ĐÓMAPµĽş˝

Waamini wanasali kwa ajili ya Papa. Waamini wanasali kwa ajili ya Papa.  (ANSA)

Papa Francisko:vita vya Ukraine ni uchungu na aibu ya ubinadamu

Papa aliyelazwa katika hospitali ya Gemelli,aliwasilisha Ujumbe wake wa Sala Malaika wa Bwana Dominika 23 Februari uliotangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican.Katika maandishi,anawasalimu washiriki wa Jubilei ya Mashemasi kuwashukuru wafanyakazi wa afya huko Gemelli kwa utunzaji wao pamoja na waamini,hasa watoto kwa upendo wao.Amekumbuka miaka 3 ya vita nchini Ukraine na kusasisha ukaribu wake na watu wa Kiukraine wanaoteswa na wito kuombea nchi zingine.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu  Francisko aliyelazwa katika hospitali ya Gemelli tangu tarehe 14 Februari, aliwasilisha  Ujumbe wake wa Sala Malaika wa Bwana Dominika tarehe 23 Februari 2025  uliotangazwa  na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican. Katika maandishi yakePapa anabainisha kuwa: Kaka na dada, Dominika njema.  â€śAsubuhi ya leo katika Basilika ya Mtakatifu Petro, imeadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuwawekwa wakfu baadhi ya wakandidati wa wakishemasi. Ninawasalimia wao na washiriki wa Jubilei ya Mashemasi ambao kwa siku hizi wamekuwa Vatican;  Ninashukuru Mabaraza ya Kipapa kwa ajili ya Makleri na kwa ajili ya Unjilishaji kwa maandalizi ya tukio hilo.”

Msiogope kuhatarisha upendo

Papa akiwageukia mashemasi hao anaeleza kuwa: “Ndugu wapendwa mashemasi, ninyi mnajikita katika kutangaza Neno na katika huduma na huruma ya Mungu kwa wote.  Ninawahimiza muendelee kwa furaha utume wenu na kama inavyotushauri Injili ya leo, ya kuwa ishara ya upendo ambao unawakumbatia wote, unaobadilisha ubaya kwa wema na kuzaa Ulimwengu wa kidugu. Msiogope kuhatarisha upendo!”

Shukrani kwa huduma huko Gemelli

Akifafanua kuhusu afya yake, Papa anabainisha “Kwa upande wangu, ninaendelea kwa imani kulazwa katika Hospitali ya Gemelli, kwa kupeleka mbele  matibabu ya lazima; na hata kupumziko ni sehemu ya matibabu! Ninawashukuru kwa moyo madaktari na wafanyakazi wa afya, wa Hospitali hii kwa umakini ambao wananionesha na kwa kujikita na huduma zao kati ya watu wagonjwa.”

Miaka mitatu ya vita Ukraine

Baba Mtakatifu Francisko akirejea juu ya kumbukizi ya vita vya Ukraine na Urusi vilivyoibuka tangu tarehe 24 Februari, alibainisha: "Miaka mitatu ya vita  inatimia kesho(Jumatatu 24 Februari) iliyowakumba ukraine. Ni  Siku ya uchungu na aibu kwa ubinadamu mzima! Wakati ninasasisha ukaribu wangu kwa watu walioteseka huko Ukraine, ninawaalika kukumbuka waathirika wa migogoro yote ya kisilaha na kusali kwa ajili ya zawadi ya amani nchini Palestina, nchini Israel na Mashairiki ya Kati, huko Myanmar, Kivu na  Sudan.”

Shukrani kwa maombi na ujumbe aliopokea Papa

Baba Mtakatifu aidha akifikiria maombi kutokana na kulazwa kwake hospitalini amebainisha: “Katika siku hizi zimenifikia jumbe nyingi za upendo na zimenishangaza kwa namna ya pekee barua na michoro ya watoto. Ninawashukuru kwa ukaribu huu na kwa sala za kunitia nguvu ambazo nimezipokea kutoka Ulimwenguni kote! Ninawakabidhi nyote kwa maombezi ya Maria na kuwaomba kusali kwa ajili yangu.”

Ujumbe wa Papa kwa Agelus
23 Februari 2025, 13:23