杏MAP导航

Tafuta

Papa Francisko anaendelea na matibabu katika Hospitali ya A. Gemelli Roma. Papa Francisko anaendelea na matibabu katika Hospitali ya A. Gemelli Roma.  (ANSA)

Papa Hospitalini Gemelli,hali inaboreka.Kushindwa kidogo kwa figo kumetulia

Uchunguzi wa kipimo cha “CT Scan”ulionesha mageuzi ya kawaida ya kuvimba kwa pafu,vipimo vya damu vilikuwa vizuri.Mchana Papa Francisko aliendelea na shughuli zake ndogo.Utabiri unabaki kuhifadhiwa.

Vatican News

"Hali za kimatibabu za Baba Mtakatifu kwa saa 24 zilizopita zimeonesha kuboreka kidogo zaidi. Upungufu mdogo wa kufanya kazi kwa figo uliokuwapo katika siku za hivi karibuni umepungua. Uchunguzi wa kipimo cha “CT scan” katika kifua, uliofanywa jana jioni, ulionesha mageuzi ya kawaida ya kuvimba kwa mapafu. Vipimo vya damu vya leo na hesabu kamili ya damu kimaabara vimethibitisha uboreshaji kuliko jana.

Baba Mtakatifu anaendelea na tiba ya oksijeni yenye mtiririko wa juu. Hata leo hii hakuwasilisha matatizo yoyote ya kupumua. Mazoezi (Physiotherapy) ya kupumua yanaendelea. Hata kama kuna unafuu kidogo, ubashiri bado umehifadhiwa. Wakati wa asubuhi Baba Mtakatifu alipokea Ekaristi. Na lasiri ilitengwa kwa ajili ya shughuli za kazi ndogo."

Haya ndiyo yaliyoripotiwa kwenye taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican, iliyotolewa jioni ya leo Jumatano, tarehe 26 Februari 2025 kuhusiana na afya ya Baba Mtakatifu  ambaye amelazwa kwa siku kumi na mbili (tangu 14 Februari)katika hospitali ya A.Gemelli, Roma.

Idadi kubwa ya barua, michoro, maua, wakati huo huo, zimefika na zinaendelea kumfikia katika siku hizi kwa Baba Mtakatifu.

26 Februari 2025, 19:40