Papa katika hospitali ya Gemelli,maambukizi ya njia ya upumuaji:anaendelea na matibabu
Vatican News
Kutokana na kuendelea kuwa na ugonjwa wa mkamba(bronchitis)katika siku za hivi karibuni, Papa Franciskp, aliyelazwa katika hospitali ya Agostino Gemelli, Roma asubuhi ya leo tarehe 14 Februari 2025, mwishoni mwa mikutano yake iliyokuwa imepangwa “alifanya vipimo vya kitaalam na kuanza matibabu ya dawa katika hospitali.” Haya yaliripotiwa katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, ikifahamisha kwamba “vipimo vya kwanza viliyofanywa vilioniesha kuwa ana maambukizi ya njia ya upumuaji.”
Hata hivyo Hali ya kliniki ya Papa “ni njema, anayo homa kidogo,” kwa mujibu wa maelezo ya Msemaji wa Vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni na kuongeza kwamba " Papa alikuwa mtulivu, mwenye roho tulivu na alikuwa amesoma baadhi ya magazeti.”