa Francisko yalipokelewa kwa nderemo na makofi kutoka katika jukwaa hadi kwa hadhira, huku watazamaji wakinyanyuka. Na Carlo Conti alianzisha mshangao kwa video kwa kueleza kwamba alikuwa amemwandikia Papa kumjulisha kuhusu wakati huu wa amani, wimbo wa Noa na Mira Awad. “Yeye ni mtu aliye ndani ya mioyo yetu sote na ambaye mara nyingi hupaza sauti yake, hupiga kelele kwa ulimwengu kuitaka amani. Niliandika kama angeweza kutuma wazo lake kutambulisha wakati huu, alifanya kitu zaidi ... ", alisema mtangazaji. Alirudia mara mbili mwishoni mwa video: "asante Baba Mtakatifu."

Papa na Sanremo
12 Februari 2025, 15:05