MAP

Papa kwa Jubilei ya Vikosi vya Wanajeshi:kwa kupanda mitumbwi mnatoa ulinzi wetu na kututia moyo!

Baba Mtakatifu aliongoza Misa ya Jubilei ya vikosi vya kijeshi,Polisi na usalama,Februari 9 na kusisitiza thamani yao katika mapambano dhidi ya uhalifu na aina mbalimbali za vurugu,kulinda kazi ya uumbaji,kuhamasisha amani na kuwaomba wasijenge roho ya vita bali wawe upande wa uhalali na wema unaoweza kushinda licha ya kila kitu.Yesu alitazama,alipanda na kuketi na ndiyo hatua ya Mungu ndani ya ugumu wa maisha ya mwanadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika maadhimisha ya Misa Takatifu Dominika tarehe 9 Februari 2025, katika Dominika ya 5 ya Mwaka C, Baba Mtakatifu Francisko aliongoza misa hiyo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, akisadiwa na Kardinali Robert Francis Prevost,(OSA), Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu, pamoja na Askofu  Santo Marcianò, Mwakilishi wa Vatican katika Jeshi la Italia na Askofu Mkuu Gintaras Grušas wa Vilnius, ambaye ni Rais wa Mabaraza la Maaskofu wa Ulaya(CCEE). Kwa mujibu wa taarifa, ya washiriki wa misa hiyo imeeudhuriwa na waamini karibia 25,000, ikiwa ni Jubilei ya Ulimwengu wa Majeshi, Polisi na vyombo vyote vya Usalama kutoka Ulimwenguni kote.

Baba Mtakatifu Francisko baada ya masomo ya Somo la kwanza: Nabii (Isaya 6,1-2, .3-8),  (Zaburi,137),  somo la Pili  (1Kor 15,1-11) na Injili ya Luka (Lk 5:1–1), alianza  kujikita na Injili akisema: “Mtazamo wa Yesu kwenye ziwa la Genesareti unaelezewa na Mwinjili kwa vitenzi vitatu: ‘alitazama, akapanda na akaketi.’ Yesu alitazama, Yesu alipanda, na Yesu akaketi.” Yesu hajishughulishi na kuonesha sura yake kwa umati, hajishughulishi na kutekeleza kazi fulani, kwa kufuata ratiba katika utume wake; kinyume chake, yeye daima huweka mahali pa kwanza kukutana na wengine, uhusiano, wasiwasi wa jitihada hizo na kushindwa ambazo mara nyingi hulemea moyo na kuondoa matumaini. Kwa sababu hiyo, siku ile Yesu “alitazama, akapanda na kuketi.”

Jubilie ya ulimwengu wa majeshi
Jubilie ya ulimwengu wa majeshi   (Vatican Media)

Baba Mtakatifru Francisko alidadavua vitenzi hivyo: Kwanza kabisa Yesu alitazama. Yeye ana mtazamo wa  uangalifu ambao, hata katikati ya umati kama huo, yaliwezesha kuona mitumbwi  miwili iliyokuwa imewekwa kwenye ufuko na kuona kukata tamaa kwenye nyuso za wavuvi hao, ambao sasa walikuwa wakiosha nyavu zao tupu baada ya usiku mbaya. Kwa hiyo Yesu anatutazama kwa huruma. Papa Francisko alikazia kusisitiza kuwa “Tusisahau hili: Huruma ya Mungu yaani mielekeo mitatu ya Mungu ni ukaribu, huruma na upole. Kwani Mungu yu karibu, Mungu ni mpole, na Mungu ni mwenye huruma, daima.” Naye Yesu alilekeza macho hayo ya huruma machoni pa watu hao, wakiwa wamevunjika  moyo na kuwa na  mfadhaiko wa kufanya kazi usiku kucha bila kuvua chochote,  wa hisia ya kuwa na moyo mtupu sawa na nyavu hizo ambazo sasa zilikuwa tupu mikononi mwao. Baada ya kusema hayo Baba Mtakatifu aliomba radhi ya kutoendelea kusoma na kumuomba Mshereheshaji ili aweze kuendelea kusoma  tadakari hiyo kwa sababu ya ugumu wa kupumua.

Katika tafakari ya Injili hii “Naye Yesu alipoona taabu yao, alipanda juu. Alimwomba Simoni aondoe mtumbwi kwenda mbali na ardhi na kupanda huku, akiingia kwenye nafasi ya maisha yake, na akiingia kwenye tabia ya kushindwa iliyokaa  moyoni mwake. Hili ni zuri: Yesu hajiwekei kikomo kwa kutazama mambo ambayo hayaendi vizuri, kama tunavyofanya mara nyingi, na kuishia kujifunga wenyewe kwa malalamiko na uchungu. Badala yake, anaanza hatua, anakwenda kukutana na Simone, anasimama naye katika wakati huo mgumu na anaamua kuingia kwenye mtumbwi wa  maisha yake, ambayo usiku huo alirudi ufukweni bila mafanikio. Hatimaye, mara alipopanda juu, Yesu aliketi. Katika Injili, huo ndiyo mkao wa kawaida wa mwalimu, wa yule anayefundisha. Kiukweli Injili inasema kwamba aliketi na kufundisha. 

Jubilie ya wanajeshi,polisi na vyombo vyote vya usalama duniani
Jubilie ya wanajeshi,polisi na vyombo vyote vya usalama duniani   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Baada ya kuona uchungu machoni na mioyo ya wavuvi hao kwa usiku wa kazi ngumu iliyoharibika, Yesu alipanda mtumbwi ili kufundisha, yaani, kutangaza habari njema, kuleta nuru katika usiku huo wa kukatishwa tamaa, kusimulia uzuri wa Mungu ndani ya taabu za maisha ya mwanadamu, kuwafanya watu wahisi kwamba bado kuna tumaini hata wakati kila kitu kinaonekana kupotea. Na kisha muujiza hulitokea: wakati Bwana anapanda ndani ya mitumbwi ya maisha yetu ili kutuletea habari njema ya upendo wa Mungu ambayo daima inatusindikiza na kutuimarisha, basi maisha huanza tena, tumaini linazaliwa upya, shauku iliyopotea inarudi na tunaweza tena kutupa wavu baharini.

Akigewaukia wanahija kutoka ulimwengu wa majeshi, Baba Mtakatifu alikazia  kusema kuwa neno hili la matumaini linatusindikiza siku ya leo, tunapoadhimisha Jubilei ya Majeshi, Polisi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, na kwa hiyo amewashukuru kwa  utumishi wao, akitoa salamu kwa Mamlaka zote zilizokuwapo, Jumuiya na Vyuo vya Kijeshi, pamoja na Wanajeshi na Mapadre wanaotoa huduma ya katika taasisi hizi za usalama. Dhamira kuu imekabidhiwa kwao, ambayo inajumuisha nyanja nyingi za maisha ya kijamii na kisiasa: ulinzi wa nchi zetu, dhamira ya kulinda usalama, ulinzi wa uhalali na haki, uwepo wa magereza, mapambano dhidi ya uhalifu na aina mbalimbali za vurugu zinazohatarisha kuvuruga amani ya jamii. Na pia Papa alikumbuka wale wanaotoa huduma yao muhimu katika majanga ya asili, kwa ulinzi wa kazi ya uumbaji, kwa kuokoa maisha baharini, kwa hali dhaifu zaidi, na kwa kuhamasisha amani. Bwana pia anawaomba wafanye kama anavyofanya wa: kutazama, kupanda, na kuketi.

Jubilei ya Ulimwengu wa Usalama
Jubilei ya Ulimwengu wa Usalama   (Vatican Media)

Awali yayote kutazama, kwa sababu wao wameitwa kuwa na mtazamo wa makini, ambao unaweza kufahamu vitisho kwa manufaa ya wote, hatari zinazokabili maisha ya raia, hatari za kimazingira, kijamii na kisiasa ambazo tunakabiliwa. Pili kupanda: ni kwa sababu sare zao, nidhamu ambayo imewatengeneza, ujasiri unaokutofautisha, kiapo walichotoa, hayo yote ni mambo  ambayo yanawakumbusha jinsi ilivyo muhimu, na  siyo tu kuona uovu ili kuukemea, bali pia ni kupanda ndani ya mtumbwi  katika dhoruba na kujitolea ili usizame na utume katika huduma ya wema, uhuru na haki.

Na mwishowe, kuketi, kwa sababu uwepo wao katika miji na vitongoji vyetu, kuwep kwao  kila wakati upande wa uhalali na upande wa wanyonge, unakuwa fundisho kwetu sote kwamba “ unatufundisha kuwa uzuri unaweza kushinda licha ya kila kitu, inatufundisha kwamba haki, uaminifu na shauku ya raia bado ni maadili muhimu leo hii, inatufundisha kwamba tunaweza kuunda ulimwengu wa kibinadamu zaidi, wa haki zaidi na wa kidugu zaidi, licha ya nguvu zinazopingana za uovu. Na katika kazi hiyo, ambayo inakumbatia maisha yao yote, wanasindikizwa pia na Makanisa, uwepo muhimu wa makuhani kati yao.

Jubilei ya Ulimwengu wa  kulinda Usalama duniani
Jubilei ya Ulimwengu wa kulinda Usalama duniani   (Vatican Media)

Hawatohi huduma  kama ilivyotokea kwa huzuni nyakati fulani za kihistoria  katika  kubariki vitendo potovu vya vita. Hapana! Badala yake wako miongoni mwao  “kama uwepo wa Kristo, ambaye anataka kuwasindikiza wao, wanawapa usikivu wa kusikiliza na ukaribu, wanatia moyo kwenda kilindini na kuwasaidia katika utume wanaofanya kila siku. Kama usaidizi wa kimaadili na wa kiroho, wanatembea njiani pamoja nao, wakiwasaidia kutekeleza majukumu yao katika mwanga wa Injili na katika huduma ya wema.

Papa Francisko anawashukuru kwa  kile wanachofanya, wakati mwingine katika hatari ya kibinafsi. Asante kwa kuingia ndani ya mitumwi yetu katika dhiki, kutupatia ulinzi wao na kututia moyo wa kuendelea na safari yetu. Lakini pia Papa alipenda kuwasihi wasipoteze lengo la huduma yao na matendo yao: kuendeleza maisha, kuokoa maisha, kutetea maisha daima. Na amewaomba tafadhali wawe makini   dhidi ya jaribu la kuchochea roho ya vita; kuwa makini ili wasishawishiwe na historia ya nguvu na kelele za silaha; kuwa makini  ili kamwe wasichafuliwe na sumu ya propaganda ya chuki, ambayo inagawanya ulimwengu kuwa marafiki wa kutetewa na maadui wa kupigana. Badala yake, wawe mashuhuda jasiri wa upendo wa Mungu Baba, ambaye anataka sisi sote tuwe ndugu. Na kwa pamoja, tutembee kujenga enzi mpya ya amani, haki na udugu.

Papa mahubiri 9 Februari
09 Februari 2025, 11:44