Papa Hospitalini Gemelli amelala vizuri usiku
Vatican News
“Papa amelala vizuri na sasa yuko anapumzika.”
Ndilo sasisho la siku ya Alhamisi asubuhi tarehe 27 Februari 2025 kutoka katika Ukumbi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican, kwa waandishi wa habari kuhusiana na hali ya afya ya Baba Mtakatifu Francisko aliyelezwa katika Hospitali ya Agostino Gemelli, Roma tangu tarehe 14 Februari 2025.
Sasisho la Jumatano tarehe 26 Februari usiku
Taarifa ya jana usiku tarehe 26 Februari 2025 ilibanisha kuwa: "Hali za kimatibabu za Baba Mtakatifu kwa saa 24 zilizopita zimeonesha kuboreka kidogo zaidi. Upungufu mdogo wa kufanya kazi kwa figo uliokuwapo katika siku za hivi karibuni umepungua. Uchunguzi wa kipimo cha “CT scan” katika kifua, uliofanywa jana jioni, ulionesha mageuzi ya kawaida ya kuvimba kwa mapafu. Vipimo vya damu vya leo na hesabu kamili ya damu kimaabara vimethibitisha uboreshaji kuliko jana. Baba Mtakatifu anaendelea na tiba ya oksijeni yenye mtiririko wa juu. Hata leo hii hakuwasilisha matatizo yoyote ya kupumua. Mazoezi(Physiotherapy) ya kupumua yanaendelea. Hata kama kuna unafuu kidogo, ubashiri bado umehifadhiwa. Wakati wa asubuhi Baba Mtakatifu alipokea Ekaristi. Na lasiri ilitengwa kwa ajili ya shughuli za kazi ndogo."