Papa alazwa hospitali ya Gemelli kwa vipimo na matibabu ya ugonjwa wa Mkamba
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican, Ijumaa tarehe 14 Februari 2025 imebainisha kuwa: "Leo asubuhi, mwishoni mwa mikutano, Papa Francisko alilazwa katika hospitali ya Agostino Gemelli kwa ajili ya vipimo muhimu vya uchunguzi na kuendelea na matibabu katika mazingira ya hospitali kutokana na Mkamba (bronchitis) ambao bado anaendelea kuwa nao kwa siku hizi."
Kwa siku kadhaa Papa Francisko mwenyewe alikuwa amezungumza hadharani kuhusu ugonjwa wa Mkamba(Bronchitis) ambao haukumruhusu kila mara kusoma katekesi , mahubiri na hotuba zake zilizotayarishwa kwa ukamilifu. Kwa njia hiyo subuhi ya siku ya Ijumaa aliweka ajenda za mipango iliyopangwa kuwa sawa na yote iliyofanyika katika Nyumba ya Mtakatifu Marta. Hii ni mara ya nne kwa Papa Francisko kulazwa katika hospitali kuu ya Kirumi ya Agostino Gemelli.